Amin nakuambia,
wako watu wenigi ndani ya CCM hufuata maslahi tuu kwa vile wamelazimishwa ili wapate ajira.
Kiukweli idadi yao inaongezeka kila uchao na siku ya kuizamisha CCM ikifika ,hao ndio watakao kididimiza kichwa cha CCM ndani ya maji makuu isiibuke tena.
Hata wana CCM wenyewe wamekichoka chama chao ,kila siku wimbo ni ule ule wa ulaghai,
Hatimae Maisha yao yanazidi kuwa magumu
Hebu fikiria ! ni CCM wangapi walivunjiw nyumba zao pale jangwani,kimara,kibamba na kwengineko bila malipo hata kupewa kiwanja?
Hivi leo hakuna mtumishi hata mmoja wa umma aliye na amani, Hata hao wakuu wa mikowa au mawaziri wakijua wazi kuwa muda wowote ule wanaweza kutumbuliwa bila ya huruma na kuvunjiwa heshima zao hadharani.Pengine kwa makosa madogo na yasiyowahusu wao moja kwa moja.
Hivi unadhani U ccm wa Membe, Kinana, Nape na wengineo ni uleule wa zamani? ujuwe lazima wapo pale kimaslahi tuu.
Muda ukifika , na muda ndio huu CCM inakwenda zake KUZIMU bila kurudi, Kiburi cha CCM na Makufuru yao yamezidi mno.
Si dhani kama Mungu atawapa tena Upendeleo.
Kujigamba kuwa Utakuwepo Milele hii ni kufuru
Kujiita wewe Nabii, Chaguo la Mungu n.k hizi zote ni kufuru .
SUPRISE iko karibu wana CCM jiandaeni kiskolojia ,na wengi wataihama nchi, maana wanajua Madhambi waliyowafanyia watanzania.
Ndani ya vyombo vya dola pia wapo watu tofauti, wengi waoni wale wasioridhishwa na mfumo kandamizi ,ila wafanyije?
Siku ikifika Hao ndio watakuwa muhimilimkubwa wa mageuzi.
Naihurumia Tanzania yangu, Maana CCM wametengeneza bomu la kutega, siku likitumbuka hali itakuwa mbaya sana.
Si jui nani ataituliza hali.
Chuki zimepandikizwa nyingi mno.
Hali ya Ubaguzi ,na Maonevu , ya visasi
Sikuhiyo hali siui itakuwaje