Wanabodi,
Hili ni bandiko la maswali yenye facts
- Jee kuna ubishi kuwa Upinzani Tanzania Unamatatizo?. Ni matatizo gani na usaidiweje?.
- Vyama vingi vya Upinzani Havina Succession Plan, kwanini vyama hivyo havina succession plan na sio tuu kwenye uongozi wa ndani, hata kwenye ubunge na udiwani, mfano tunaelekea uchaguzi wa 2020, Chadema ina wabunge wa majimbo ambao wengine wame deliver na wengine hawaja deliver, hivyo uchaguzi wa 2020, wengi wanakwenda kupigwa chini na CCM!. Kwanini hakuna succession plan ya ndani kuwapima kukubalika na kuwapiga chini kabla kwa kusimamisha more able candidates wanaokubalika zaidi?.
- Vingi ya Vyama vya Upinzani, Vina Uongozi wa Kisultani, na sio Chadema pekee, Mzee Cheyo wa UDP, Mrema wa TLP, Lipumba wa CUF, etc. Kwanini hakuna grooming mechanism to groom their future leaders?.
- Hivyo jee hata uongozi wa Mhe. Freeman Mbowe ndani ya Chadema, ni kama Usultani fulani?.
- Jee Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Chadema hiyo 18 Dec, ni uchaguzi kweli au ni uchaguzi kiini macho tuu?, kama utakavyokuwa Uchaguzi Mkuu wa 2020, tayari mshindi anajulikana!. Hivyo ni uchaguzi wa kukamilisha tuu taratibu kuonekane demokrasia amechukua mkondo wake? au ni uchaguzi kweli?.
- Kuna msemo, " no one is indispensable", no matter how good one is, huwa anafikia kiwango cha mwisho wa uwezo wake, ndio maana katiba unaweka ukomo wa uongozi, hata katiba ya Chadema ya 1992 ilikuwa na kipengele hicho, kwenye katiba ya 2006, kipengele hicho cha ukomo, kiliyeyuka, just vanish into thin air, bila kujadiliwa popote!. Jee kipengele hiki kiliyeyukaje?
- Waliokiweka kipengele hicho kwenye katiba ya Chadema, walikuwa na maana yao, kwa vile ile katiba ya 2006 kipengele hicho hakikuondolewa, bali kilijiondokea tuu chenyewe, kuondoka huku kwa kipengele hicho kuna maana gani kwa Chadema?.
- Je ni kwa kutokuwepo kwa kipengele hicho, cha ukomo ndiko kunatoa fursa ya usultani kwenye uongozi wa vyama vya siasa yenye Usultani, Jee Chadema nacho ni chama cha kisultani?, kuna Usultani?.
- Mkimfanyia Mhe. Mbowe a quick assessment tangu alipoitoa Chadema alipoingia kwenye uongozi mpaka hapa alipoifikisha Chadema, jee hakuna kweli wana Chadema wenye kuona mbali ambao wanao ona trends za Mhe. Mbowe kuwa japo amekifanyia mengi, makubwa na mazuri Chadema, lakini pia amefikia kiwango chake cha mwisho wa uwezo wake kwa Chadema kuhitaji kupata fresh blood?.
- Swali la mwisho na la msingi sana ni, jee kuendelea kwa Mhe. Mbowe kama Mwenyekiti wa Chadema, kwenye era hii ya changing political dynamism ya siasa za Tanzania chini ya JPM na CCM imara, Mwendelezo huu wa Uenyekiti wa Mhe. Mbowe, Jee Utakinua Zaidi Chadema kuliko hapo kilipofika, Au Utakiangamiza na sasa Chadema kinaelekea Kwishney?.
NB. Hili ni bandiko la maswali, kama una majibu ya maswali haya karibu, ukiwa huna, nakushauri jipitie tuu kimya kimya, sio lazima kuchangia kila thread.
Natanguliza shukrani.
Nawatakia Chadema maandalizi mema uchaguzi na wengine wote Jumapili Njema.
Paskali