jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,329
- 25,263
Traitors ni wale Watanzania ambao wamekaa tu na kusubiri wengine wahangaike kuleta mageuzi. Ni wale wanaokaa bila mchango wowote katika mabadiliko ya kisiasa nchini petu. Ni wale wanaokaa na kulaumu wenzao na kusubiri wakosee wawaseme. Ni wale ambao wanadhani siasa ni tamu na hivyo wanasiasa tunafaidi ilihali tunarisk maisha na hata kutojiendeleza. Traitor sio Marando alieanzisha chama wakati ambao ilikuwa ngumu hata kuwaza kuanzisha chama. Traitor sio Marando ambae hata sasa anasaidia gazeti la mwanahalisi litoke kwa kutoa mchango wa hali na mali. Traitor si Marando alietukanwa na kila mtu bila kujali mchango wake katika mageuzi hapa nchini. Hawezi kuwa Marando traitor ambae wenzake wote wamerud CCM ila yeye na Ndimara bado wapo na chama chao! Traitor ni Mtanzania asietambua harubu tupatayo wanasiasa wa upinzani! Harubu tuipatayo tunapoenda vijijini kuongea na watanzania na kulala mahala ambapo mushi huwajahi lala.
Nakumbuka hadithi ya Prince Bagenda na Mabere Nyaucho Marando walipoenda Rufiji na kulala katika kitanda cha kamba. Watu wazima 2 kitanda kimoja. Kitanda kikakatika na wote kuanguka. Walikuwa katika kueneza vyama vingi. Wakati ambao ulikuwa ukihubiri vyama unaonekana kichaa na watu wanakaa kuleeeeeeeeeee! Hawa wanapswa kuenziwa na sio kuitwa majina yote mabaya. Wale waliopotea njia wanapswa kusikitikiwa kwa kuishia njiani. Lakini tukifika safarini tutawatambua mchango wao walioutoa. Tutafika siku chache zijazo.
Mzee Mtei husema mapambano ya kisiasa ni kama gari moshi liendalo Kigoma. Kuna abiria watashuka Pugu (chemponda etc) wengine morogoro (msabaha etc), wengine Kilosa (Lamwai etc), wengine Dodoma ( Tambwe Hiza etc), wengine Manyoni (Kabourou etc), wengine Kintinku (Akwilombe etc) na bado kuna wengine watashuka gari moshi linavyozidi kwenda. Ila kuna wengi watapandia Tabora, Urambo na Hata Luiche kuelekea kituoni Kigoma. Kuna wengine watajaribu kudandia tutakapokuwa tunatia breki Kigoma ili nao wawemo katika ushindi. Gari moshi hili linabadili madereva kila inapofaa.
Hekima hii ya Mtei ni muhimu sana. Gari moshi sasa linaenda kwa kasi, limekaribia Igalula. Siku si nyingi litafika Kigoma na Watanzania watapata uongozi unaostahili! Uongozi unaojali historia ya nchi na uongozi unaojua ni wapi nchi yapaswa kwenda. Uongozi utakaorevive Tanzanian Dream waliokuwa nayo akina Nyerere! Lakini kwa ushujaa wa akina Mkwawa, Isike, Mazengo, Kinjikitile na wengineo!
Nimeshukuru sana kwa maelezo yako!
Lakini nimeonelea niseme something..Especially hapo nilipo highlight!
Kwamba hayo maisha waliyokutana nayo kina Marando pamoja na nyie wanasiasa wa upinzani kwa ujumla ndio maisha wanayoishi watanzania walio wengi!
Hivyo basi si mbaya sana kwasababu hilo lita wasaidia kutokuwa out of touch.Litawasaidia kuyajua machungu ya wananchi walio wengi na shida na taabu wanazozipata! Si tu kwenye kulala bali chakula na matibabu pamoja na elimu!
Jingine ni hilo la kina Marando kuendelea na Siasa licha ya kwamba no body cares!
Na hapo ndio penyewe haswa! Kusema kuwa Mrema asingekuwa na mahali pa kwenda kama si Marando siyo kweli!
Kama angetaka na yeye kufungua chama chake angeweza..Ila bado ingemchukua muda zaidi na kwasababu hiyo aka consider watu amabo kimwonekano walikuwa kama wapinzani wa kweli na wazalendo!
Kumbe wao kina Marando walikuwa wakijua kuwa..MORE WANACHAMA=MORE MONEY! Which proved to be true!
Mrema hakujua kuwa hawa watu wanajali maslahi zaidi ya uzalendo!
Mimi niliwaona wakianza kunawiri mara baada ya kupata wanachama wengi na hivyo mapato ya chama kuongezeka! Sasa mara baada ya kupata umaarufu mkubwa na mipesa..Wakaanza urafiki na CCM na kujidai eti wanajali maslahi ya Taifa! WAPI BANA!
Mara nikaanza kusikia migogoro na Marando kuwa favored na CCM na Mkapa na Mrema kuendelea kuchukiwa na CCm huku akiitwa Kichaa!
Na marando kusapoti huo uoza!
Huku na yeye akiwapa CCM siri za Mrema na wapinzani na hivyo kumporomosha kisiasa!
Sasa yeye ni kipi kilichomfanya ageuze mawazo tofauti na wenzake kina Lamwai?
Hivi kweli Zitto...
CCM wamsapoti Marando,halafu waendelee kumwua mrema kisiasa..Hiyo sio maana sahihi ya kuwa "Traitor?
Ama kuna mengine tusiyoyajua?
NB: (kwenye red highlight) Nimeshawahi lala sehemu crazier ma man! Ila maybe in a diffrent situation and/or mission!