Tatizo kubwa na utawala wa nchi ni CCM. Tatizo la uongoza mbaya ndanibya CCM ni CCM. Tatizo la uongozi ndani ya vyama vya siasa vya upinzani ni CCM.
CCM inaendesha siasa za hila, uwongo, udanganyifu, udikteta na kwa kiasi fulani siasa za kigaidi. Siasa ovu za CCM zinajenga hali ya kutoaminiana ndani ya vyama vya siasa vya upinzani kiasi kwamba wengi wafia vyama ndani ya vyama vya siasa vinaona aheri kubakia na viongozi hao hao wanaoaminika kuwa siasa mamluki na wasioweza kununulika kwa muda mrefu, hata kama hawataleta mabadiliko kuliko kumpa uongozi mtu ambaye kesho wakasikia ameunga mkono juhudi.
CCM itakapokuwa na siasa nzuri, itasababisha serikali kuwa na utawala mzuri, itasababisha vyombo vya ulinzi na usalama kusiamamia sheria na kutenda haki, mahakama kutoa haki na Bunge kufanya kazi mujibu wa katiba na kwa maslahi ya nchi. Mazingira hayo yatakapokuwepo, tutashuhudia uongozi na demokrasia kila mahali, pamoja na ndani ya vyama vya upinzani.
Kwa sasa CCM inanajisi kila mahali. Kila mahali inapakaza uchafu. Inanajisi vyombo vya ulinzi na usalama, inanajisi mfumo wa mahakama, inalinajisi Bunge mpaka taasisi za Elimu kiasi cha kuwa na wasomi wasiokuwa na akili kama hawa maprofesa wa majalalani, madokta wanaoweza kumtisha na kumwelekeza msajili wa vyama namna ya kufanya kazi, n.k.