Upole wa watanzania si ujinga msipuuze Watanzania aisee

Lah! hivi ni wewe kweli!
Mbona ni kama umewehuka ghafla; au umekwisha bugia chimpumu ndio ukaja tena hapa na kuweka uchafu?

Ukiniambia wewe unalijali taifa lako kwa akili unazoonyesha kwa mwandiko tu hapa nitakwambia kuwa hupo mbali na ushetani.
Taifa lolote haliwezi kuwa na watu wa aina yako kama unavyoionyesha kwa maandishi haya hapa.

Sasa kama wewe unawaona waTanzania wenye dini ya kiislam wote katika mlengo huo;; wewe kweli tupe heshima ya kuwa mTanzania mwenye kutolea mfano kwa uzalendo kwa taifa hili? Wewe unayo tofauti gani na hao waislam wanaojiona dini yao ni muhimu zaidi ya utaifa wao kwa nchi hii. Mbona wote mmo kwenye chungu kimoja!

Unaitwa naninvile? Ngoja nikalilijina 'Lwiva' nisije nikakosea tena kumpa heshima mtu asiye istahili kabisa.

Hovyo Kabisa.
Salimu si chochote niamini mimi ndiyo.maana hakuna anaye jua misimamo jake kuhusu taifa .....hakuna anacho kemea au anacho shauri kinacho julikana .....
 
ccm ndo wanaung'ang'ania muungano na wanahakikisha hauvunjiki, tutapima vizuri huu utawala wa kizenji ukushaondoka

tanganyika ilikufa kwa amri ya mwalimu nyerere ~ Lissu
Nilihisi MIZANIA TZ alikuwa na maana hiyo, lakini sikutaka kumlisha maneno.
Ukweli ulivyo sasa hiyo CCM iliyokuwa inautaka muungano huo, haipo tena; sasa hivi kuna kivuli cha CCM chenye malengo tofauti kabisa na yale ya mwanzo.
Kwa hiyo siyo sahihi kuendelea kutumia sababu ile ile kueleza hali iliyopo sasa.

Huo mstari wa maneno unaoueleza wewe kuwa ni maneno aliyo sema Tundu Lissu, naomba unitajie aliyasema lini/wapi na maudhui yake yalikuwa ni nini.
Siyo sahihi kwamba Mwalimu Nyerere ndiye aliyetoa amri ya kuiua Tanganyika. Haya ni maneno ya upotoshaji, na siamini kuwa Tundu Lissu aliyasema maneno hayo kwa sababu za kupotosha watu.
 
  • Thanks
Reactions: Lax

katika bunge la katiba Lissu ndo alisema maneno hayo akimaanisha mwalimu nyerere aliivika tanganyika joho la tanzania kwa amri , hapa ilikua kwenye kulalamikia muundo wa muungano maana zanzibar wanakatiba na raisi , ila huku tanganyika vitu hivyo vipo kwa jina la tanzania (na wakati huohuo tanzania ni muunganiko wa tanganyika na zanzibar)

article mwananchi

video link youtube japo quality ya video ni hafifu sana

View: https://www.youtube.com/watch?v=4Yvp-8AKWgc
 
Heshima sama mkuu 'Lax'.
Nakushukuru kwa kuchukua muda wako na kutafuta ushahidi kuhusu jambo linalohojiwa. JF siku hizi ni nadra sana kupata ulicho kifanya wewe.
Sasa tukirudi kwa hoja husika, ya Tundu Lissu kuyatamka hayo maneno.
Kwanza siyo kweli kwamba "Mwalimu Nyerere alitoa amri"; na siamini kwamba nawe unakubali maneno hayo kuwa ni sahihi.Nami pia siamini kwamba ukimuuliza Tundu Lissu tafsiri ya maneno hayo leo atakueleza kuwa ni kama yalivyo semwa.
Nadhani Tundu Lissu amejifunza mengi toka enzi hizo hadi hapa alipo fikia sasa; na moja ya fundisho litakuwa ni hili la kueleza kwa hisia jambo ambalo linaweza kutafsiriwa kuleta maana hasi.

Lakini ninakubaliana na wewe kwamba Tanganyika iliuliwa katika muungano huo; na iliuliwa kwa lengo maalum. Mategemeo yalikuwa ni kwamba muungano ungeendelea kuimarika kadri ya wananchi wa pande zote wangezidi kuzoeana na kuaminiana kiasi kwamba waliokuwa na hofu ya kumezwa (wazazibari); hofu hiyo ingeendelea kupungua na uhitaji wa kubaki kuwa wazanzibari kupungua na kukubali kuwa waTanzania.

Hayo ndiyo yalikuwa ni matarajio ya muungano kama ulivyo undwa wakati huo wa uasisi wake.

Kwa hiyo kuondoka kwa Tanganyika kulikuwa na nia ya kufikia lengo la nchi moja Tanzania kwa haraka zaidi na kwa urahisi.

Sasa sote tunajuwa mambo hayakwenda kama ilivyo tarajiwa.
Kero za muungano, kama walivyo ziita baadhi ya viongozi wa Zanzibar zikawa zinaongezeka badala ya kupungua, kama ilivyo tegemewa. Maana yake ikawa ni kuudhoofisha muungano, badala ya kuufanya kuwa imara. Sote tunajuwa hizo kero zimeshamiri sana wakati wa viongozi gani wa nchi na CCM; viongozi ambao waliutumia muungano kukidhi mahitaji yao badala ya nchi (Tanzania).

Je, niendelee kueleza hata haya yaliyopo sasa ambayo yapo wazi kabisa?
Ni matumaini yangu kwamba utanielewa vizuri nilicho jaribu kukieleza hapa.

Mwalimu Nyerere hakutoa "amri" mahali popote kuifuta Tanganyika; hayo yalikuwa ni maamuzi ya vikao vya chama na kamati zilizoshughulilika maswala ya muungano wakati huo.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
katika bunge la katiba Lissu ndo alisema maneno hayo akimaanisha mwalimu nyerere aliivika tanganyika joho la tanzania kwa amri , hapa ilikua kwenye kulalamikia muundo wa muungano maana zanzibar wanakatiba na raisi , ila huku tanganyika vitu hivyo vipo kwa jina la tanzania (na wakati huohuo tanzania ni muunganiko wa tanganyika na zanzibar)

article mwananchi

video link youtube japo quality ya video ni hafifu sana

View: https://www.youtube.com/watch?v=4Yvp-8AKWgc

Mkuu 'Lax', utanisamehe kidogo nikirudi hapa haraka hivi.
Nilipo andika niliyo weka hapo juu kukushukuru kwa kuleta ushahidi, sikuwa nime sikiliza hiyo video uliyo iwasilisha.

Nimeisikiliza sasa, na sina lolote ninalohoji katika aliyo yasema Tundu Lissu kwenye video hiyo.
Lililo wazi kutokana na hiyo video ni dhihirisho la wazi kuhusu uwezo mkubwa alio nao huyu mtu katika uchambuzi wa mambo, na uwasilishaji wake. kilicho wazi ni kuwa msema kweli. Hana tabia ya kuvunga vunga mambo kama ilivyo zoeleka na kuwa tabia wa viongozi wa nchi hii. Tazama vizri sura za viongozi hao waliomo humo ndani ya Bunge hilo, utadhihirisha wazi unafiki ulio wajaa, hata wanapo ambiwa ukweli.
Mwalimu Nyerere, kama Tundu Lissu hakuwa na tabia za kuvunga vunga jambo kama hakubaliani nalo; kama anavyo fanya Tundu Lissu; pengine tofauti inaweza kuwa kwenye njia za uwasilishaji tu wa maneno yanayotumika tu basi.

Nikushukuru tena kwa kuiweka hiyo video hapa. Natumaini itatazamwa na wasomaji wengi wa mada hii fikirishi kuhusu muungano wetu huu ulioingia dosari kubwa sana.
 
shukrani mkuu, nimejikuta naendelea kusikiliza muendelezo wa mjadala jinsi ulivokua naimani nitajifunza mengi -- haya mambo ya muungano yanamalalamiko mengi mazito
 
Lililo wazi sasa hivi, kamwe hatuwezi kuendelea na muungano wa aina hii. Hili halikuwa lengo la muungano uliotarajiwa kuwepo kati yetu.
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Lililo wazi sasa hivi, kamwe hatuwezi kuendelea na muungano wa aina hii. Hili halikuwa lengo la muungano uliotarajiwa kuwepo kati yetu.
naam, hii hali ni yakuibadilisha
 
Mimi naweza kufa lakini wajao nyuma watafukua wajue tatizo lilikoanzia!
Tanganyika lazima iamke ipiganie chake!
Mkuu Tanganyika iamke kwani imelala??? Si bora ingekuwa imelala, wewe Tanganyika ilishukufa kitambo, tena kwa kunyongwa!!!
 
Kifo ni usingizi kusubiria kiyama... Huko huko Tanganyika iliko... Iamke!
 
Nyie wakristo tunawajua. Hakuna mnaloweza kuongea tukawaelewa. Mtawakamata waislamu mazuzu tu. Ila muislamu anaejielewa hawezi kuwaunga mkono.
Hakuna chama kinachoweza kuleta umoja wa kitaifa zaidi ya CCM. Hayo mavyama yenu kutwa mnazunguka na maaskofu kama kuna muislamu anasapoti huyo ni mwehu.
Siku CCM ikitoka madarakani waislamu tupambane kuchukua kipande chetu kila mtu abaki kwake. Hatuwezi kuongozwa kwa maelekezo ya kanisa.
 
gallow bird kumbe wewe ndio mmoja mliotumwa kuzima mashambulizi mitandaoni..kwa njia ya kugawa watu kidini..unalipwa sh ngapi
 
Back
Top Bottom