Uchaguzi 2020 Upinzani ukimweka Membe itakuwa tofauti kubwa na ilivyokuwa kwa Lowassa! Watashinda

Tatizo kubwa ambalo upinzani wanalo ni kuhusu ruzuku maana watapata kidogo sana kipindi hiki kwa sababu ya yaliyofanyika na ambayo Watanzania wanategemea kufanyika na kukamilika chini ya JPM na CCM.

View attachment 1485424

Hapa kazi tu!
Hao vijana naona wamekosa elimu. Bango lenye maneno machache kama hilo, lina makosa kibao ya kiuandishi.

Kiongozi usiwategemee sana wajinga, wategemee watu werevu. Mjinga akieleweshwa na akaelewa hawezi kuendelea kuunga mkono alichokuwa akikiunga mkono wakati wa ujinga.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu lowasa alikuwa ni national figure yule nje na hapo alikuwa na majority suport ya mikoa mitatu [kama unaakili utanielewa] hata kabla ya kampeni

Kiufupi itahitaji miaka mingine hamsini upinzani kupata mgombea mwenye ushawishi kama mzee lowasa
Kuna siku hata magufuli mtaanza kumponda wanafiki bhana
 
Tatizo kubwa ambalo upinzani wanalo ni kuhusu ruzuku maana watapata kidogo sana kipindi hiki kwa sababu ya yaliyofanyika na ambayo Watanzania wanategemea kufanyika na kukamilika chini ya JPM na CCM.

View attachment 1485424

Hapa kazi tu!
Mbona anaogopa watu kumu challenge?
 
Kuna rafiki yangu mmoja hupendelea kusema "Mungu (ni) fundi" akimaanisha "never say never". Mambo yanaweza kubadilika kwa namna ambavyo wengi hatukutarajia. Tumuachie Mungu tu.

By the way, najaribu kufikia kauli za Membe za hivi karibuni kuhusu kukiukwa taratibu za kufukuzwa ccm na uwezekano wa yeye kugombea ......amechagua maneno sana, ametumia sana nafsi ya "wingi"....."Sisi......!" Wapo yeye na nani?
 
Ni kweli BM anaweza kuitikisa sana CCM, hili hata wao wanalijua! .....Anaifahamu CCM na anaujuwa udhaifu wake lakini zaidi ya yote ana ushujaa na ujasiri ambao wana CCM wengi hawana, Tena anaweza kuongea bila kumung'unya maneno!
Vuta picha kwa mfano katika kampeni zake akataja mauzauza kibao ndani ya ccm yakiwemo mipango ovu ya kununua wapinzani n.k. Akaja kwa wanafunzi vyuo vikuu awambie anapunguza makato ya Bodi ya mikopo toka 15% hadi 5%, na pia mwanachuo ukimaliza chuo utapewa 2miln za kuanzia ujasiriamali na makato yake yanajuishwa hapohapo kwenye hiyo 5%! Je hapa si wanafunzi wote na wanufaika watamuunga mkono! Vuta picha awaambie watumishi atawalipa nyongeza zote za mishahara ya miaka 5 waliyodhulumiwa na serikali ya jiwe na kuanzia hapo nyongeza ya mshahara itakuwa kama kawa! Unazani wafanyakazi watamuangusha? Hebu vuta picha aje na ajenda ya kuhakikisha wafanyabiashara wote walionyanyaswa na serikali wanapata haki zao, hivi mfanyabiashara gani atamtupa! Hebu vuta picha aje na ishu ya kuwalipa fidia wananchi wote Tanzania nzima waliokwishabomolewa nyumba zao bila kulipwa chochote, Je hapa wananchi watamuacha? Aje na ishu ya kukomboa wakulima wa korosho, Pamba, ufuta na mazao mengine, Je hapa wakulima watamtosa kweli?.....Kwa hakika BM anaweza kuleta upinzani mkali sana na hata kuiondosha CCM madarakani na watu wasishangae!
 
Mkimweka mamluki kutoka ccm tena aje agombee kupitia vyama vya upinzani ndio itakuwa mwisho wangu kuamini upinzani,sio kwa usaliti alioufanya lowasa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Good!
 
Mkuu lowasa alikuwa ni national figure yule nje na hapo alikuwa na majority suport ya mikoa mitatu [kama unaakili utanielewa] hata kabla ya kampeni

Kiufupi itahitaji miaka mingine hamsini upinzani kupata mgombea mwenye ushawishi kama mzee lowasa
Ujinga kabisa na upuuzi. Miaka hamsini ya kumpata mtu kama Lowassa? Kwa kitu gani special alichokuwa nacho? Sidhani na siamini kabisa kuwa kama taifa tumeishiwa kiasi hicho. Lowassa alikuwa wa kawaida tu na tena kawaida sana na kilichompandisha ni promo tu za Team Lowassa. Hakuwa presidential material kiivo kama unavyotushawishi. Na kwangu binafsi naona hakufikia upepo wa Dkt Slaa alipogombea urais.
 
Si ndiyo Mimi nashangaa yani Jambo dogo Kama hilo mpaka tutumie nguvu kubwa kulielezea? Hana impact yoyote ile ni bora wakomae wenyewe inaweza leta mashiko wakimchukua tu wameharibu tena zaidi
 
Wewe unazijua siasa. Ni kweli ulio dhahiri kuwa Lowasa hakuwa presidential materia kama walivyo akina Tundu Lissu, Membe na Zitto kwa sasa!
 
Duh!
Hii story INACHEKESHA!
 
2015 Lowassa alikuwa puppet wa CCM
Hapo ndipo ninapoiheshimu CCM.
Waliisoma CHADEMA wakajua pale wakufanya nao biashara ni MBOWE na LISSU tu. Wengine wote ni misukule, itafuata chochote kitakachoamliwa.
Wakapiga dili, dili likatiki wakaacha MISUKULE ikikunja ngumi na kuzungusha. GAME OVER!
 
Amin nakuambia,
wako watu wenigi ndani ya CCM hufuata maslahi tuu kwa vile wamelazimishwa ili wapate ajira.
Kiukweli idadi yao inaongezeka kila uchao na siku ya kuizamisha CCM ikifika ,hao ndio watakao kididimiza kichwa cha CCM ndani ya maji makuu isiibuke tena.
Hata wana CCM wenyewe wamekichoka chama chao ,kila siku wimbo ni ule ule wa ulaghai,
Hatimae Maisha yao yanazidi kuwa magumu
Hebu fikiria ! ni CCM wangapi walivunjiw nyumba zao pale jangwani,kimara,kibamba na kwengineko bila malipo hata kupewa kiwanja?
Hivi leo hakuna mtumishi hata mmoja wa umma aliye na amani, Hata hao wakuu wa mikowa au mawaziri wakijua wazi kuwa muda wowote ule wanaweza kutumbuliwa bila ya huruma na kuvunjiwa heshima zao hadharani.Pengine kwa makosa madogo na yasiyowahusu wao moja kwa moja.
Hivi unadhani U ccm wa Membe, Kinana, Nape na wengineo ni uleule wa zamani? ujuwe lazima wapo pale kimaslahi tuu.
Muda ukifika , na muda ndio huu CCM inakwenda zake KUZIMU bila kurudi, Kiburi cha CCM na Makufuru yao yamezidi mno.
Si dhani kama Mungu atawapa tena Upendeleo.
Kujigamba kuwa Utakuwepo Milele hii ni kufuru
Kujiita wewe Nabii, Chaguo la Mungu n.k hizi zote ni kufuru .
SUPRISE iko karibu wana CCM jiandaeni kiskolojia ,na wengi wataihama nchi, maana wanajua Madhambi waliyowafanyia watanzania.
Ndani ya vyombo vya dola pia wapo watu tofauti, wengi waoni wale wasioridhishwa na mfumo kandamizi ,ila wafanyije?
Siku ikifika Hao ndio watakuwa muhimilimkubwa wa mageuzi.
Naihurumia Tanzania yangu, Maana CCM wametengeneza bomu la kutega, siku likitumbuka hali itakuwa mbaya sana.
Si jui nani ataituliza hali.
Chuki zimepandikizwa nyingi mno.
Hali ya Ubaguzi ,na Maonevu , ya visasi
Sikuhiyo hali siui itakuwaje
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…