Upweke umewaanza vijana mapema, Uzeeni sijui itakuwaje. Ni janga kubwa

Upweke umewaanza vijana mapema, Uzeeni sijui itakuwaje. Ni janga kubwa

Ni Ukweli Kabisa. Chanzo Kikuu Ni Mapenzi, Tunawapenda Ambazo Hawatupendi Tukitegema Tufunge Nao Ndoa Tuanzishe Familia Lakini Mwisho Huwa Ni Maumivu. Mwanaume Una 30+ Umetoka Kazini Umechoka, Biashara Haijaenda Sawa Unafika Home Hata Wa Kusema Baba Waooo Hakuna. Wa Kukwambia Pole Na Kazi Kipenzi Hakuna. Unapumzika Unajiuliza Maswali Unajijibu Mengine Yanakosekana Majibu. Ndoa Ni Jambo Jema Sana. Ukipata Mwanamke Anayekuheshimu Na Kukutii Muoe. Vijana Tusibabaike Na Shape Na Rangi.

Sio pouwa!
Inahuzunisha mno
 
Ni Ukweli Kabisa. Chanzo Kikuu Ni Mapenzi, Tunawapenda Ambazo Hawatupendi Tukitegema Tufunge Nao Ndoa Tuanzishe
Vijana mnapaswa mrudi kwa wazee wenu mkijihisi mmekua kiasi cha kuanzisha familia wao wana jicho la kuona mbali zaidi ili wakuangalizie binti anayekufaa au wakushauri,oa mke anayetokana na asili ya kwenu (kabila) mnaofanana asili,ondoa vigezo kama elimu na kazi kwani kuingia labour kuzaa hakuhitaji certificate wala I'd ya anakofanya kazi kunahitaji mwanamke aliye tayari kuwa mama.

Wewe mwanaume hukupewa moyo wa kupenda umepewa moyo wa kujali na kuthamini while mwanamke amepewa moyo wa kupenda hakupewa moyo wa kuthamini ndiyo maana kama alipokuwa hana kazi wewe ulimjali na kumthamini kumvisha kumlisha etc kwa miaka mitano but wewe ukikosa kazi ukakaa nyumbani akawa yeye ndiye anayeenda kutafuta ndani ya mwezi nyumba unaiona chungu,kinachomfanya mwanaume aamini amependa ni kule kusikilizia sana hisia za ngono na sauti ya wizi pale mwanamke akitaka kumpanga ampe hela nothing else.
 
mimi nasema kazi sasa

Kiasili binadamu hajaumbwa kufanya kazi.
Ila upendo kiasili upo kwa kila kiumbe.
Hakuna ambaye hataki kupendwa.
Upendo ukikosa upweke upo automatically.

Ila unaweza kosa kazi na usiwe mpweke.
Ndio maana wapo watoto wadogo hawafanyi kazi na wazee hawafanyi kazi lakini hiyo haimaanishi wapo wapweke. Ila wakikosa wanaowapenda automatically upweke unabisha hodi.
 
mimi hapana,
nna options kadhaa za kutoa huo upweke, kucheza GTA-5, kwenda Tabata kubarizi ki-maakuli, nk
ila siyo kutegemea kiumbe KE ambaye anatumia pesa zangu

Kwa nini atumie zako wakati hataki utumie zake?
Wapo wanawake wengi ambao unaweza kutumia nao bila ubinafsi
 
Back
Top Bottom