Pascal huu ni ujinga na upumbavu uliopita kiasi wanaopendekeza hawa. Hivi wana akili sawasaa kweli? Kwa haraka haraka ngoja nikuambie;
- Special status tofauti na uraia pacha ina expire kila baada ya miaka kumi. Usipo renew unakuwa huna special status na mali zako ulizowekeza nchini kuwa hatarini kupotea
- Special status hairithiwi. Yaani nawekeza hata Dola bilioni moja, ikitokea nikafa watoto wangu hawana haki ya kurithi mali kwa sababu special status inakuwa granted kwa mtu mmoja. Tofauti na hili, nikia na uraia pacha, uraia wa Tanzania na USA, watoto wangu nao wanakuwa na uraia huo
- Vipengele vya kukunyang'anya special status ni vyepesi mno! Kw mfano, unaongea na enemy of Tanzania. Hebu watuonyeshe list ya enemy of Tanzania ndio tujue nani tusiwasiliane nae kama tuna special status. Katika ubinafsi na roho mbaya na corruption ya Watanzania wengi, ku-revoke special status satus siku zote itakuwa ni rahisi sana. Usipomsifia raisi inaweza kuwa revoked
- Kwa mfano, mtu anaweza ku-revoke on basis of is of "good moral standing". Kuna sheria kuhusu moral standing? Kwa mfano, kuwa mlevi, kuwa fuska, kuvaa nguo fupi, skin tight, nk, kuna watu wataona ni bad morals. Sasa unaweza kunyanganywa special status kwa sababu mtu anasema wewe mlevi, wewe fuska. Sasa hiyo clause imeandikwa na mwanasheria kweli? Sio mwanasiasa au mtu anaedhani kunywa pombe, kuvaa mini skirt ni dhambi? Kuwa na bad morals is not necessarily ku-commit crime, na the aspect of morals can be very subjective
Sasa ningeona hawa waliopendekeza special status kuwa na akili kiasi kama wangesema special status ni permanent, na parent akiwa na special status automatically watoto wanakuwa nayo. Hii nchi imejaa vichwa maji katika jina la viongozi. Waondoe hili wazo lao la special status, hakuna mtu mwenye akili timamu atakubali ujinga kama huu ili eti awekeze mtaji mkubwa nchini.
La sivyo njoo Tanzania na special status yako uwekeze halafu uliwe!