Uraia Pacha, Wanadiaspora Mshukuruni Rais, sasa mnatambuliwa rasmi kwa Special Status ya Diaspora Tanzanite Card, una enjoy baadhi ya Haki za Uraia!

akili zao zinafanana.
Mie kuna muda hadi nasemaga inawezekana Tanzania tulilaaniwa kweli.

Ukiangalia akili za Viongozi wetu na watendaji wetu unaweza kulia kweli.

Ukiwauliza ni kwa nini tusiwe na uraia pacha hayo majibu wanayokupa unaweza fikiri hii nchi inawezakana Mungu alitunyimaga akili tofauti na nchi zingine duniani. Ni kama tunafikiri kwa makalio badala ya ubongo
 
Bongo land
 
Special status ndiyo upuuzi gani huo?
 

I couldn't agree more.
 
hebu eleza faida za uraia pacha, binafsi sizioni
 
Wanachofanya Wajanja. Hata siku moja usitumie passport ya nchi nyingine kuingia TZ Tumia ya TZ tu.

Ukiwa na passport ya Sweden, unaondoka huko na passport ya Sweden. Ukifika Dar unaificha na kuchomoa ya TZ. Unaingia TZ kwa passport ya TZ.

Wakati wa kuondoka pale kwenye ndege wakati wa ku check in unatoa passport ya Sweden. Ukishamaliza unaiweka ndani. Unaenda immigration desk na passport ya TZ na kuweka vidole vyako na kuondoka.

Sio kazi ya Uhamiaji kujua unakoenda una visa au la. Hiyo ni Kazi ya watu wa ndege.

Kwa taarifa yako watoto wengi wa viongozi ndio wanafanya hivyo Kwahiyo hawawezi kubadili utaratibu.

Ikija serikali isiyo ya wahuni wata kubali uraia pacha.

Nimekupa majibu, tunga maswali yako.
 


Tatizo la uraia pacha hakuna hata mmoja hasa kwa wazawa na hata Kenya tumeona hakuna tatizo kabisa. Kuna wasomi wengi sana kwenye academia nje yaani Watanzania ambao nio Prof huko ni wengi sana sijui kwanini jamii ya wasomi kama Prof wetu waziri wa Sheria ni waoga sana na wana ego sana na hawa wataalamu wa nje kiasi cha kuogopa watu wanaojua kuliko wenyewe. Tumepoteza fursa nyingi sana
 
Wengine tushavurugwa hatutaki uraia pacha wala special status.

Na Bongo tutarudi kwenye misiba mikubwa ya familia tu.
 
Kaka Paskali za masiku,
Hii issue ya diaspora na uraia pacha bado hatujafikia kiwango cha kuishukuru serikali kwa sababu bado ifanya wajibu wake kama kwa hisani vile.

Kitu tunachofahamu ni kwamba CCM inahofia Watanzania kuwa na uraia pacha kwa sababu hali hiyo inatishia nafasi ya Masultani ndani ya CCM kukoma kutawala milele. Kinachotakiwa ni kusema ukweli kwamba HATUA ILIYOFIKIA HAITOSHI KUPONGEZWA bali serikali inapaswa kufanya zaidi ya hapo.

Ninachokiona ni kwamba nchi yetu imekuwa na vitambulisho holela hadi kufikia kupoteza maana ya utambulisho. Mfano mzuri ni ile kadi ya BVR kisha tuna kadi ya NIDA kisha unahitaji passport na kadi chungu mzima. Serikali inatuhadaa kila tunapokaribia uchaguzi ndo maana mimi ninaona kabisa kwamba hatua hii bado siyo ya kupigia makofi
 
Hakuna haja ya Mtu ailyepoteza Uraia wake kw akuchukuw aUrai wanchi nyingi apewe ( Special Status ya Diaspora Tanzanite Card) Ushauri Wangu Waruhusu kabisa uraia Pacha M-Tanzania anaweza kuwa na Uraia wa nchi yake na nchi nyingine anayoipendakuwa Raia. Serikali yetu inachoogopa nini M-Tanzania kuwa na Uraia Pacha? Wakati Nchi kubw aduniani ka Marekani na uingereza Wana Uraia Pacha? Au jirani yetu Kenya pia anaruhusu Uraia pacha iweje Serikali yetu kwanini iogope M-Tanzania kuwa na Uraia Pacha?mimi ninashangaa kweli bado tupo nyuma Kimaendeleo Wenzetu wanafikiria mambo makubw aya maendeleo sisi bado tupo Bungeni tunajadili Uraia Pacha? Nchi yetu itachukuwa Miaka 1000 ijayo kuwa na maendeleo ya ukweli tupo nyuma kwa kila kitu. Tujifunze kw amajirani wetu walioruhus Uraia Pachajamani mbona tumekuwa wajinga namna hiyo?
 

Ukitoka Sweden na passport ya Sweden inamaanisha ukifika Tanzania, pale immigration ukaonyesha passport ya Tanzania itakuwa haina visa wala muhuri wowote wa Sweden.

Unapotaka kusafiri na passport ya Tanzania obvious haitakuwa na visa ya Sweden watajiuliza unaendaje Sweden, unapandaje ndege yoyote bila visa.

Wanaweza kujiuliza pia unaishiji Sweden, kwahiyo wakahisi of course utakuwa na passport nyingine.
 
Kama umekana uraia wa nchi yako si ubaki na nchi uliyoipenda. Umalaya wa uraia nao si mzuri kubaki njia moja ni muhimu.
 
Kwa akili kama hizi no wonder nchi yetu ni masikini hivi.
Tanzania itajengwa na watanzania na si na watu wasioweza kuamua uraia wa nchi zao. Kama hutaki kuwa raia wa Tanzania si ukae huko unakopenda, acha kuwa kigeugeu. Mwisho malaya hao wa uraia watakuja kutaka hata uongozi wakati hata msimamo wa uraia hana amebaki kutangatanga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…