Nina uhakika weee ni Clinical Officer au Mwanafunzi wa Utabibu
Mosi, haitwi Mfamacia bali ni Mfamasia
Pili, Kusomea ABC yaani Airways, Breathing and Circulation sio big deal. Hilo ni somo la kawaida hata Red Cross wanaliweza na linafundishwa katika First Aid tuu. Ni wajibu wa kila mtu kujua ABC kama ilivyo kuzima moto.
Tatu, Eti Madaktari na Manesi wamesoma Pharmacology. Huu ni uelewa duni ulionao juu ya Kozi ya Famasi. Naomba nikuambie Mfamasia anasoma Dawa zaidi ya kitu kingine chochote. Anaijua dawa ndani na nje kuliko Mtu yeyote chini ya jua
Nakutajia Masomo makuu ( core subjects) za Kozi ya Famasi ambazo husomwa throughout miaka 4 ya Shahada yake
1. Pharmaceutics hii ni science of dosage forms and design. Hii ndio shule ya dawa zinatengenezwaje, kwa nini dawa iwe ya kidonge, ya maji au kupakaa n.k. Kwa nini dawa hii itolewe mara moja, mbili au tatu kwa siku. Nini kinaenda kutokea kwenye mwili wa mwanadamu akipewa dawa hii. Dawa hii ihifadhiwe wapi na vipi.
Pharmacology. Mfamasia anasoma Basic Pharmacology ( pamoja na Madaktari) lakini huendelea kusoma Clinical Pharmacology and Therapeutics ( pekke yao Madaktari hawasomi hii). Hii ndio shule hasa ya magonjwa kwa nini dawa fulani hutolewa kwa Wagonjwa fulani. Daktari anasoma tuu Ugonjwa fulani hutibiwa kwa dawa fulani.
Pharmaceutical ( Medicinal ) Chemistry. Hii ni sayansi/kemia ya dawa. Kwa nini dawa hii hutolewa kwenye ugonjwa huu. Nini kipo katika dawa hii ambacho aidha kinaua wadudu wanaosababisha magonjwa au kipo katika dawa kinachofanya correction ya physiological abnormalities. Katika somo hilo Wafamaisa hujifunza ni kwa nini dawa fulani haiwezi kutengenezwa katika hali fulani mfano huwezi kuta Benzyl Penicillin maarufu kama Cristapen haiwezi kuwa ya vidonge au hakuna Aspirin ya maji. Kwa nini baadhi ya wadudu huuwawa na dawa fulani na dawa fulani haziwaui kulingana na Structure Activity Relationship
Pharmacognosy hii ni sayansi ya kupata dawa kutoka vyanzo vya asili kama mimea, madini n.k
Pharmaceutical Microbiology hii haina tofauti na Microbiology ya Madaktari lakini huenda mbali zaidi ku include aseptic techniques katika uzalishaji wa dawa na vaccines
Pharmacy Practice hii sasa ni somo la utendaji kila siku unapofanya kazi. Ni kuhusu Sheria, Miiko na taratibu za Taaluma ya Famasi ikiwemo management ya magonjwa mbalimbali