Upotoshwaji unaoendelea kufanywa na baadhi ya Wafamasia kumpotosha Waziri wa Afya

Kwa hii nchi tunategemeana, Niwe muwazi kuna madaktari hawawezi bila manesi, wafamasia na hata wataalamu wa maabara,
Baadhi ya madaktari ni zerro brain

Kila mmoja ana umuhimu hata USA kuna Baraza la Phlebotomist kwa kua wanaheshimu kaz ya hao jamaa,

Tuwe na ushirikiano katika sector ya Afya Ili tufike mbali na SI maneno.
 
Blatant lie

Umesoma zaidi clinical management lakini mfamasia kasoma zaidi therapeutics

Sisi wauguzi tumesoma zaidi patient care

Stop lying
 
NAENDELEA KUKUPONGEZA.UNAHOJA ZA MSINGI.
 
Sijui kama unajua tofauti kati ya kutoa ( administer ) na Ku dispense.tuanzie hapo kwanza.the doctor can dispense and administer the drug.
 
Unapigiwa simu na ADDO.. Unasema mfamasia....
Daktari anajua dawa... Mfamasia anajua dawa inafanyaje kazi ndani ya mwili na kwa muda gani mgonjwa anatakiwa awe amerespond kwa matibabu...
Mfamasia pia anatoa ushauri pia kwa daktari kuhusu dawa flani kama haitoi matokeo chanya...
 
Kwa wenzetu ishu kama hizi wangeandaa mjadala wa wazi tena kwenye media then sisi waitaji wa huduma zao tungeamua tumfuate nani
 
Nasema wakasome Ufamasia namaanisha degree
 
Ninajivunia sana kuwa sehemu ya mtandao wa kijamii ambapo msomi kama huyu ni sehemu yake pia.

Umetumia lugha inayoeleweka sana na kwa umakini sana kuchambua na kushauri.

Heshima kwako sana Prof.
 
1.Kwanini cheti cha daktari kihitajike na sio cheti cha Mfamasia ambaye ndiye manasema mtaalamu wa dawa?
Dawa zinazotolewa kwa cheti cha daktari kwa sababu zinachukuliwa kuwa hatari ikiwa hazitatumiwa chini ya usimamizi wa mtaalamu wa afya aliyeidhinishwa.
Dawa hizo kwa ujumla zinakusudiwa kutibu matatizo makubwa zaidi ya kiafya. Hii inaweza kujumuisha kisukari, saratani,magojwa ya moyo,bakteria,virusi nk.

Baadhi ya nchi kama vile Uingereza wapo wafamasia na manesi ambao wameidhinishwa kutoa baadhi ya dawa hizo.

👇👇👇👇👇👇
 
EeeeenHeeee Heeeee Heeeee!

Imenibidi leo nitoe kile kicheko changu cha kawaida baada ya kusoma kimakini hili andiko la huyu kijana ambaye bado ndio kaanza shughuli za kiutibabu. Bado ana ule msisimko wa sisi zaidi kuliko wao, kama vile Simba na yYanga; kumbe anayoyazungumzia ni maswala nyeti sana yanayohususu maisha ya mteja wao wote, ambaye kwa kweli ndiye BOSS wao wote, ambaye ni mgonjwa. Bila ya ushirikiano wa mgonjwa, huu usimba na uyanga kati yao hauna maana yoyote.

Baada ya kusoma, nimejiridhisha, hakuna mtu anayejiita "Profesa Patrick Koboro" mwenye 'credentials' za MD, MMED, MPH, MBA, PH.D., n.k..

Mtu huyo hayupo. Huyu anayeandika hapa ni kijana tu asiyekuwa na ufahamu wa muundo wa hizi taaluma za Udaktari na Ufamasia, na wala hajishughulishi kutaka kujua kwa nini muundo huo ulivyo kama ulivyo sasa, si kwa Tanzania pekee, bali duniani kote.

Tena, inawezekana sana hata asiwe mtu aliyehitimu na MD, inawezekana sana hata akawa ni clinical ofisa tu au mtu tu aliye na maslahi na hiyo ADDO, ambayo imemchanganya sana kiasi kwamba anasahau kuwa ADDO ni sehemu ndogo sana katika mpangilio wa huduma za afya hapa nchini.

Baada ya kugundua haya, sioni lazima ya kufafanua hatua kwa hatua yote aliyoyaandika, labda tu kwa ufupi nikazie haya yafuatayo.

Famasia na Udaktari ni taaluma mbili tofauti, lakini zinazotegemeana. Huwezi kusema Famasia inatokana na au ilikuwa tawi la utibabu, kwa hiyo ni lazima utegemee mzazi kwa uwepo wake.
Hao aliowataja kama waanzilishi wa taaluma hizo mbili, yeye kaamua kuwachukuwa wawe upande wake, lakini hataki kukubali kwamba walikuwa pande zote toka mwanzo kabla ya mgawanyo wa taaluma hizi.
Inafaa pia atambue kwamba tokea wakati huo, hadi sasa, pamekuwepo na mabadiliko makubwa sana, kiasi cha kwamba huwezi kuhusisha taaluma moja kuwa kisehemu cha taaluma nyingine, na mabadiliko ndiyo yanazidi kupamba moto wakati huu na haya maswala yanayojitokeza ya "individualized therapy" na maswala mazima ya Biotechnology inavyochukua nafasi yake. Hata huko kwenye utibabu kwenyewe, si swala tena la sisi ni madaktari. Watu wanajipambanua katika fani hiyo hiyo na kufanya vitu vya kipekee kabisa ambavyo wengine hawafanyi.
Kulilia kuwa sehemu ya kuuza madawa wakati huu, na kuacha kushughulikia kazi inayokuhusu ya kumhudumia mgonjwa katika utambuzi wa kinachomsibu mgonjwa, maana yake ni kwamba anatafuta kukimbia kazi anayotakiwa kuifanya kwa ufanisi na kwenda kufanya kazi ambayo hahusiani nayo kabisa.
Kama hapo mwanzo ilionekana kuwepo umuhimu wa kutenganisha majukumu ya udaktari na mambo ya kushughulika na dawa, iweje sasa wakati huu tena huyu kijana alilie kuongezewa majukumu zaidi, wakati hata yale aliyosomea bado hayamudu?

Weka 'focus' kwenye kazi yako uliyosomea, uifanye kwa ufanisi zaidi, hayo ya akina Famasia, himiza tu, na wao wafanye ya kwao kwa ufanisi

Ninakubaliana naye juu ya uozo mwingi uliopo huko ndani ya taaluma ya Famasia unaotakiwa kushughulikiwa na kunyooshwa, lakini siyo swala la kuleta tena tabaka jingine kwenye uozo huo huo. Hilo siyo suluhisho la tatizo hata kidogo.

2. Mara nyingi huwa sipendi kuandika magazeti marefu katika ukumbi huu. Kwa hiyo inanilazimu niishie hapa kwa sasa.

Ikilazimu, nitaweka bandiko jingine la mwendelezo wa hapa nilipoishia.
 
na hapo ndipo penye palipojaa ujinga wenu wa kujiona Nyie na Madaktari ni sawa.


Kwahiyo ukishakua Mfamasia, wee una unauwezo wa kufanya Diagnosis na kutoa treatment ?.


ADDO?. unategemea Daktari ,ambaye alipitia Huu wizi wa ADDO, ... Anaweza nipigia simu Daktari mwenzie Et, Kuna Mgonjwa kaja, analalama hivi nahivi, nimpe dawa gan???.



Ifike Mahali, kubalini tu , nyinyi ni wasaidizi wa Madaktari.
 
Nina uhakika weee ni Clinical Officer au Mwanafunzi wa Utabibu

Mosi, haitwi Mfamacia bali ni Mfamasia

Pili, Kusomea ABC yaani Airways, Breathing and Circulation sio big deal. Hilo ni somo la kawaida hata Red Cross wanaliweza na linafundishwa katika First Aid tuu. Ni wajibu wa kila mtu kujua ABC kama ilivyo kuzima moto.

Tatu, Eti Madaktari na Manesi wamesoma Pharmacology. Huu ni uelewa duni ulionao juu ya Kozi ya Famasi. Naomba nikuambie Mfamasia anasoma Dawa zaidi ya kitu kingine chochote. Anaijua dawa ndani na nje kuliko Mtu yeyote chini ya jua

Nakutajia Masomo makuu ( core subjects) za Kozi ya Famasi ambazo husomwa throughout miaka 4 ya Shahada yake

1. Pharmaceutics hii ni science of dosage forms and design. Hii ndio shule ya dawa zinatengenezwaje, kwa nini dawa iwe ya kidonge, ya maji au kupakaa n.k. Kwa nini dawa hii itolewe mara moja, mbili au tatu kwa siku. Nini kinaenda kutokea kwenye mwili wa mwanadamu akipewa dawa hii. Dawa hii ihifadhiwe wapi na vipi.

Pharmacology. Mfamasia anasoma Basic Pharmacology ( pamoja na Madaktari) lakini huendelea kusoma Clinical Pharmacology and Therapeutics ( pekke yao Madaktari hawasomi hii). Hii ndio shule hasa ya magonjwa kwa nini dawa fulani hutolewa kwa Wagonjwa fulani. Daktari anasoma tuu Ugonjwa fulani hutibiwa kwa dawa fulani.

Pharmaceutical ( Medicinal ) Chemistry. Hii ni sayansi/kemia ya dawa. Kwa nini dawa hii hutolewa kwenye ugonjwa huu. Nini kipo katika dawa hii ambacho aidha kinaua wadudu wanaosababisha magonjwa au kipo katika dawa kinachofanya correction ya physiological abnormalities. Katika somo hilo Wafamaisa hujifunza ni kwa nini dawa fulani haiwezi kutengenezwa katika hali fulani mfano huwezi kuta Benzyl Penicillin maarufu kama Cristapen haiwezi kuwa ya vidonge au hakuna Aspirin ya maji. Kwa nini baadhi ya wadudu huuwawa na dawa fulani na dawa fulani haziwaui kulingana na Structure Activity Relationship

Pharmacognosy hii ni sayansi ya kupata dawa kutoka vyanzo vya asili kama mimea, madini n.k

Pharmaceutical Microbiology hii haina tofauti na Microbiology ya Madaktari lakini huenda mbali zaidi ku include aseptic techniques katika uzalishaji wa dawa na vaccines

Pharmacy Practice hii sasa ni somo la utendaji kila siku unapofanya kazi. Ni kuhusu Sheria, Miiko na taratibu za Taaluma ya Famasi ikiwemo management ya magonjwa mbalimbali
 
Umesema vyema kwamba Wafamasia wanachoweza ni drug dispensing. Basi hilo ndilo Taaluma yao. Daktari hajui drug dispensing ndiyo maana ni lazima asome ADDO.

Hayo mengine ni mbwembwe tuu.
Mfamasia hajui chochote zaidi ya kukaa stoo ya daw
 
same as Prof Koboko's post!
 
well said prof maana naona huku mtaani kika mvaa koti jeupe anajitutumua kuwa daktari
 
Mfamasia hajui chochote zaidi ya kukaa stoo ya daw
Angekuwa hajui chochote huyo Profesa Uchwara asingeanzisha thread kwa thread kulia lia hapa.

Jua na uelewe, hakuna mtu anajua dawa chini ya jua kama Mfamasia. Anaijua nje ( kiwandani) anaijua ndani ( ndani ya mwili)

Nyie wengine kaeni kwa kutulia. A Pharmacist is the master and the owner of medicines.
 
Wamempotosha hadi Hospitali ya MLOGANZILA, badala arudishe MUHAS yeye anafanya tofauti.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…