Urafiki wa Afrika na China hauna maslahi kwa Wananchi. Una maslahi kwa watawala Madikteta

Urafiki wa Afrika na China hauna maslahi kwa Wananchi. Una maslahi kwa watawala Madikteta

Mnacho kifanya nyinyi nikurudia rudia propaganda za America na Uingereza kuhusu ubaya wa ujio wa Wachina Barani Africa.
Ni wakati gani inakuwa propaganda na wakati gani inakuwa ukweli? Mmarekani hakopeshi wala hamung'unyi maneno. Cheki katangaza dunia mzima grant ya kuwadhibiti wachina kusambaza silaha za hatari na udukuzi kama lile jengo la AU walilotujengea wachina Addis kumbe lilikuwa limejaa electronic bugs zinapeleka habari zote China. Na sisi walitujengea jengo la mafunzo ya kijeshi Bagamoyo. LIsije nalo limejaa bugs!! Changamkia fursa kuna $300,000 kuupinga ubeberu mamboleo wa kichina 🙂 KItu kimoja kizuri Magufuli alichokifanya ni kuachana na mradi wa bandari ya Bagamoyo. Kwa hili namuunga mkono.
 
Ujanja mwingine wa moderators ni kuhamisha uzi jukwaa ambalo lina watu wengi na kwenda ficha jukwaa ambalo limepoa. Huu uzi ulitumwa jukwaa la Siasa. Wameupeleka International Forum wakati uzi ni wa tanzania na Kiswahili, ila wameogopa serikali itaudhika.
Jamaa ndo walifanya nikaacha kabisa kuandika huku nimebaki mkomentiji tu
 
Popote pale China ilipo inaweka mazingira mazuri kwa ajili ya watu wake. Hivyo hujitahidi sana kukamata Serikali iliyopo Madarakani kwa kui support kwa hali na mali ili Serikali hiyo iendelee kuwanyonya wananchi na China ifaidike kwa maslahi ya nchi yake.

China ya sasa siyo China ya Ujamaa. Hii ni China ya Utamaa. Inayoangalia namna ya kujitanua zaidi kiuchumi. Angalia mikataba ya ki Chief Mangungo wa Msovero ambayo China imeingia na mataifa mengi ya kiafrika. Nenda kafuatilie kinachowapata Zambia sasa.

Waulize Kenya. Kaulize mkataba ambao ilikuwa tuingie kuhusiana na Bandari ya Bagamoyo. Ni Mkataba wa kihuni kupata kuwekwa na hili sina budi kumpongeza Magufuli.

Lakini kuna madudu mengi ambayo bado China inayafanya kwa nchi zetu za Kiafrika.

Mi sijui.
Ni5tena
 
Ni wakati gani inakuwa propaganda na wakati gani inakuwa ukweli? Mmarekani hakopeshi wala hamung'unyi maneno. Cheki katangaza dunia mzima grant ya kuwadhibiti wachina kusambaza silaha za hatari na udukuzi kama lile jengo la AU walilotujengea wachina Addis kumbe lilikuwa limejaa electronic bugs zinapeleka habari zote China. Na sisi walitujengea jengo la mafunzo ya kijeshi Bagamoyo. LIsije nalo limejaa bugs!! Changamkia fursa kuna $300,000 kuupinga ubeberu mamboleo wa kichina 🙂 KItu kimoja kizuri Magufuli alichokifanya ni kuachana na mradi wa bandari ya Bagamoyo. Kwa hili namuunga mkono.
Here we go again accusing Chinese with all sorts of vices under the SUN!! Swali dogo - who is the World seasoned sniffer and spoofer was masula ya mitandao na Simu za watu Duniani kote anadakuwa mpaka anao jifanya ni marafiki wake was karibu mfano: waziri mkuu wa Ujerumani Angela Merkel, Rais wa Ufaransa na Austria mpaka wajomba zake Waingereza hata Simu yako inayo tumia Android au iOS inakuwa monitored 24X7 hata uki- switch off labda utoe beteri, hapo hatujazungumzia CISCO Routers zinazo tumika sana kusambaza masuala ya mitandao Duniani simu zote za Android, iOS operating systems pamoja na CISCO router manufacturers wamekuwa instructed na taasisi ya kijasusi ya Kimerikani (NAS) kwamba waziachie baadhi ya ports ili iwe rahisi kwa NAS kudukuwa smart phones za watumiaji pamoja na mitambo ya kusambaza voice na data - hakuna MTU ambaye ni salama dhidi ya massive udukuwaji wa NAS, taasisi hii na hatari sana kwa mstakabali was privacy za watu Duniani - Ukitaka kujua ushenzi wa taasisi hii fatilia ufafanuzi wa kina wa jasusi aliye wahi kufanya kazi kwenye taasisi ya NAS kabla hajatorokea huko Urusi, Huyo ndiye alifumbua macho Dunia kuhusu hatari za tasisi ya NAS.

Leo hii baadhi ya waswahili wana join band wagon ya kuwasema vibaya Wachina as if USA ni watakatifu linapojuja suala LA udakuzi wa mitandaoni, kumbe ndio vinara wa mambo hayo, hivyo USA hawana moral authority ya kuwanyoshea vidole wachina - kama unataka ufafanuzi wa kina kuhusu modus operandi ya taasisi ya "NAS" someni machapisho ya Snowden.

Kuhusu jengo la AU pale Addis, no wapi Secretary General wa AU aliwahi kulalamikia China kwamba jengo liko laden na listening devices - wapi? Eti Wachina wametujengea chuo cha kijeshi B'moyo bila shaka limajaa bugs - uzushi mtupu hata aibu huna, ina maana hata Chuo cha Kijeshi cha Moduli nacho kiwe torn down kusaka bugs kwa kuwa kilijengwa na Wachina, cha Kunduchi je? Hivi kwa akili za kawaida Wachina watakuwa na interest gani ya ku-install bugs za kusikiliza/record conversations za Govt Officials wakati Tanzania si tishio kwa Wachina kiuchumi wala kijeshi mnatuletea Mickey Mouse stories za kubuni tu - kisa? Mmehaidiwa $300,000 kuichafua Uchina, which means you are simply a Uncle SAM paid troll to demonise China - mbinu zenu hazitafanukiwa hata kidogo.

Kuhusu Bandari ya Bagamoyo hiyo ntaizungumzia siku nyingine.
 
WACHINA, WAHINDI NA JAMII ZINGINE ZA KIBUDHHA, ISHIENI KUWAANGALIA KWENYE MOVIE TU, ILA NI WATU MAKATILI SANA...

BORA UTAWALIWE NA MZUNGU KULIKO MCHINA, MHINDI AU JAMII ZINGINE ZA KIBUDHHA BARANI ASIA...
Usiseme "Bora tutawaliwe na mzungu" bali sema inafaa tujitawale wenyewe kwa kujiimarisha na kuepuka misaada maana mitego yao mikubwa iwe America, Asia na Ulaya ni misaada tu ili kujenga ushawishi wao, tukishinda vishawishi vya misaada tutakuwa huru kifikra.
 
Wengi umeongea shit sana Kwa mchina Ila mnafanya unafki wa wazi uku mkijua wazungu Kwa miaka Mingi walikuwa wanatoa bidhaa zao Kwa gharama kubwa kuliko mchina Leo hii tunanunua bidhaa kiurahisi Kwa gharama nafuu sababu ya mchina miundombinu yetu Mingi ya barabara imejengwa Kwa gharama nafuu toka Kwa mchina kuusu mikataba tunayoingia uwo ni ulafi wa watawala wetu huwezi mlaumu mchina Kwa Tamaa za viongozi wetu wachina wanatoa rushwa ndyo kupata tenda lakini viongozi wetu hawafikirii miaka kumi mbele kipi kitatokea tulipata mkopo toka benk za China kwenye bomba la gesi lkin Hadi Leo bomba linapitisha asilimia 6 tu ya gesi inayotakiwa kupita vipi na apo utamlaumu mchina wachina wanapata tenda Hadi ulaya na America lakin viongozi wao wanafata sheria zao uku kidogo mkipewa vipesa mnasahau madhila wanayopitia wananchi na kujiangalia wenyewe
 
Well said, barikiwa sana - ukweli wa mambo ni kwamba Chinese Govt is helping Africans to help themselves unlike Western Govts,we angalia China ilivyo endeleza Continental Africa 4 the better in terms of ujenzi wa infrastructure,uwekezaji kwenye viwanda, Agrobusiness nk. Halafu kuna baadhi ya Waswahili wanadai kwamba Wachina si watu wazuri ni wezi, wanasahau kabisa kwamba African Govt Officials ndio ushinikiza Chinese companies ku-inflàte gharama alisi za tenda ili wapate cha juu - niliwahi kuwasikia Wachina wakilalamikia ushenzi wa baadhi ya African Govt officials kuhusu kudai rushwa iliyo pitiliza mipaka, mwisho wa siku wanakuja kulahumiwa Wachina, mbona Wachina wakipewa tenda za ujenzi huko Ulaya na Amerika kusini mbona hatujawahi kusikia wakilalamikiwa na mataifa hayo?

Ukweli ni kwamba wanao waharibia sifa Wachina ni media za kimerikani ndio ueneza stories za kutunga tutu: Mara atambiwa Kenya itapata hasara kubwa kutokana na ujenzi wa reli ya SGR unaosimamiwa na Wachina pamoja mkopo kutoka China ambao haulipiki, reli yenyewe haijakamilika sasa wanajuaje kwamba Kenya itashindwa kulipa mkopo? Mara sijui Sri Lanka imerubuniwa na Uchina kuwauzia Bandari kwa bei ya kutupa,Mara Wachina wamewarubuni Wazambia kuwauzia migodi ya Shaba kwa bei ndogo sana, wakati wakijua wazi wazi kwamba migodi ya Shamba huko Zambia ilikuwa ICU, imekuja kufufuka baada ya Wachina kuingilia kati kwa makubaliano na Serikali ya Zambia.

Kwa kifupi major projects za Wachina Duniani kote zinafuatiliwa kwa karibu sana na Serikali za magharibi, halafu wanatumia vyombo vyao vya habari kupotosha/tisha watu Duniani kuhusu ubaya wa Wachina - crusade against China rise imesukwa kweli kweli na Serikali za Uingereza na Amerika wanawanunua mpaka waandishi wa habari wa kiafrika kueneza propaganda dhidi ya Wachina USA hawataki Uchina iwapiku kiuchumi na jeshi ndio maana wanaedeleza hujuma za chinichini dhidi ya Uchina.
 
Back
Top Bottom