Upotoshwaji unaoendelea kufanywa na baadhi ya Wafamasia kumpotosha Waziri wa Afya

I knew several cases of medical errors hata kwenye hizi mada mbili kuna wachangiaji wameongelea poor decision za medics which almost cost their lives.

If anything haya majibizano ya wataalamu ndio yamehalalisha the extent of the problem if this how they work.

Sasa medical error zinasababu nyingi main one ni ‘human factor’ kama wewe daktari unajifanya unajua kushinda mtu yeyote na professional mwenzako ana second opinion utaki kusikiliza kwa sababu wewe ni superior si unauwa mgonjwa.

Ni hivi hiyo wizara mifumo iliyopo tu kuheshimiwa shida ili huduma iwe na quality Dr Gwajima alionyesha madhaifu hayo; jumlisha na changamoto za kureview mifumo inayolea uzembe na kuja na mikakati mingine ya supervision kuboresha huduma.

Huyo waziri aliyepo hapo anatosha kweli.
 
Hicho ndicho tukipige vita!! Wafamasia wana maadili yao ya kitaaluma na hawawezi kutoa dawa ambazo zinahitaji prescription ya daktari. Tuwaelimishe watu wasiwakwepe madaktari na kukimbilia pharmacy. Lakini hatuwezi kutatua tatizo la watu kuwakwepa madaktari kwa kuwaruhusu madaktari kukaa pharmacy moja kwa moja. Tukifanya hivyo watazigeuza pharmacy kuwa dispensary na hospitali kosa ambalo ni baya zaidi!! Tatizo tulitatue kwa kutoa elimu kwa jamii!!
 
Ata daktari afanyi kila diagnosis mwenyewe kuna vipimo vya machine kama x-rays, scanners, laboratory and so forth; ndio anaamua matibabu na dawa.

Sasa ni upuuzi kusema pharmacists aliye pharmacy ambayo aina assitive technology wala maabara ya vipimo anaweza fanya diagnosis na kuamua dawa.

Ni hivi hiyo wizara inahitaji technocrat kuna so much ego amongst different professionals.
 
Nakuambia kitu sasa Daktari anakalili Sawa full stop..... STANDARD TREATMENT GUIDELINE hichi ni kitabu kinaelezea kila ugonjwa utibiwe na dawa gani

Hichi kitabu hata wewe unaweza download na ukajua

NB:Ndicho hutumia kukalili baada ya kumaliza miaka Yao 5 shule..... it's so simple


Jiulize sasa hakuna mfamasia ambae Hana hii soft copy, ila vitu vingi it's normal things kwenye management so mfamasia anaweza akafanya substitute ya dawa ila Daktari asijue,mana anajua kile Tu kilicho andikwa na kama hakipo anakufosi ukainunue


ila pharmacist anaangalia inaenda kutibu nini na hii dawa chemically ipoje, na inauwezo gani katika hili na Hali ya mgonjwa ipoje.... lastly unashangaa Anakupa m'badala ukatumie




Nawasilisha
 
Issue sio kuelimisha watu ni wizara kutoa maelezo kipi kinaweza uzwa pharmacy na kipi lazima kitolewe kwa prescription only na kupiga ban kwenda tofauti; vinginevyo ukibainika sheria ichukuwe mkondo wake.

Sema sasa humu naona kuna arguments za sijui kuna watu wapo mbali na hospitali mara vituo vya afya ndio maana pharmacists wanaweza toa dawa bila ya prescription; hilo swala alikubaliki bila ya Dr kama kuna mazingira hayo.
 
Mimi nimeshangaa huyu jamaa anajiita Koboko...
Eti Pharmacist hajui diagnosis...
Na unaweza kukuta huyu ni Medical officer wa kawaida.. Anataka akae Pharmacy...
Wanaenda huko Wizarani na kuandaa research hewa na kumdanganya waziri mambo mengi tuu kuhusu hii taaluma ya famasi..
 
NAENDELEA KUKUPONGEZA.UNAHOJA ZA MSINGI.
Unampongeza bure!! Hujajua hoja yake ya msingi!! Hoja yake ni kwamba, kwa kuwa yeye ni daktari basi afanye pia kwenye pharmacy kwa kuwa anazijua dawa anazohitaji mgonjwa na hahitaji msaada wa mfamasia. Anataka wafamasia waende viwandani kutengeneza dawa na kufanya tafiti za dawa! Dr KIoboko kimsingi anataka kuunganisha kamba yake kama daktari na ile ya mfamasia!! Hajaridhika kula kutokana na urefu wa kamba yake ya udaktari!! anataka na ile kamba ya ufamasia!! Huu ni uroho! Dr Koboko ningemwelewa kama angekuwa anasisitiza wagonjwa lazima wapate cheti cha daktari kwa baadhi ya dawa kwa mujibu wa sheria. Sasa yeye Koboko anataka mgonjwa hana haja ya kuwa na cheti cha daktari anapoenda pharmacy maana huko pharmacy atamkuta daktari pia!! Sasa hii ni dhana hatari na itavunja sheria, maana daktari akikaa pharmacy ataigeuza pharmacy kuwa dispensary au clinic au hospitali! Dr Koboko ridhika na jukumu la kumtibu mgonjwa kwa maana ya kumchunguza na kumwandikia dawa!! Sehemu iliyobaki kwa mgonjwa waachie taaluma nyingine za afya kama wauguzi na wafamasia!!
 
Kwahiyo pharmacognosy ndio ikazaa bupiji sio? Tanzania nchi yangu nakupenda, mnavyobishana hapa utadhani nchi inatengeneza hata Panadol au hatupeleki wagonjwa India kutibiwa yaani
 
Basi MD & Nurse fanyeni kazi zote hospitalini wenyewe na kozi ya famasi waifute Tanzania mazimaa

Sijawahi kuona watu wenye gubu na wivu kama watz dah walio soma kitu fulani wanajiona special kuliko wengine.
 
Hoja yake sio kuingiliana majukumu
Hoja yake ni pale Daktari anapo onekana hawezi kutoa dawa ambazo yeye mwenyewe ndiye ameziandika.
Hakuna anayesema kuwa daktari hawezi kutoa dawa pale pharmacy, maana hata manesi wanaruhusiwa kutoa dawa pale pharmacy!! Ila Daktari anaweza kutoa dawa pale pharmacy kwa usimamizi wa mfamasia pale pharmacy! Dr Koboko anataka ajitawale pale pharmacy bila uwepo wa mfamasia. Anataka wafamasia waende viwandani kutengeneza madawa na kufanya tafiti zaq madawa!! Hilo hapana! Kitu ninachokubaliana naye ni ile bodi ya pharmacy ilikuwa inataka daktari au muuguzi kupata mafunzo ya ADDO ili kuweza kuhudumia duka la dawa. Huo ulikuwa ni upigaji!! Na tayari wizara ilishaliona hilo na kulizuia!!
Dr Koboko anataka kumiliki pharmacy na kuihudumia bila msaada wa mfamasia! Ukiruhusu hilo ataigeuza pharmacy kuwa dispensary!!
 
Unachosema ndivyo ilivyo!! Kuna baadhi ya dawa pharmacist haruhusiwi kutoa bila prescription!! Sheria hairuhusu!! Watu wanavunja sheria kwa sababu ya ujinga na njaa!! Ndiyo maana ni muhimu kuwekeza pia kwenye elimu ya jamii!! Wazo la Dr Koboko ni la hatari!! Anataka daktari akae pharmacy ili kuondoa ulazima wa mgonjwa kwenda pharmacy akiwa na prescription kwa baadhi ya dawa! Ukifanya hivyo huyu daktari ataigeuza pharmacy kuwa dispensary. Sasa hao wenye dispensary wafanyeje?? Pointi yake kuhusu ADDO ni sahihi, ila hili la ADDO tayari wizara ilishalifanyia kazi na bodi ya pharmacy walikubali.
 
Sio vizuri kudanganya au kuandika uongo hapa
 
Dah sasa nimeelewa, huyu Dr tamaa.
 
1. Duniani kote utafiti unaonyesha, kwa wengi, mtu akiumwa mtu wa kwanza kwenda kumuona ni pharmacist. Kuna dawa nyingi sana anazoweza pewa na mfamasia bila kuhitaji cheti cha daktari. Anapata ushauri mwingi pia.

2. Daktari hajui kilichopo ndani ya dawa. Ni hatari kumuachia pharmacy. Mfano rahisi, kuna dawa kibao za kikohozi ambazo ni mchanganyiko wa mitishamba, hata kumi sometimes. Daktari anafahamu vile ni vitu gani? Anajua vinafanya nini mwilini? Wafamasia tunaziogopa sana dawa, tunajua vilivyopo ndani.

3. Sheria ya utoaji wa dawa zinazohitaji cheti cha daktari zinajulikana. Kutoifuata ni kosa. Lakini si kutumia kosa hilo kutaka wasiofahamu masuala ya dawa nao waruhusiwe kuzihandle.

4. Na historia. Mtu wa kwanza kuanza kuchanganya na kuponda mitishamba kwa lengo la kujitibu ndiye mfamasia wa kwanza. Si ajabu ufamasia ulianza kabla ya udaktari.
 
Hata kama ni kweli kuwa watu wengi wakiumwa hupenda kwenda pharmacy, hayo mazoea ni mabaya! Ukweli utabaki kuwa pharmacy si mahali pa kutolea tiba!! Hayo ni makosa makubwa ambayo jamii inapaswa kuelimishwa!! Mahali pa kupata tiba ni hospitalini na mtu sahihi wa kutoa ushauri wa kitabibu ni daktari!! Pharmacy ni mahali pa kotolea dawa!! Japo si kila dawa inahitaji prescription ya daktari! Kama dawa unayotaka haihitaji prescription ya daktari hapo ni sahihi kwenda pharmacy moja kwa moja!! Watu wanataka urahisi, japo kuendekeza urahisi kwenye suala la afya yako kunaweza kukuingiza kwenye gharama kubwa sana!!
Tunawaomba hawa wataalamu wetu wa afya wazingatie maadili ya kazi zao na kutanguliza utu badala ya fedha! Mtu wa pharmacy anakuja mtu dukani kwako nanataka madawa ya moyo tena ya bei mbaya!! lakini hana cheti! usitamani hiyo pesa bali mwelekeze mgonjwa akamwone daktari kwanza!! Na madaktari wana hulka ya kudharau kazi za kada nyingine as if wao peke yao ndio wanaweza kila kitu! hapana!! Vinginevyo tuondoe wauguzi na wafamasia hospitalini wafanye wao peke yao!! Msiendekeze njaa!!
 
Shida ya madaktari wengi huwa wanahisi wamesoma sna kuliko watu wengine
 
Madaktari wao huwa wanahisi wana akili kuliko watu wote
 
Lengo lao ni maslahi wala hawana lolote
 
Shida ya nchi nyingi za Africa ni mfumo mbovu wa kiutawala
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…