Upinzani wa Tanzania ni wa vimatukio, Rais Samia ameumaliza kisayansi

Wewe kila ukilala unaota CHADEMA tu. Huna shughuli nyingine?. Unasema Samiah ameudhoofisha upinzani wakati Jana tu msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA umezuiliwa na polisi.

 
Wewe kila ukilala unaota CHADEMA tu. Huna shughuli nyingine?. Unasema Samiah ameudhoofisha upinzani wakati Jana tu msafara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA umezuiliwa na polisi.
Kwani msafara ungendelee mbele ndio ungeondoa ukweli kuwa upinzani hauna nguvu kwa Sasa hapa nchini, Fuateni taratibu za kisheria mnapotaka kufanya Jambo lolote lile la kisiasa
 

Dah haya maneno mazuri sana, huyo jamaa atakua chizi katoroka mirembe
 
Dah haya maneno mazuri sana, huyo jamaa atakua chizi katoroka mirembe

Dah haya maneno mazuri sana, huyo jamaa atakua chizi katoroka mirembe
Imebidi nimwandikie hivyo kutokana na heading aliyoileta.

Heading inazungumzia UPINZANI WA TANZANIA hhalafu mbele kwenye yakiyomo anampaka Rais mafuta kwa mgongo wa chipa.

Katika Uzi huo hajatanabaisha Upinzani wa Tanzania katika Nini? Tanzania hatuna Upinzani wa maendeleo Ila tuna Upinzani wa kisiasa ambako tunapingana katika sera, itikadi na namna bora ya kuendesha nchi. Yote haya yakiwa na azma Moja TU ya kuwaletea wananchi maendeleo.

Wazee wetu walipoubali mfumo wa vingi hawakukaribisha uhaini nchini kama ambavyo ccm mambo Leo na. Washamba wa kisiasa wanavyojaribu kuwaaminisha wasiojua siasa kwamba Upinzani ni uhaini na kuamua kutumia vyombo vya dola kuharamisha Upinzani nchini.

Ndio mtu kama huyu anakuja kwenye jukwaa akitokea FB anaanza kuandika UPINZANI WA TANZANIA badala ya Upinzani wa kisiasa Tanzania;

Ni Jukumu la chama Cha mapinduzi kuwanoa vijana wa chama Ili wajue sera miongozo ya chama Ili wanapokuja kwenye platform kama hizi wanapomtetea mwenyekiti wa chama waoneshe namna Gani amesimaia ilani ya chama Ili wananchi na wasio wanachama waone ni namna Gani serikali imetekeleza majukumu na wajibu wake.
Swala la kusifia litabaki wa watakaolewa.

Na sio Kuja kwananga watu waliowafungia KILA kitu na kwanyima pumzi kama stepping stone ya kuonesha mafanikio!

Hakuna mahala ambapo kipimo Cha maendeleo ya taifa lolote la kidemokrasia ni kusambaratisha Upinzani au wenye mawazo tofauti na watawala. Kwani kipimo kimojawapo Cha maendeleo ni kukua kwa demokrasia.

Huyu bwana afaa akasome dira ya maendeleo ya taifa halafu atuoneshe kama kipo kipaumbele au katika bajeti ya serikali Kuwa ni kusambaratisha Upinzani.

Vijana kama hawa wakipewa madarka makubwa hujiona miungu watu na ni wepesi kusababisha maafa, kugawanyika kwa taifa na hata vita vya wenyewe kwa wenyewe! Sio wepesi wa kubishana kwa Hoja na kukubali kutokukubaliana. Hapo alipo anawaza uteuzi na kushibisha Tumbo lake!
 
Hakuna anayezuiliwa ikiwa mtu au chama kitatakuwa kimefuata taratibu zote za kisheria
Bro una uhakika na ulichoandika au mapenzi yamekuzidi mpaka unakua mjinga kiasi hiki:

Unajifanya hujui kwamba tamko la JPM ambalo halijawahi kutenguliwa na ambalo liko kinyume Cha sheria ya vyama vya siasa Bado linatekelezwa?

Mfano kwa mujibu wa sheria polisi hawaombwi ruhusa ya kufanya mikutano au makongamano ya kisiasa wanachotakiwa ni kutoa ulinzi na usalama! Lakini Kuna barua lukuki zipo wadau watakuletea ambapo polisi wanakataza vyama vingine kufanya mikutano ya hadhara makongamano na mambo kama hayo kwa visingizio lukuki huku ccm kikiruhusiwa kufanya hivyo!

Ukitaka mijadala yenye afya jitahidi Kuwa honest Ila ukijizima data utazidi kuonekana mjinga na asiyejielewa.
 
Kwani msafara ungendelee mbele ndio ungeondoa ukweli kuwa upinzani hauna nguvu kwa Sasa hapa nchini, Fuateni taratibu za kisheria mnapotaka kufanya Jambo lolote lile la kisiasa
Upambe bila kutumia akili na kuwa na hoja zenye rejea ni kipimo cha juu cha ujinga.
Hata hao mafisadi ambao wanafaidi uovu wao wanajua ukweli na hawana muda mchafu wa kuandika maujinga unayo jichosha nayo humu kwa ujira wa makombo

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
 
Bila Shaka itakuwa mgeni na siasa za nchi hii wewe, hivi Mara ngapi Tumeona vyama vya upinzani hasa chadema vikipinga kila kitu kinachofanywa na serikali hii ya CCM hata ambacho kipofu anaona kina manufaa kwa mtanzania mnyonge?

Rais Samia alipoweka mkakati wake wa kukabiliana na mfumuko wa Bei ya nishati ya mafuta kwa kutoa Ruzuku ya billioni Mia moja kila mwezi hao upinzani wakiongozwa na wanachadema walipinga mkakati huu, walibeza na kumshambulia Sana Waziri wa fedha mpaka Rais kuwa hela hiyo haina msaada wowote na Wala haitasaidia chochote, lakini mwisho wa siku Tuliona namna mpango huo wa serikali ulivyosaidia kupunguza Bei ya nishati ya mafuta iliyokuwa imepanda Sana katika soko la Dunia kutokana na Vita huko ukrein, Tuliona namna uamuzi huo ulivyo tuweka katika Hali nzuri ukilinganisha na nchi zingine

Tuliona pia baada ya serikali hii chapa kazi inayoongozwa na mama samia ilipoamua kutoa Ruzuku ya billion Mia moja hamsini katika kilimo napo upinzani ulipinga Jambo Hilo na bila sababu za msingi na kusema hela hizo zinaliwa na wachache na hazitaleta tija yoyote Ile kwa mkulima, lakini leo hii wote Ni mashihidi kuwa uamuzi huo wa serikali ya mama Samia imekuwa mkombozi kwa mkulima wa Tanzania baada ya msimu huu mpya wa kilimo Bei ya mbolea kushuka kwa zaidi ya nusu ya Bei ya msimu ulio pita, mfano DAP ambayo mwaka Jana iliuzwa kwa laki na 40, msimu huu inapatikana kwa elfu 70 tu madukani kwote kwa mawakala waliodhinishwa na serikali, je wewe siyo shahidi kuwa uamuzi huo wa serikali umeleta nuru kwa wakulima? Huoni imeleta matumaini kwa watu wengi wanaojihusisha na kujiajiri katika kilimo?

Upinzani Wa nchi hii umekuwa na mchango mdogo Sanaa katika suala Zima la hoja zenye kuleta mabadiliko chanya katika Taifa letu, hii nikutokana na kuwa Ni mkusanyiko wa watu wasio na Sera Wala ajenda, Ni watu waliokosa dira na muelekeo juu ya wapi wanahitaji kwenda au wanaweza wakafanya Nini Kama wangekuwa na mamlaka, Ni mkusanyiko wa wasaka tonge tu, Ni mkusanyiko wa wasaka madaraka tu, Ni mkusanyiko wa watu waliokosa malezi Bora ya kiuongozi, Ni watu wasio na msimamo Wala Haieleweki wanasimamimla Nini zaidi ya kuendeshea na kwenda na matukio ya mpito tu
 

Dah naona aibu mimi
 
Nikujibu tu kwa ufupi;
Mimi ni Senior member hapa JF Wewe ni expert, sio kwamba sikua na Cha kupost tangu nimejiunga hapa la hasha nilikua nachukua Muda kujifunza kutoka kwa watu tofauti ikiwemo vilaza kama Wewe. Kwahiyo Mimi sio mgeni au mchanga katika siasa. Huwa naangalia kipi niandike na wApi niandike! Yamkini Maarifa na umri nimekuzidi.

Rais alipoidhinisha fedha za serikali ziingizwe katika ruzuku, sio chadema tu hata wanazuoni na wataalamu wengi wa uchumi walishauri badala ya serikali kuingiza fedha katika ruzuku ya mafuta kuwepo na upunguzwaji wa Tozo zaidi ya Tisa zilizopo katika mafuta Ili kuleta unafuu wa bidhaa hiyo pamoja na swala la uagizaji wa mafuta wa pamoja. Haya ni mawazo mbadala juu ya kutatua tatizo la kupanda kwa Bei ya mafuta ambalo athari yake kubwa imetoea katika nyanja mbali mbali za maisha ya mtanzania.

Kwa Bahati mbaya licha ya serikali kuweka ruzuku hiyo Bei ya mafuta haijashuka, sanjari na gahrama za maisha mathalani bidhaa za chakula (nafaka) pamoja na nauli!
Swali langu kwako Jana Saudi Arabia akiongoza OPEC+ ametangaza kupunguza uzalishalishaji wa mafuta kama njia ya kuunga mkono Rusia juu ya Uvamizi wa Ukraine, Je serikali imechukua hatua Gani kutokana na athari itakayojitokeza?

Kwanini kwako watu au mtu anapotoa mawazo mbadala juu ya utekelezaji wa jambo Fulani ama la Muda mrefu au dharura anaonekana anapinga au hatakii nchi mema?

Mimi ni mfuasi wa Karl Marx naamini katika kutofautiana katika Hoja ili Kuja na namna iliyo Bora zaidi katika kutekeleza jambo husika!

Hii brainwash aliyowalisha mwendazake inawafanya muwe watu wa kujipendekeza badala ya watu wa kupendeza kwa Hoja. Nimwkujibu kwa Hoja Moja TU maana naona una akili za kuahikiliwa
 
Mikutano na shughuli zote za kisiasa ya namna ya kuendesha hapa nchini Tayari serikali imeshatoa ufafanuzi kuwa utaratibu mzuri unapangwa na majadiliano yatafanyika na wadau wote kupata muafaka mzuri maana Wote tunajenga nyumba moja
 
Mimi naongea ukweli, Kama hauamini angalia hata mitaani namna watu wasivyo na habari na muda na habari zenu
Usipende kusema bila kutafiti. Hoja zako mara nyingi zinakosa msingi kwani ni za kufikirika na siyo halisi.
Jiulize, Kama kweli upinzani umezimwa kwanini ccm wawatumie polisi kuwaghasi wapinzani? Rejea ya juzi morogoro Kwa maarifa zaidi.
 
Nashindwa kukuelewa na hata mtu mwingine hawezi akakuelewa vizuri unaposena kuwa Ruzuku haikusaidia kushuka kwa Bei ya mafuta, lakini pia lazima ufahamu na utambue ya kuwa nchi inaendeshwa kwa Kodi hivyo huwezi ukaondoa kila Kodi au kila aina ya tozo halafu utegemee usipate athari katika uchumi wako, Lazima kufanyike upembuzi yakinifu na wakiutafiti kuangalia faida na hasara zinazoweza kupatikana endapo uamuzi fulani ukichukuliwa Kama huo unaosema kuwa serikali ingeondoa tozo.serikali ikiona kutakuwa na athari ndipo hapo Ina kuja na mkakati wa kutoa Ruzuku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…