Upoteaji wa majina ya asili ya Waafrika

Wewe umepumbazwa(brainwashed).
Ebu nipe tofauti ya mzimu na mtakatifu? Hayo Majina yenu ni ya mizimu ya kiarabu na ya kizungu.
Nitafitie mzungu anayeitwa abdulaziz au mwarabu anayeitwa Johnson.

Jina linapaswa kutokana na lugha yako unayoongea na siyo dini.
 
Mzimu ni shetani aliyevaa roho za watu wa familia,kabila,au ukoo wa Jamii fulani,akijifanya still yupo hai na uhitaji tambiko la kafara ya damu ya mtu, wanyama,nk,mzimu unashikilia miongozo yote ya maisha ya jamii husika.
Mizimu haitaki maendeleo na unazuia mafanikio ya jamii inayoabudu mizimu hofu ya kwamba watu wakipata maendeleo wataacha kuabudu mizimu.
Mtakatifu ni mtu aliyeishi maisha ya uadilifu na utakatifu mbele ya jamii na Mungu pia. Waafrika watakatifu wapo wengi.
Haya ni kwa ushahidi wa Quran, Biblia na Elimu ya uchawi pia imethibitisha ninayoyasema.
 
Watu wa West Africa wametuzidi sana. Kuanzia majina, mavazi na lugha. Sisi huku kusini mwa jangwa la Sahara tumekuwa kama misukule ya wazungu. Yaani unakuta mtu majina yote matatu ya kizungu, hadi unashangaa huyu ni mdudu gani wa kizungu?!!
 

Ukikataa majina yao, mkatae na Mungu wao pia.
 
Hiki kizazi cha nyoka hakitauelewa huu uzi kwa sasa. Ila siku zaja ambapo wajukuu, vitukuu na vilembwe vyetu vitaitafuta asili yao (utamaduni na mila) maana watajikuta majina yao ni kama ya wazungu lakini asili yao ni tofauti na wazungu.
Umenena vyema sana
 
Ongezea pia mtu mweusi anaitwa Abdoul razack majid au fatma masoud
Hao wazanzibar ndio wana majina ya kitumwa kabisa;
Khalifa Hamis Seif
Suleiman Aboubakar Khatib
Mahmoud Salim Mahboub
Khalid Said Khalid
Khadija Maalim Juma
Yaani ni vichekesho vitupu!!! Waarabu weusi wasiojua walitoka wapi na asili yao ni nini. Hakuna utumwa mkubwa kama kupoteza identity yako!
 
Mi najiulizaga wale wavaa kobazi hawana makabila? maana karibia wote wana majina ya kiarabu
 
Ukweli usemwe, hizi dini za kuletewa zimetutoa kwenye asili yetu. Wakristo wamechukua majina ya kizungu, waislamu wamechukua majina ya kiarabu.
 
Hizo ni tafsiri za jamii iliyopumbazwa. Kwanini jamii zetu ndo zipewe maana mbovu ya mizimu? Na mizimu ya wazungu ipewe maana nzuri ya mizimu?

Inshort babu yako aliyekufa anaitwa mzimu, babu wa kizungu aliyekufa anaitwa mtakatifu kama ujui.
Huo ndo upumbavu wenu na akili ya kupumbazwa. Yaan inaingia akilini mtoto kuumwa kwa sababu umempa jina la asili.

Acheni ujinga ndo maana watoto wenu mnawapa Majina ya mashoga na wasagaji. Mwisho wa siku mtaua kizazi chenu.
 
Tambiko lina faida gani, waafrika wameanza kutambika hata kabla ya ujio wa wageni,nini wamepata.Wenzetu weupe wapo vile sababu hawana connection na upumbavu.
Unajua maana ya matambiko? Kanisa katoliki ambalo ndo kiongozi wa makanisa yote inafanya matambiko.

Tatizo lenu mnadhani wazungu Wana maisha mazuri kuliko sisi, yaan kwa Hawana shida hata kidogo.

Connection na upumbavu kivp wakati upumbavu wao unausoma na kuufuata kwenye dini na elimu zao.

Penda vya kwenu kama vibovu, vifanyie maboresho.
 
Ni Nchi gani hiyo ambayo institutional racism imetamaraki hivyo? Nchi nyingi za ulaya na America hata kusema Black man ni kosa. Utasikia wakisema coloured man, nk
Hapo ndo ujinga wetu ulipo, yaaan unajisikia vibaya kuitwa black man. Hawa jamaa wanajua kucheza na akili zetu ndo maana tunakataa asili zetu, Majina yetu, rangi zetu na lugha zetu ila tunajisikia vizuri tukitumia Majina yao, lugha zao, asili zao na rangi zao.

Tukiwa comfortable na asili zetu, hata ukibaguliwa utaona sawa. Na anayekubagua akikuona uko comfortable na asili yako hatakubagua kwa sababu atajua unajua thamani yako.
 
Mifumo yao ya maisha Ina nafuu sana ongelea maisha bora basic needs sizungumzii utajiri,hata nchi za kiislamu za kiafrica Wananchi wao awaisomi Sana number. Katoliki na matambiko wapi na wapi.
Kutambika ni ushirikina.Na ushirikina ni ibada ya shetani.
 
Ndugu yangu kuna watu hapa duniani utadhani wanatumia makalio kuwaza/kufikiri. Usipate tabu sana maana miafrika mingine ndivyo ilivyo!
 
Majina ya kitamaduni za Kiarabu nayo ndio balaa, mtu anajiona wa maana sana kujiita au kumpa mwanae jina kama Farhiya, Masoud, Mohammed, Juma, Abdulmalik n.k anajiona kama kaisha fika mbinguni!

Upande mwingine sasa kuna jina watoto wa kike sasa hivi wanapewa kabla hata hawajazaliwa Precious "Preshaz"!!

Ni ujinga unaoenda kwenye upumbavu!

Tumeiga kila kitu cha wageni, nguo, majina, nyumba, pombe, majina, miungu n.k
 
Hapa babu ameamua bora ajiite Maghayo badala ya Copenhagen 😂


Halafu ninyi wadada wa dar najua mpo hapa, kwanini mnapenda kujiita majina ya precious, Conscious, diva n.k?
 
Mtu akishakufa roho yake urudi kwa Muumba wake kusubiria hukumu na mwili unarudi udongoni.Hio nadharia ya mzimu ni babu aliyekufa inatoka wapi.Hata ukisoma vitabu vya elimu ya wachawi au mambo ya giza elimu yao inadhibitisha Hakuna roho inayobaki hai mtu akifa,sasa wewe hio Elimu ya mzimu ni babu umeipata wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…