Upinzani watangaza mapambano 2008


Nimeshukuru sana kwa maelezo yako!
Lakini nimeonelea niseme something..Especially hapo nilipo highlight!
Kwamba hayo maisha waliyokutana nayo kina Marando pamoja na nyie wanasiasa wa upinzani kwa ujumla ndio maisha wanayoishi watanzania walio wengi!

Hivyo basi si mbaya sana kwasababu hilo lita wasaidia kutokuwa out of touch.Litawasaidia kuyajua machungu ya wananchi walio wengi na shida na taabu wanazozipata! Si tu kwenye kulala bali chakula na matibabu pamoja na elimu!

Jingine ni hilo la kina Marando kuendelea na Siasa licha ya kwamba no body cares!
Na hapo ndio penyewe haswa! Kusema kuwa Mrema asingekuwa na mahali pa kwenda kama si Marando siyo kweli!

Kama angetaka na yeye kufungua chama chake angeweza..Ila bado ingemchukua muda zaidi na kwasababu hiyo aka consider watu amabo kimwonekano walikuwa kama wapinzani wa kweli na wazalendo!

Kumbe wao kina Marando walikuwa wakijua kuwa..MORE WANACHAMA=MORE MONEY! Which proved to be true!

Mrema hakujua kuwa hawa watu wanajali maslahi zaidi ya uzalendo!

Mimi niliwaona wakianza kunawiri mara baada ya kupata wanachama wengi na hivyo mapato ya chama kuongezeka! Sasa mara baada ya kupata umaarufu mkubwa na mipesa..Wakaanza urafiki na CCM na kujidai eti wanajali maslahi ya Taifa! WAPI BANA!

Mara nikaanza kusikia migogoro na Marando kuwa favored na CCM na Mkapa na Mrema kuendelea kuchukiwa na CCm huku akiitwa Kichaa!

Na marando kusapoti huo uoza!

Huku na yeye akiwapa CCM siri za Mrema na wapinzani na hivyo kumporomosha kisiasa!
Sasa yeye ni kipi kilichomfanya ageuze mawazo tofauti na wenzake kina Lamwai?

Hivi kweli Zitto...

CCM wamsapoti Marando,halafu waendelee kumwua mrema kisiasa..Hiyo sio maana sahihi ya kuwa "Traitor?

Ama kuna mengine tusiyoyajua?

NB: (kwenye red highlight) Nimeshawahi lala sehemu crazier ma man! Ila maybe in a diffrent situation and/or mission!
 
Mimi nisikufiche Zitto wananchi wanakuangalia kwa moyo wa matumaini makubwa mno!
Kuliko hata ya Mh Rais mwenyewe!
Ni kweli tunampa heshma zake zote lakini ikija kwa wananchi wa kawaida kama sisi..Ni wewe ndio tegemeo letu
!

mhm ! kama kweli, itabidi nianze kumuomba autograph mapema !
 


Mrema ana nafasi kubwa sana katika siasa za vyama vingi na mageuzi ya kisiasa hapa nchini. Lakini naye pia ana makosa yake kama ilivyo kwa akina Marando. Wote wana makosa makubwa ambayo ipo siku watapaswa kuwaomba radhi watanzania. Mrema kanyanyaswa sana, kazuliwa mambo mengi sana. Lakini historia ya nchi itawalinda. Pale historia ya kweli ya nchi itakapoandikwa
 

Mheshimiwa Zitto, taadhima na shukrani siku zote kwa mchango wako.

Mheshima, hao kina Marando, Bagenda na wewe pia nadhani hamtakiwi kabisa kurudia hadharani hiyo hadithi ya kulala kwenye vitanda vya kamba kama kielelezo cha shuruba mnayo ipata. Inaonyesha mlivyo kuwa out of touch. Kama mnadhani ni harubu kuwa katika mazingira hayo wakati hivyo ndivyo wananchi wengi wanavyo ishi basi ujumbe wenu ni elitist.

Bonge la faux pas hilo.
 

Nadhani ni hadithi nzuri na inayofanya viongozi kuona hali ya maisha ya watanzania. Kuacha kusema ni unafiki kwani ukweli ni kwamba watu wengi hamuishi hivyo na wakati mwingine mnasahau kuwa kuna watanzania wanaishi hivyo. Nadhani ni hadithi nzuri na inafaa kuwa recited
 
Kuhani mkuu,
Kiongozi yeyote ni lazima afanane kimaisha na wananchi anaotaka kuwaongoza iwe kwa kifikra ama kimwili...
Kama ukionyesha hujalala ktk amka nikukaze ukazunguzia maisha ya Masaki na O'bay kwenye vyopo vya kuvuta, mkuu hao wakulima wetu huko vijijini watashindwa kukuelewa..Yaleyale ya The Gods must be crazy!
Ni muhimu uzungumze lugha wanayoifahamu na sio kuwaahidi Ndege kupaa wasifahamu unachojaribu kusema.
 
Lakini haina maana kuwa wote wanaolala masaki ama osterbay hawajawahi kupitia suruba!
 
Tusisahau pia kujitolea siyo kujionyesha!
Kuna watu amabo ni matajiri lakini wamepitia mengi na bado wanakuwa concerned na watu masikini!
At the same time kuna wanaopitia maisha kama hayo na badae kuwadharau wengine kwasababu ya uchungu wa kule walikopitia!
 

Mkandara ahsante.

Hujanielewa hata kidogo.

Pointi ya Mh. Zitto, mtanisahihisha kama naikosea, ni kwamba moja ya mfano wa shuruba wanazozipata ni kama vile walivyo lala kwenye vitanda vya kamba wakati wa uchaguzi. Pointi yangu mimi ni kwamba hicho kitu kukisema kama nembo ya heshima ni elitist kwa sababu sio cha ajabu hicho kwa wengi. Ndugu zangu wengi kijijijini ndivyo wanavyo lala, tena wengine hawana hata hivyo vya kamba.

Kwa hiyo kiongozi akisema nimepata shuruba kwa kulala kwenye kitanda cha kamba huyo mtu yuko out of touch.
 
Mimi naomba tu Mungu aisadie nchi yetu na wapinzani wasigawanyike tena jamani!
I am deeply concerned!
 

 

Kweli kabisa Zitto,

Nakubaliana nawe kuwa matraitors ni kama kina Mushi hawa ambao wao wamekaa Marekani kwenye confort na kuanza kutukuna wenzao ambao wako msitari wa mbele.

Kwa nini wewe Mushi usiende Tanzania kuanzisha chama ambacho hakina wasaliti?
 
Sasa kila mtu akianzisha chama kuna usalama?
Eti matraitor ni kina Jmushi waliokaa marekani!
Nani aliye kiongozi ambaye hakuwahi kukaa marekani?
Mwalimu?
Nani? Taja
Si wote waliokaa marekani lakini asilimia kubwa wamekaa marekani!
Na mimi niko hapa kimasomo na usishangae nikiwa kwenye kampeni 2010! Kuwapigia kampeni wazalendo!
Sasa kukaa marekani kunahusiana nini na mimi kutoa mchango wangu na kuuliza when mafisadi watakamatwa?
Wewe si ndio umemwambia mchafuzi akamtafute Balali?
Lugha chafu chafu tu na kujikomba komba!
 

Wakati ukiwa marekani unategemea nani akuendeshee upinzani kule Tanzania?
 
Wakati ukiwa marekani unategemea nani akuendeshee upinzani kule Tanzania?
Nimeshakwambia nipo hapa kimasomo!Tena najisomesha elimu kama waliyosomeshwa mafisadi na wananchi!Si baba si mama si serikali! MAN ALONE!
Na kama ni kupigika nimepigika kama wengine tu!
Kwani marekani ndo mbinguni?
Nani kakwambia sirudi bongo?
 
Kuna moja nilliliacha lipite lakini naona watetezi kama kina Mgaya wanaliamsha bila kujua madhara yake.

Mheshimiwa Zitto angekuwa kwenye jamii iliyo iva kisiasa halafu akaita wananchi wasaliti angekuwa amejinywesha sumu ya panya. Angekufa kisiasa!
 
Lengo hapa ni kuibadilisha nchi yetu!
Bado na mimi nitatoa mchango wangu kama wengine!
Ila usifikiri kuwa mimi ni mgeni wa Tanzanian Politics!
Na therefore this time nasympathize na watu wanaopitia yale ambayo niliyapitia mimi!
Siwezi kukaa tu!
Nikitaka kufanya hivyo naweza! Ila kuna msukumo ambao siwezi kuuzuia na i dont know why!
Sio msukumo mbaya! Bali ni msukumo wa kutotaka kuona yale mabaya yaliyotokea kwenye upinzani yakiwa hayarudiwi tena!
 
Kuna moja nilliliacha lipite lakini naona watetezi kama kina Mgaya wanaliamsha bila kujua madhara yake.

Mheshimiwa Zitto angekuwa kwenye jamii iliyo iva kisiasa halafu akaita wananchi wasaliti angekuwa amejinywesha sumu ya panya. Angekufa kisiasa!

Kama watu ni wasaliti basi wanaitwa kwa jina lao - wasaliti. La sivyo watajua vipi kama wao ni wasaliti?
 
Nimeshakwambia nipo hapa kimasomo!Tena najisomesha elimu kama waliyosomeshwa mafisadi na wananchi!Si baba si mama si serikali! MAN ALONE!
Na kama ni kupigika nimepigika kama wengine tu!
Kwani marekani ndo mbinguni?
Nani kakwambia sirudi bongo?

Wakati ukiwa marekani, nani anakuendeshea hicho chama ambacho hakina wasaliti kama kina marando (kwa msimamo wako)?
 

Ungekuwa na nia ya kuhakikisha yaliyotokea kwenye upinzani hayarudiwi basi ungekuwa msitari wa mbele kule Tanzania kupigania watanzania na wapinzani.

Mengine yote hapa ni kelele tu na kupondea wenzako ambao wanafanya kila wanachoweza kujenga demokrasia nchini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…