Upinzani Tanzania una matatizo? Vyama havina Succession Plan hivyo vina Usultani! CHADEMA kuna Usultani? Usultani huu Utakiinua au Utakiangamiza?

Ukimaliza hili Paskali andaa la SISIEMU maana inakuwaje kuchagua mwenyekiti wa chama chao aruhusiwi mwanaccm kucompete na rais ambaye ccm wanasema by Default anakuwa mwenyekiti wa chama chao?
 
It is very difficult kuwa na succession plan kwenye hivi vyama vinavyoendeshwa kama mali binafsi. Baadhi yao vilianzishwa kama NGO na watu binafsi ambao wanaclaim wameinvest energy yao ya kutosha (fedha, muda, emotions, vipigo etc) na kwao kumuachia mtu mwingine achukue wakati hao “hawajavuna faida” inakuwa ngumu.

Cheyo, Lipumba, Mrema, Dovutwa, Rungwe, Mbowe

Ndio maana anapokuja mtu mgeni probably mwenye maono tofauti, ataitwa ‘pandikizi’ au ‘hana uchungu’ au ‘huyu hajui historia yetu’.
 
Muonee huruma paskali, amelazimishwa aandike kuhusu chadema, huenda kuna kabahasha, sijaona akiandika kuhusu mchakato wa hovyo uchaguzi hewa wa S/mitaa.
 
Hao wenyeviti wanachaguliwaje, je ni kwa demokrasia au ni kwa kuchagua kivuli na mtu. Demokrasia ni pamoja na wanachama kuruhusiwa kumchagua mwenyekiti wanaemtaka sio kwenda kumpigia kura mtu na kivuli, obvious mtu atapita tu maana hata mkichagua kivuli hakipo.

Wakati upi? Vyama vya siasa vya Tanzania hawana cha kuchekana wote wamejaa unafiki, ukitoa maoni unaonekana unawatukana viongozi, ni mambo ya ajabu.
 
Upinzani ni nini? Na mpinzani ni nani? Na nani ni mnufaika wa upinzani?
 
Sijui ni kwa kutojua historia au ni ulevi wa ushabiki wa kisiasa? Sikutegemea mtu kama wewe kuuliza maswali yasio na mashiko kama haya! Fuatilia kokote duniani watu wanapokuwa katika mapambano ama ya kutafuta uhuru au haki zao zinazoporwa na watawala mabeberu na madikteta mabadiliko ya uongozi katika vyama vya ukombozi hufanyika kwa mikakati maalum. Angalia Nyerere, Kenyatta, Samora, Kaunda, Mandela, Nujoma nk hawakubalishwa katika nafasi zao eti kwa sababu wamekaa kwa muda mrefu. Mabadiliko yo yote ambayo yangefanyika yangepunguza momentum ya mapambano kwa sababu wao walikuwa nembo ya mapambano na umoja.

Hali kadhalika hapa nchini kwa vyama vya upinzani kufanya mabadiliko ya uongozi eti kwa sababu wamekaa muda mrefu ni kuyumbisha mapambano ya kupigania demokrasia na hasa kwa utawala huu wa awamu ya tano unaodhamiria kuua vyama vya upinzani. Mabadiliko ya uongozi katika vyama vya upinzani yatafanyika kwa uangalifu mkubwa ambao hautaingiza mamuluki katika vyama hivyo ambalo ndiyo lengo kuu la CCM. Vyama vya upinzani havitaruhusu mashinikizo ya CCM katika kuweka viongozi wake. Ndiyo sababu hata CCM haijawahi kufanya uchaguzi wa Mwenyekiti wake wa Taifa kwa sababu ikiruhusu uchaguzi huo kuna uwezekano mkubwa wa Rais na Mwenyekiti kuingia katika mgogoro wa kutokuelewana. CCM itafanya uchaguzi wa Mwenyekiti wake pale tu itakapo ondoka madarakani! Kwa sasa embu nionyeshe succession plan ya CCM!
 
Makala inayofata, zungumzia Mchakato wa Uchukuaji na Urejeshaji form, kuenguliwa kwa Wagombea wa Upinzani kwa Makosa yanayofanana, zungumzia mpaka Uchaguzi wa Serikali za Mitaa!
 
Sina hakika kama una akili timamu!
Hivi mtu kama waitara mnaweza kumpa uongozi wa juu ktk chama chako?
 
Succession Plan ya CCM ndio ile ya kusukumizia watu uongozi? Au kwenda kwenye mkutano na majina mfukoni?

You are loosing my brother
 
Nenda shule jifunze juu ya "Succession Plan" umeandika tu
 
Pascal Mayalla
tatizo unafikiri kila mtu ni mjinga na unasahahu ni kwanini hali halisi ipo hivyo. hivi unafikiri bila yeye leo CDM ingekuw ahapo au ingeshakuwa NCCR and CUF au TLP?
Unasahahu ni kipi kilitokea NCCR ? TLP ? nahili la CUF juzi juzi tu ?

Then naomba unisaidie kwa nini Mwalimu Nyerere alikaa kwenye uenyekiti kwa kipindi chote hiki?

1. April 1953, he was elected president of the Tanganyika African Association (TAA)
2. 7 July 1954 TANU.
3. February 1977 ( Kwa kauli ya makongoro YUPOTUUU!!

na Msichotaka kusikia ni kuwa hata kipindi cha Nyerere ni wangapi walifukuzwa na kutengwa kwenye chama maana walikuw ahawaendani na malengo ya chama.
 
Succession Plan ya CCM ndio ile ya kusukumizia watu uongozi? Au kwenda kwenye mkutano na majina mfukoni?

You are loosing my brother

MKuu usishangae huyu ni mchumia tumbo na hali yake sionzuri japo ni wa kanda pendwa zile tender tender sikuhizi hakuna tena. kwahiyo muache ajipendekeze tatizo lake ni Aibu tu, mimi namshhuri ajitoe tu mazima na kujiunga na mfalme na hakuna atakaye mshangaa.
 

Nyerere kaaa miaka mingapi?
na kwanini?
Tokea 1953 TAA mpaka 1990's CCM ni mingapi hiyo na nikwanini? je hawakuwepo watu wenye uwezo ?

hivi huoni mazingira ya TAA, TANU na CCM ya nyerere yanfanana na mazingira ya sasa ya VYAMA PINZANI?

Au kwakuw atu sasa tuna mkoloni Mweusi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…