Upoteaji wa majina ya asili ya Waafrika

Hakuna tatizo kabisa kuwa na jina la Kizungu, Kirusi, Kilatini , Kichina, Kihindi n.k
 
Petty issues
 
Wakina yohana na wakina hamis walikufa kitambo
 
Hii kitu bana iliwahi kunitokea mwaka 2017 nilienda nchi flan za mbali, ukaguzi immigration yao aliekuwa counter akaniambia "when i saw your name i thought you are a white man" nikamwambia ni majina ya kikristo akaniambia kabla ya ukristo aliekuwa anaitwa John alibadili jina? Shortly ni fedheha kiasi chake na haya sio ya kikristo au Islamic ni majina ya wazungu na waarabu.. Kutokea pale nimewapa watoto wangu majina ya kilugha maana mm kubadilisha siwezi yapo kwenye documents muhimu
 
Licha ya mimi kupewa jina la kukopa toka Ujerumani kwa kisingizio eti ni jina la kikristo (ujinga wa aina yake), baada ya kuokoka toka kwenye utumwa huo wa fikra, watoto wangu wote wanapewa majina ya asili toka sehemu mbalimbali Afrika. Nimegombana na ndugu zangu lakini sijali, watanielewa siku na wao wakiokoka.
 
Tuko pamoja kwenye hili...
 
Kuna jamaa yangu ana watoto 8 na watoto 7 wana majina ya asili sasa hawa watoto wote hakuna aliyemzima ni mwendo wa kuumwa kila wakati hebu tazama kuna kipindi watoto 3 walilazwa kwa pamoja kuna aliyekuwa bugando, Sekwao Toure (Seketule) na Mhimbili na wengine nyumbani baadhi wanalipuka mapepo n.k ila huyu mwingine 1 asiye na hayo majina hana shida yoyote akaja gundua baba yake na mama yake dada zake shangazi zake wengi ni wachawi wa kutupwa hivyo wanachezea watoto tangu nilipoona hili tukio la huyu bwana tena kwa macho yangu na wala si kusimuliwa HAKUNA MWANANGU ATAITWA HAYO MAJINA

Tatizo africa ktk koo zetu kuna mambo machafu na ya ajabu ila hatupendi hata kuyajadili unaweza jikuta unateseka ktk maisha yako yoote ya hapa duniani kisa majina ambayo kwa hakika hatujui hao wahenga wetu walikuaje. Mfano kuna jamaa alimaliza form 6 1992 PCB kutoka shule kubwa flani hapa nchini alipata division 1.5 yaani alikuwa BBA kabla ya kujiunga na MUHAS aliumwa miaka 3 yupo home na baadae akajiunga MUHAS akaumwa tena mwisho akaambiwa ili apone inabidi awe mganga wa kienyeji na kweli alipokubali akapona sasa hivi anatibu watu huko kijijini ana manywele mareefu kama jini lililofufuka hana mbele wala nyuma.
 
Ni ujinga wa muafrika unaendelea. Hebu pata picha msanii mkubwa anamwita mtoto wake "cookies"
 
Mkuu hawezi kukuelewa majina ya kurithi mabaya sana,
 
Haya mambo yalianza tulipobadilishiwa tamaduni ya kuabudu tukaletewa Dini na tukazikubali kua ndo dini sahihi kuliko za mababu.Mababu zetu waliweza kutunza hayo majina kwasababu waliweza kuanzisha KOO.sasa leo tuna tamaduni za kizungu za mke mmoja mume mmoja na watoto wawili hiyo koo itaanzishwaje.Kwasababu huwezi kudumisha jina la asili kama huna uzao wakutosha wanaotumia majina ya asili.kwahiyo baada ya muda ata ilo jina la ukoo la asili litakuja kupotea kwasababu hakuna tena kizazi kitakachodumisha jina la ukoo.maana utakuja kukuta babu mzaa babu mzaa baba wote wana majina ya kigeni.Kwahiyo ata hizi Koo miaka ya badae zitakuja kufutika.
 
Hakuna uhusiano wa majina ya asili na hayo uliyoyataja.kwasababu ata hayo majina ya kigeni tunayoyatumia ni majina ya asili ya uko yalikotoka.Leo unaona matambiko mabaya kwasababu umeletewa Mungu mwingine ukamwamini tofauti na yule wa zamani.Umaskini wetu unatokana na ujinga.
 
Tambiko lina faida gani, waafrika wameanza kutambika hata kabla ya ujio wa wageni,nini wamepata.Wenzetu weupe wapo vile sababu hawana connection na upumbavu.
 
Bado nawalaani wakoloni, yaani mzungu na mwarabu.
Matokeo yake ndio babu kurithi, baba kurithi na miye, kuanzia dini mpaka majina.
Msijali nilifanyia kazi wandugu
 
Bado nawalaani wakoloni, yaani mzungu na mwarabu.
Matokeo yake ndio babu kurithi, baba kurithi na miye, kuanzia dini mpaka majina.
Msijali nilifanyia kazi wandugu
Usiwalaumu ni nature,ni kawaida ya itikadi dhaifu kufa inapopambana na itikadi yenye nguvu.
 
Ni Nchi gani hiyo ambayo institutional racism imetamaraki hivyo? Nchi nyingi za ulaya na America hata kusema Black man ni kosa. Utasikia wakisema coloured man, nk
 
Hii yote inatokana na ujinga wa kukumbatia dini na mila za watu kuwa ni zetu....mtu anaona ufahari kuitwa Mohammed au Daudi wakati hawa wote walikuwa vibaka tu. Yaani tunarithisha watoto wetu laana za watu wa kale wakati wangeweza kupewa majina ya kifahari toka kwa wazee wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…