Mnasomba mali za Tanganyika mnajenga Zanzibar lakini Watanganyika wakae kimya.
Mnauza mali zote za Watanganyika kwa ubabe kama mnavyowafukuza wamasai kwao, bandari, madini, kwa mikataba ya kuwakomoa, wakae kimya.
Mnaajiri wazanzibar hata nafasi zisizo za muungano wakae kimya.
Watanganyika wakija kwenu mnawapiga fimbo na kuwanyanyasa eti wanakula mwezi mtukufu, wakae kimya.
Watanganyika wakiimba nyimbo zao kwenu mnawaita makafiri mnawafukuza kwenye nyumba za kupanga lakini wakae kimya.
Mnanunua ardhi ya Tanganyika mnavyotaka ila kwenu mnawabagua na mmetunga sheria ya kukataza Mtanganyika kutonunua ardhi kwenu lakini wakae kimya.
Ni ujinga, uharamu, na uovu kutumia udini kumuibia mtu/mtanganyika.
Miaka ya nyuma walikazana sana na kero za muungano kila siku kwenye majukwaa nk.
Sasa hivi wanavyojichotea mali za mabwege huwasikii hata kwa bahati mbaya.
Watanganyika sio wapole ila mimi naona majuha, mazezeta mabwege na wasiojitambua