Uchaguzi 2020 Upinzani ukimweka Membe itakuwa tofauti kubwa na ilivyokuwa kwa Lowassa! Watashinda

Uchaguzi 2020 Upinzani ukimweka Membe itakuwa tofauti kubwa na ilivyokuwa kwa Lowassa! Watashinda

Membe ni dhaifu kuliko hata Januari Makamba.

Na upinzani hatuhitaji wagombea wa kuokoteza.
 
Mkuu lowasa alikuwa ni national figure yule nje na hapo alikuwa na majority suport ya mikoa mitatu [kama unaakili utanielewa] hata kabla ya kampeni

Kiufupi itahitaji miaka mingine hamsini upinzani kupata mgombea mwenye ushawishi kama mzee lowasa
Nyie huko ni lini mtampata mzuri ambaye haitaji kubebwa na tume ya uchaguzi na ambaye ushindi wake hakutahitajika ma-ffu kutanda nchi nzima kabla na baada ya matokeo kutangazwa???
 
Washabiki wa Membe ni wanachadema, Lowasa alikuwa na washabiki ndani ya CCM na chadema wakawa nae, ila Membe atabaki na chadema peke yenu sasa sijui atapata kula laki sita za mbowe?
 
Mtaendelea kuhangaika na membe, na kusahau ni kitu gani mfanye kuelekea uchaguzi,
Hapa kuna mambo mawili

1=Membe amegundua muda unaisha lakini hakuna chama kimeonyesha kumpa nafasi ya kugombea uraisi sasa anafanya drama ili afukuzwe kisha mumuonee huruma mumpe ugombea Chadema.

2=Anawapotezea muda mshindwe kujipanga kuelekea uchaguzi kisha anaomba msamaha na kueleza ukweli kwamba ametumia vema jina kama mnavyomuita JASUSU MBOBEZI na kuacha upinzani ukiwa hoi,
Nacheka tu😂😂😂😂
 
Mbali na hivo pia membe Ni mtu wa system
Kule anao watu wake
Kwa hiyo kazi haitakua ngumu Kama kweli atasimama.
 
WashAbiki


Washabiki wa Membe ni wanachadema, Lowasa alikuwa na washabiki ndani ya CCM na chadema wakawa nae, ila Membe atabaki na chadema peke yenu sasa sijui atapata kula laki sita za mbowe?
Usijidanganye haloooo!
 
Washabiki wa Membe ni wanachadema, Lowasa alikuwa na washabiki ndani ya CCM na chadema wakawa nae, ila Membe atabaki na chadema peke yenu sasa sijui atapata kula laki sita za mbowe?
Bro nikurekebishe kwanza hakuna kitu "washabiki" Ni mashabiki.
Hicho tu Ndo kimefanya nisijibizane na wewe make inaonekana haujui kinachoendelea.
 
Bro nikurekebishe kwanza hakuna kitu "washabiki" Ni mashabiki.
Hicho tu Ndo kimefanya nisijibizane na wewe make inaonekana haujui kinachoendelea.
Kaa hivyo hivyo,mnajitoa ufahamu,
Zungumzieni tundu lisu na akina msigwa mnampa nani achana na mtu alishafukuzwa?
Kma mnakili kuwa wale mliowafukuza akina Rwakataele bado wana haki chadema basi Membe nae atakuwa na haki ingawa itakuwa ndogo sana,
Kama anpenda chama basi asubili ampigie kura Magufuri
 
Lowasa alikua na mambo 4
1 pesa zake zilikua saport
2 vingozi ndani yaserikali
3 matajiri wengi
4 ushawishi wa pande zote
 
Lowassa pamoja na kupendwa sana kwa kweli alikuwa dhaifu mno 2015. Tena mno, kimawazo (hakuwa na mvuto wa hoja) na hata kiafya (enzi za siha njema zilishampita). Kwangu mie hata JK kuhakikisha Lowassa hawi Rais ilikuwa ni kumsaidia rafiki yake ambaye alikuwa anajua undani wake. Lowassa asingeweza kuongoza vizuri na pengine hata afya yake ingetetereka zaidi na zaidi iwapo angekuwa Rais. Ni afadhali anavyoenenda kwa namana hii.

Ninawahakikishia Membe akibahatika kugombea kupitia upinzani - kuna uwezekano mkubwa sana wa upinzani kushinda uchaguzi ama kupata asilimia zaidi ya 40 za kura zote kwa Mwaka huu. Mwembe anakuja na approach nzuri, yaani analenga kupata msimamo wa kimataifa kuhusu chaguzi bora na zilizo huru (Fair and Free Election). Membe ameshaanza kuieleza Jumuiya ya Kimataifa kuwa Tume ya Uchaguzi ya Chama sio huru. Yaani ni MCCM halafu anajisema kuwa chombo cha kumpa ushindi yeye mwenyewe iwapo akipitishwa na CCM kugombea hakipo huru.

Ajabu sana kwani amekuwa akisema hili kwa muda tu na sio jana tu. Inawezekana kabisa huko huko Tume wanamtonya kuwa "Mkuu hatuko huru!". Sasa ukushaanza kuongelea kuwa Tume sio huru na kuvuta Jumuiya ya Kimataifa kwa jambo hilo ujue kuna watu unawaeleza siri zako za ndani na unawakaribisha waingilie. Kwa vyovyote vile iwapo Uchaguzi huu yatatokea maafa sio mbaya utawala huu kuja kuwajibishwa na vyombo va kimataifa hata kwa mauaji ya kimbari. Membe amelenga mbali sana - naamini akipata nafasi akaanza kuongea kwenye Kampeni atabadilisha sana upepo.

Membe akiongea kwa kukosoa Chama Chake kuhusu ujenzi wa mamiundo mbinu bila kujali hali za kipato kwa wananchi na kutamka wazi wazi wafanyakazi wamenyanyasika ni nani hatamsikia. Membe akitoa hadi njema kwa wananchi dhidi ya habari za kujenga mamiundombinu za awamu hii nani atasikiliza mambo ya mamiundo mbinu. Membe akieleza kwa ufasaha kuhusu zao la korosho lilivyodukuliwa na kuwasababishia wananchi wake ni nani hatamwelewa?

Membe akiongelea kupotea kwa akina Ben Saa Nane kwa kutoa siri anayoijua kuhusu hilo nani hatavutiwa naye? Membe akiongelea na kuwataja walimtwanga Tundu Lissu mirisasis kibao, ni nani hatamwelewa? Kumbukeni unaweza kutenda mema mengi lkn ukatenda baya moja tu likakuangusha katika maisha yako yote ya kutenda mema. hebu mchuku askofu aliyeponya wat na watu, siku ikatokea bahati mbaya tu akambaka muumini si na uaskofu wake anaweza kuukosa?

Mie ninaamini kabisa sasa CCM inaelekea kudondoka kwa kishindo kikubwa sana. Iwapo CCM itashinda mwaka huu basi itakuwa imeshinda kwa mbinde sana. Na isiposhinda itakuwa imejitakia yenyewe kwani asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Wananchi walikuwa wana mengi ya kusikilizwa na awamu hii - yamepuuzwa kwa kiburi cha kufikiri ni awamu inayopendwa kumbe ni hovyo kabisa na imejawa na udikiteta lukuki.
Agomber kupitia CCM au upinzani, Membe hafai kwa urais kwani ni muongo wa kupitiliza na mbinfasi wa hali ya juu
 
Tatizo kubwa ambalo upinzani wanalo ni kuhusu ruzuku maana watapata kidogo sana kipindi hiki kwa sababu ya yaliyofanyika na ambayo Watanzania wanategemea kufanyika na kukamilika chini ya JPM na CCM.

1592761948715.png


Hapa kazi tu!
 
Mkuu lowasa alikuwa ni national figure yule nje na hapo alikuwa na majority suport ya mikoa mitatu [kama unaakili utanielewa] hata kabla ya kampeni

Kiufupi itahitaji miaka mingine hamsini upinzani kupata mgombea mwenye ushawishi kama mzee lowasa
Umechambua vizuri lowassa 2015 hakuwa mtu sahii wakuiangusha ccm
2015 Lowassa alikuwa puppet wa CCM
Lowassa alishinda ila bao la mkono ndio liliharibu kila kitu. Membe ana kazi yake nyie subirini.
 
CCM kuendelea kutawala nchii hii,kama waliweza kuvuka 2015 mwaka huu wanatiririka tuu.Ni ngumu 2020 kuwashinda CCM na ninavyoona bunge lijalo kijani kutawala mno
 
CCM kuendelea kutawala nchii hii,kama waliweza kuvuka 2015 mwaka huu wanatiririka tuu.Ni ngumu 2020 kuwashinda CCM na ninavyoona bunge lijalo kijani kutawala mno
Oktoba urudi tena kuthibitisha uzi kwa neno moja tu "NILISEMA"
 
CCM kwa sasa inachukiwa kuliko kipindi kingine chochote. Lakini pia ni kipindi hiki ambacho Serikali imetenda mambo yake kwa kutumia nguvu bila ushawishi kuliko wakati wowote. Ni wakati huu kumekuwa na ugandamizaji na uonevu kuliko kipindi chochote. Ni kipindi hiki watu wamekoseshwa haki ya kunena kwa uhuru, hali ambayo imezalisha wanafiki wa kusifu mdomoni, na kulaumu mioyoni.

Hali ya sasa ya CCM siyo ya kujivunia kwa namna yoyote ile kwa chama cha kisiasa. Mizizi ya CCM imekauka, inaishi kwa kushikiliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom