Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Acheni kutupigia kelele za Membe,ni walewale tu.

Si nyie mliokuwa mnatuaminisha kwamba mkulu ndiye mfano halisi wa Nyerere? Tena mkaenda mbali zaidi hadi kumuita ‘mpakwa mafuta’?

Shida ya nchi hii sio mwananchi namba moja bali mifumo iliyopo,katiba na sisi wananchi wenyewe hatujielewi tunataka nini na hatuna utayari kwa hata hayo machache tunayojitanabaisha kuyataka.

Ila lazima nikiri kwamba bora ya Membe kuliko...
 
Mwanzoni walisema awe Rais wa Maisha....

Mkashuka mkasema aongezewe iwe 7 kwa awamu....

Ghafla mnataka mnyima hata awamu ya pili...yani 5 tu imtoshe!!!

Masisiem em tuelezeni kuna nini huko!??
 
Ngoja tuone hii movement..2015 ilikuwa lowasa..hawa huwa wanafurahisha sana harakati zao
 
Me ni CCM nampenda Sana Membe
 
Anayeongelewa ni yule yule aliyekuwa waziri awamu ya nne au ni mwingine? Tusisahau Mungu bado anaipenda TZ. Alituepusha na Membe 2015 japo alikuwa na sapoti ya vigogo lakini Mungu akasema NO. Ingekuwa Mungu anapokea rushwa ni wazi Membe anaweza kuwa rais wa TZ. Mungu hata siku moja hapokei rushwa na bado anaipenda saaana TZ.
 
Membe hana tofauti na Lowassa kwa wizi/ufisadi…..hafai hata kidogo kuwa rais.
 
Sikuingia JF kwa siku kadhaa lakini leo na jana naona jina la BM linatrend. Kwani amesema au kufanya nini karibuni hapa? Au ndio anaundiwa Zengwe
 
Mkuu kuna mambo ya kuyatafakari kwa kina sana,Magufuli hatakiwi ndani ya chama na nje ya chama.
Ni Rais pekee anayechukiwa na watanzania kuliko marais wote waliopita,na yeye analijua hilo kabisa,sasa hatokubali kukataliwa ndani CCM na nje, atatumia nguvu kubwa kubaki madarakani na hapo mauaji makubwa mno yatatokea.
Magufuli ameshajiandaa kwa yote,na ndo maana akaiba ile 1.5 trillion kwa ajili ya 2020, ndugu huo utakuwa mwaka mbaya zaidi kwa Tanzania, damu itamwagika mno.
 
Membe oyeeeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…