Uraia pacha kwa taifa changa ni kifo kuliko faida


Mwambie huyo. Hapa kwenyewe hatuna uraia pacha ila watu wanaiba kama kawa
 
Chunguza sana,wenye uraia pacha ndio wengi ni magaidi,wacha hawa wanaotumiwa kutekeleza ugaidi,kuna wanaoingia kutoka nje,wana uraia pacha au ni raia wa nchi husika,lakani ana passport ya UK au Amerika au kokote,imeandikwa kazaliwa Somalia,wakati ni mtanzania,hata kisomali hajui,wapo mpaka the wanawake,kutafuta wenyeji wafanye ugaidi kwa kuwashawishi,kuwalipa pesa,wafanye ugaidi.
 
Hapo tatizo sio uraia pacha wala uchanga wa nchi bali tatizo liko kwa wale waliopata dhamana yakuongoza hii nchi toka mkoloni hadi leo bado wameshindwa kuweka mifumo thabiti yakuondoa hizo kasoro ulizozianisha.Na hizo akili kamwe hawawezi kua nazo ndio maana option kwao ni kukwepa hiyo hoja badala yakutafuta ufumbuzi.Mapungufu yote uliyoyataja yanarekebishika.Sasa tunatakiwa tusubiri miaka mingapi ili tuje tupate serikali itakayolinda rasilimali za nchi na mambo mengine yenye manufaa?..
 
Wewe ni mjinga katika wajinga wa Tanzania wewe ni mpumbavu hasa huna uelewa wala huna vision .Uraia pacha haukimbiliki lazima watafanya tu kwa sababu Tanzania siasa zake zinaendesha na Bwana wake Kenya .Kenya ikifanya kitu lazima TZ watafanya tu hata kama watachukua muda hizo fikra ni za kimasikini.
 
Kwenye hii thread kuna watu wako serious sana. Unfortunately mwenye thread yake either hayuko serious or haelewi 😂 😂
 
Sawa bosi!

Endeleeni kufyatua maelfu ya wahitimu na kuwarundika mitaani bila ajira wala misaada yo yote ya kimfumo huku mafisadi yasiyozidi 50 yakiiba raslimali zote na kujirundikia mali bila huruma. Siku moja mtakipata tu mnachokitafuta.

I am out 🙏🏿

 
Uchanga upo ukilinganisha na nchi km UK, USA n.k. nchi iliyopata uhuru mwaka 1013 utalinganisha vp na ya 1961? Tofauti ipo wazi ukizingatia hao waliokutangulia hakupi fursa zaidi ya kukukandamiza
Hata kama ikiisha miaka elfu moja kwa akili hizo hizo bado tutajihesabu ni wachanga maana nchi hizo ulizozitaja zilitutangulia kupata uhuru.Umri wa mtu mzima ni miaka Ishirini,kama miaka yetu ilishavuka huo umri hakuna uchanga hapo tatizo ni kujipanga.
 
Niambie mfano wa taifa dogo kama letu ambalo linafaidika sana na uraia pacha kiasi cha kutamani kuiga maisha na hali yao kiuchumi, kijamii na kisiasa. Mnatafutia majizi njia nyepesi ya kutoroshea nje mali zetu.
Tatizo huna exposure ... nenda ghana ukaone diaspora wanavyofanya mambo makubwa

Wanajenga malls, wana viwanda , migahawa na wamewekeza heavily kwenye kilimo

Ukienda ghana especially accra utaona expensive cars kila sehemu unayoenda hao ni diaspora wamechangamsha uchumi na kutoa ajira kwa watu wengi sana

Sasa nyie endeleeni na ujima wenu wa kukataa uraia pacha huku nchi ikiendelea kuwa maskini wa kutupwa.
 
Bro umeongea fact ila bado haujatupatia mofano halisi ya hizo nchi
 
Yaani umeniacha kapa la kuongeza. Umeeleza vizuri sana..heko mkuu
 
Aliyewaambia watanzania ni matajiri sana, kila mtu anawaonea wivu na anataka kuwaibia aliwajaza ujinga wa kiwango cha lami. Mmekua mazuzu na woga kama kunguru. Kila kitu mnaogopa
Kama watanzania ni masikini unataka uraia pacha wa nini? kaa na uraia wa sehemu tajiri. Sisi huku ni masikini jeuri. Ukifungua mlango wako wataingia wema na wezi, na shida yetu sio wema bali wale wezi wa ndani na nje. Ukikarbisha mgeni nyumbani hakikisha kuwa mwenyeji unakuwa wa mwisho kwenda chumbani kulala na funga mlango na nenda chumbani na ufunguo wa milango ya kutokea ili kuhakikisha kuwa mgeni hakuibii na kutoroka. Hatuwezi kuruhusu uraia pacha eti ili tupate read made wachezaji mpira wa timu yetu ya taifa (non sense) badala ya kuwekeza kwenye soka la watoto na vijana.
 
Serikali iko tayari kuruhusu wadada kwenda kufanya kazi za ndani nje, kuliko kutoa uraia pacha. By the way Nikipata gape siwezi kuishi bongo, imagine unasoma huku unawaza kama utaweza kuishi maisha ya standards, maana no ajira, no mitaji🚶🚶
 
Amani iliyoko Tanzania hats marekani haiko Na haipatikani. Hakuna amani kabisa kufa ni kitu cha kawaida kabisa, upweke (loneliness) mkubwa, madeni mengi, homeless mengi, wenye stroke na stresses wengi, kila kitu ghali sana.
Unazungumzia amani au maisha bora au nini hasa unachozungumzia maana nimeshindwa kukuelewa?
 
Huna akili.

Nimejisikia vibaya sana kukwambia “huna akili”
Ila nilikuwa sina jinsi.
jizi ni jizi tu, haliwezi kujibu hoja kwa hoja hiyo inafahamika. Sababu ziliwafanya Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli wasiruhusu uraia pacha wala hata kuujadili zingali zipo valid mpaka leo. Wahindi wengi hapa wana uraia pacha, fedha zao nyingi zinachumwa Tanzania na kwenda kujenga nchi za canada, uingereza, marekani kwasabu ya urahisi wa kuingia na kutoka kama raia. Wanahodhi ardhi yetu hapa na kwenda kuikopea canada.
 
Hakuna uraia pacha na bado tunapigwa..
Wacha uwepo bana sio kesi
 
Aliyewaambia watanzania ni matajiri sana, kila mtu anawaonea wivu na anataka kuwaibia aliwajaza ujinga wa kiwango cha lami. Mmekua mazuzu na woga kama kunguru. Kila kitu mnaogopa
Kuna huu ujinga wa kukaririshwa amani kana kwamba dunia nzima ipo kwenye vita kama Ukraine au Gaza ila Tanzania tu ndio ina amani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…