Nilitaka kuandika nikujibu kwa hoja mujarabu Ila nimeona na kugundua kuwa una shida sehemu Fulani na kama wewe ndio aina ya vijana tulio nao katika Taifa hili kwakweli kama Taifa nachelea kusema kwamba tumepoteza mwelekeo!
Katika aya zote ukizoandika hakuna hoja yoyote uliyoitoa inayoonesha kupevuka kwako kielimu na kisiasa.
Nina hakika hata mheshimiwa Rais akisoma ulichoandika atatikisa kichwa na kucheka mwenyewe kwa ujinga huu uliondika ukijazia na makosa ya kisarufi na kiuandishi uliyoyaweka.
Badala ya kutumia muda mwingi kuandika kwa kumpaka mama Mafuta kwa mgongo wa chupa Huku ukishindwa kutanabaisha maadui wakubwa wa nchi hii ambayo na ujinga maradhi na umaskini na sio upnzani kama ulivyokaririshwa, ungetumia muda huu kuainisha maeneo ambayo bado serikali ya mama inapaswa kuyaangalia kwa muktadha mzima wa kuwaletea wananchi maisha Bora kijamii na kiuchumi.
Labda nikwambie tu adui wa Tanzania sio upnzani kwa maana ya hivyo vyama visivyokua ccm, adui wa Tanzania ni mfano wewe unayesifia hata nadharia.
Mwalimu alitutaka vija kuwa jeuri na kuhoji huu ya mstakabali wa nchi yetu. Na sio kukaaa na kusifia hata ambavyo havipo. Elimu uliyo nayo ungetumia kuadress cross cutting issues ambazo watanzania wengi wanapitia ungeheshimika zaidi au hata ungeandika juu ya mafanikio ya serikali ya awamu ya Tano pamoja na mapungufu yaliyopo na namna ya kuaproach hayo mapungufu ungekua sehemu ya bunge la wananchi!
Huwezi kusema wapinzani au vyama mbadala havina sera wakati unajua KABISA Kuna unbalanced political platform Kati ya ruling party na upnzani!
Mtaji wa chama ni wanachama na wanachama ndio wasikiliza sera na ndio wanaoamua!
Kwa mujibu wa Sheria ya vyama vya siasa na kanuni zake Ili chama kiwafikie wanachama aumbao ni wananchi yafaa kifanye mikutano ya hadhara, makongamano na midahalo.
Je huoni kila wakati havipewi fursa hiyo na jeshi la polis? Wakifanya kwa lazima wanaishia kuawa na kuwekwa gerezani?
Media haziruhusiwi kutumika Ili kueneza propaganda, agenda, milpango na sera za vyama vingine isipokua Ccm! Unataka usikie wapi sera hizo!
Vyama mbadala viliwekwa maksudi Ili kuisaidia serikali iliyoko madarakani kujitazama na kujitathmini pamoja na kujirekebisha Ili isalie madarakani na kukidhi matakwa ya wananchi!
Kwa uandishi wako unaonesha una chuki ya wazi wazi na vyama hivyo na kusahau kwamba Wewe pia ni mtanzania na hao wanachama wasio Ccm ni watanzania ambao ni Ndugu zako rafiki zako nk. Ila kutofautiana ideology kumekufanya uweke tumbo mbele kwa kivuli Cha uzalendo!
Jitathmini Tanzania ni kubwa kuliko wewe