Upotoshwaji unaoendelea kufanywa na baadhi ya Wafamasia kumpotosha Waziri wa Afya

Hoja yake sio kuingiliana majukumu
Hoja yake ni pale Daktari anapo onekana hawezi kutoa dawa ambazo yeye mwenyewe ndiye ameziandika.
 
Mawazo ya koboko ndio mawazo ya madaktari wengi jobless mtaani wakiamini wao ndio vyeti vyao vilipaswa vitumike kusimamia pharmacy na wala sio mfamasia

Hapa yapaswa tufahamu huyu kijana mdogo anaejiita profesa koboko anawawakilisha madaktari wenzake majobless .
Wafamasia jitahidin kumjibu Kwa hoja huyu koboko
 

Wewe Dr kama ni Dr kweli una matatizo makubwa!! Unatamani ufanye kazi ya wafamasia!! Unataka kuwafukuza kwenye maduka ya madawa eti wakafanye utafiti wa dawa viwandani!! Nenda kasomee pharmarcy kama unatamani wanachokifanya wafamasia leo. Kwenye pharmacy hatuhitaji daktari, daktari abaki hospitalini. Wagonjwa tutakufuata hospitalini na utatuandikia cheti halafu tutakwenda pharmacy kupata dawa ulizotuandikia. Daktari una hila za kushika nafasi zote za udaktari na ufamasia!! Unadai eti mgonjwa akienda pharmacy akamkuta mfamasia atasaidiwaje?? Hey!! Wewe kama daktari haiwezekani uwatie moyo wagonjwa waende pharmarcy wanapougua! Pharmacy siyo hospitali au clinic!! Kama daktari unapaswa kuwa mstari wa mbele kuwaelimisha watu wasiende pharmacy kabla ya kumwona daktari kwanza. Si lazima awepo daktari au nurse kwenye pharmacy kama kuna mfamasia hapo!! Hapo pharmacy hakuna kazi ya daktari!! Kuna kazi ya kutoa dawa tu maana tayari anayeenda hapo amepitia kwa daktari. Tukazanie hilo!!
Hatuwezi kusema watu wasiende hospitali eti kwa sababu kwenye pharmacy watamkuta daktari!! Ni kosa kubwa daktari kudowea nafasi ya mfamasia! Najua kinachomkera huyu daktari kama ni daktari kweli!! Anataka kufungua pharmacy lakini kumtumia mfamasia kwa kuwa eti na yeye anazijua dawa na ndiye anayewaandikia wagonjwa prescription!! Huna jinsi, itabidi utoe tu hyo milioni moja kwa mwezi kwa mfamasia ili asimamie pharmarcy yako japon utauza mwenyewe!!
 
Mimi sio
Mimi sio Daktari hata hivyo nimesoma post zenu moja ya Dactari na hii ya kwako ya Pharmacist
Nilichokiona hapa ni kuwa kila mmoja amebobea kivyake na maanisha Dactari anajua dawa gani inatibu nini hata kama hajui composition ya hiyo dawa kitu ambacho ndicho kinafanywa kwenye drug dispensing
Na maanisha Pharmacy inamuhitaji Mfamasia kwa ajili ya kuangalia storage na zile dawa zinazo hitaji kuchanganywa nk hata hivyo sijui kwa nini Dactari asiweze kutoa dawa aliyo iandika mf: Oxycline 10mg 2x3/14days? ( sorry mimi sio dactari)
Ila naamini wafamacia ni watu muhimu sana hasa kwenye kuandaa/kutengeneza dawa nk
 
Clinical pharmacists provide direct patient care that optimizes the use of medication and promotes health, wellness, and disease prevention.[1][2] Clinical pharmacists care for patients in all health care settings but the clinical pharmacy movement initially began inside hospitals and clinics. Clinical pharmacists often work in collaboration with physicians, physician assistants, nurse practitioners, and other healthcare professionals.[3] Clinical pharmacists can enter into a formal collaborative practice agreement with another healthcare provider, generally one or more physicians, that allows pharmacists to prescribe medications and order laboratory tests.
 
Professor nchi zingine wanafanyaje? eg Marekani, U.k n.k?
Nchi zingine Daktari hahusiki kabisa na pharmacy! Daktari hufungua Medical Consultation Office na kazi yake ni kutoa ushauri kwa wagonjwa na kuwaandikia wagonjwa cheti (prescription). Kazi yake inaishia hapo!! Halafu mgonjwa huenda pharmacy akiwa na cheti chake na huko atahudumiwa na mfamasia kwa mujibu wa prescription!!

Tatizo la huyu Dr ni kwamba yeye anaqtaka afanye vyote! Anataka awaandikie wagonjwa cheti kisha na huko pharmacy akae yeye ili awape dawa!! Kisa eti kwa sababu kazi ya kutoa dawa anaiweza kwa kuwa prescription ameandika mwenyewe!. Nimwulize huyu daktari, kwani yeye kama daktari hajui kuchoma sindano? je hawezi kumchukua mgonjwa wodini na kumhudumia wodini?? Basi adai kufanya na majukumu ya nurse/muuguzi maana anayaweza! Achome wagonjwa sindano, awatundikiea drip nk. Wagonjwa wakifa, awapeleke mochwari! kwana daktari si anajua namna ya kumpeleka maiti mochwari!! Afanye yeye!!

Ninachotaka kusema hapa ni magawanyo ya majukumu baina ya kada mbali mbali za tiba! Daktari baki hospitalini uandikie wagonjwa dawa! Mfamasia baki pharmacy ukihudumia wagonjwa kwa mujibu wa prescription ya daktari kwa dawa zinazohitaji prescription ya daktari. Tatizo la Maboko anataka kumfukuza mfamasia pale pharmacy halafu yeye afanye peke yake!! Huo ni ulafi!! Basi mfukuze na muuguzi wewe daktari uoshe vidonda na uchome sindano, si unaweza kuosha vidonda na kuchoma sindano kama unavyojua kutoa dawa??
 
Kupitia hizi mada it’s obvious hizi medicine and health care degrees zinafundisha core modules tu ndio mzizi wa haya matatizo na mabishano.

Sidhani kama hawa watu wanasoma professional skills kama; decision making, team working, professional communication, safeguarding, evidence based medicine, person centred intervention approaches, reflective (ili kujenga tabia ya kujikosoa na kukosoa mfumo) and so forth to do with the importance of everyday operational necessary professional reasoning and practice skills.

By now kupitia huu mjadala lipo wazi kwa wasomaji wote majukumu ya Dr, Nurse na Pharmacists.

However mpaka sasa swala la ziada inaonekana apparently kuna maeneo ambayo yapo mbali na hospitali na hayo mazingira nilivyoelewa kwenye haya mabishano linaruhusu pharmacists kutoa dawa kwa mgonjwa ambazo otherwise asingezipata bila ya prescription.

Kutokana na hali hiyo wizara or whoever is in charge wanadhani Dr’s nao wawe sehemu ya pharmacy kuongoza maamuzi kama hayo. This is rightly so kama kuna mazingira hayo kwa sababu kwa kanuni za evidence based Dr na Nurse ndio wapo trained to diagnose condition not pharmacists as far as medical practice is concerned (at kama pharmacists wanasoma aspects of medicine) rules are rules; kama kuna mazingira hayo it is highly irresponsible kutoa baadhi ya dawa bila ya Dr au Nurse.

Ni hivi hiyo wizara ni technical na inachangamoto nyingi, kazi ya waziri sio kuhimiza chanjo za polio sijui, COVID na mambo mengine health promotion ambayo ata aliesomea marketing tu anaweza fanya.

Kuna maswala muhimu ya kupokea ushauri wa operation changes and making policy decisions ambayo yanahitaji medical system understanding as the premise of reasonability before deciding; uwezo ambao waziri aliyepo hana.

Mambo mengine ni ya kujitakia kila nchi hii mzaha, atujaongelea amount medical errors ambazo zinafanywa na wataalamu huko mahospitalini ambayo inahitajika mifumo ya kupambana nayo.

I know for certain Dr Gwajima hiyo kazi wizara ya afya anaiweza ata yeye huko alipopelekwa sasa hivi amebaki kufura tu kwa marupurupu ya uwaziri na uelewa wake wa social services ni mdogo kila siku kesi za kulawiti watoto haziishi na wala hana solution zaidi ya kuzunguka; Iwala wizara ya afya kwa yeye kipele kilipata mkunaji ni moja ya maamuzi ya kijinga sana aliyofanya bi tozo kumtoa Dr Gwajima.

Huyo Mwalimu wampe ata wizara ya sheria kama wanampenda sana, Simbachawene apelekwe social services (huyu hana shida ata na uwaziri wenyewe ana bahati tu ya kuteuliwa) na warudishe Dr Gwajima afya ndio sababu aliyofanya apewe ubunge wa kuteuliwa ili aongeze hiyo wizara kwa kutumia utaalamu wake.
 
Asante kwa kuelewa kwamba Daktari anajua dawa X inatibu ugonjwa fulani ila nini kipo na kwa nini kipo huyo ni Mfamasia.

Mfano, Daktari anajua ukiwa na uncomplicated Malaria ( Malaria isiyo kali) dawa ya kuanzia ni Mseto ( ALu) hata hivyo, hata hivyo hajui Alu ni nini na inaenda kufanya nini kwa mdudu au binadamu. Mfamasia anajua ALu ni nini, inatengenezwaje, inaenda kufanya nini kwa Plasmodium wa Malaria na inaenda kufanya nini kwa seli hai nyekundu za damu. Vile vile anajua kwa nini ukimpa mgonjwa dawa hiyo na chakula cha aina gani utaongeza kiwango cha absorption cha dawa mwilini maana anajua kemikali ya dawa. Lakini pia anafahamu kwa nini ukimpa mtu Mseto wenye jina la Coartem ya Kiwanda cha Novartis ya Uswizi inaweza kuleta matokeo bora zaidi kuliko Mseto wenye jina Lumartem kutoka India.

Kuhusu utoaji wa dawa kwenda kwa mgonjwa ndiyo hiyo inayoitwa Pharmacy Practice maana yake Taaluma halisi ya Famasi. Communication skills katika utoaji dawa na kuhakikisha kuna adherence, kuhakikisha rational use ya dawa, kuhakikisha proper recording ya taarifa za dawa iliyotolewa kwenda kwa mgonjwa na mengineyo. Sasa Daktari hawezi fanya dispensing kwa sababu hajasomea taaluma hiyo na sio eneo lake
 
Mimi nimeeelewa uliposema rules are rules tuu

Sasa rules zote duniani ni kwamba Mfamasia ndiye custodian wa dawa na sio Daktari. Sijui kama kuna nchi inaruhusu Daktari kufanya dispensing katika mazingira ya kawaida.

So if unakubali rules are rules basi tuziache rules ziendelee. Daktari afanye jukumu lake la Diagsnosis and prescribing, Nesi afanye jukumu lake la Nursing Care na Pharmacist afanye jukumu lake la Drug Dispensing.

Kutakuwa na tatizo hapo?
 
Reactions: Uni
Wamempotosha hadi Hospitali ya MLOGANZILA, badala arudishe MUHAS yeye anafanya tofauti.
Huyo dada kuna watu wengine wanadhani nina personal issue nae jinsi ninavyopinga uwepo wake hapo kuna maisha ya watu yanachezewa na yeye ni clueless kwenye hiyo wizara.

Kipindi hiki cha serikali haribifu it doesn’t matter nani waziri wa fedha, kama J.K alimuweka Saada Mkuya waziri wa fedha surely Ummy Mwalimu mwenye degree ya Law na postgraduate anatosha hapo apige deal wanazotaka na shoga yake bi tozo; lakini watutotelee huyo dada kwenye maisha ya watu.
 
Afadhali umesema ukweli!! Njaa inawasumbua madaktari sana!! Wanawaonea wivu wafamasia kwa sababu daktari hana ruhusa ya kufungua pharmacy ili agange njaa bila kumtumia mfamasia japo kwa taaluma yake anaweza kuuza dawa kwa wagonjwa bila shida na bila kulazimika mgonjwa kuwa na cheti. Ila Daktari anachokifumbia macho ni kuwa basi hatuna haja ya kuwa na wauguzi maana daktari anaweza pia kuchoma sindano na kuosha vidonda!
Daktari Koboko ridhika na urefu wa kamba yako ule hapo!! Waachie na wafamasia kwenye urefu wa kamba yao!! Kama Dr Koboko anataka kufungua pharmacy asione kinyaa kumwajili mfamasia na amlipe sh, milioni moja kwa mwezi kwa kusimamia pharmacy yake japo atauza mwenyewe! Hakuna namna lazima mfamasia ale tu pesa yako!!
 
Huna akili
 
Umetaja medical errors

Naomba nikueleze amount ya medical errors katika nchi hii ni nyingi sana. Najua medical errors zina stem kutoka maeneo mbalimbali. Lakini hebu pitia hii study kidogo tuzidi kujielimisha hawa Madaktari wanao claim wao ndio Watu sahihi wanaojua dawa ili tuone wanafanyaje kazi hapa nchini

 
Sijabishia hilo lakini pia aruhusiwi kutoa baadhi ya dawa bila ya prescription ya MD, sasa kama kuna mazingira ambayo watu awawezi kwenda hospitali (I don’t know how is that possible or just permitted kwa uzembe wa wasimamizi) ambayo yanaruhusu pharmacists kufanya diagnosis na kutoa dawa this is against evidence based medicine approach kwa sababu a pharmacist is not trained to that.
 
Hamna watu wabinafsi na wenye tamaa kama hao madaktari mbona mmejimilikisha hiyo wizara ya Afya utasema ya kwenu bado mnataka muingie na Pharmacy ?
We unasoma pharmacology semester 1 leo unajiit wewe ni unajua dawa ?
Kila mtu abaki na utaratibu wake mbona wafamasia hawalalamiki wafanye diagnosis?
Eti naye professa🤣
 
Hakuna tatizo!! shida ni kuwa daktari anataka afanye yeye kazi zote eti kwa kuwa anaweza!! Basi awahudumie na wagonjwa kwenye wodi si anaweza kuwapa dawa na kuwachoma sindano!! Dr Koboko analazimisha kuunganisha kamba yake na ile ya mfamasia!! Dr Koboko inabidi uridhike tu kula kama urefu wa kamba yako ya udaktari inavyokuruhusu!! Usitamani kuunganisha na kamba ya mfamasia!! huo sasa ni uroho!!
 
Hii ni kosa kabisa kusema eti Pharmacist hawajui diagnosis 😃😃😃

Shule ya Mfamasia inamtosha kufanya a rational judgement ya magonjwa mengi tuu. Ndiyo maana kuna Pharmacy Only Medicines ambazo Mfamasia anaweza kuzitoa bila ya kuhitaji cheti cha Daktari
 
Ungejibu kwa hoja ingekuwa poa sana kuliko hii panic attack uliyofanya
 
Hii Wizara ifumuliwe kuna ukiritimba kama wa huyu anayejiita profesa na phd ya mchongo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…