Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Acheni kutupigia kelele za Membe,ni walewale tu.

Si nyie mliokuwa mnatuaminisha kwamba mkulu ndiye mfano halisi wa Nyerere? Tena mkaenda mbali zaidi hadi kumuita ‘mpakwa mafuta’?

Shida ya nchi hii sio mwananchi namba moja bali mifumo iliyopo,katiba na sisi wananchi wenyewe hatujielewi tunataka nini na hatuna utayari kwa hata hayo machache tunayojitanabaisha kuyataka.

Ila lazima nikiri kwamba bora ya Membe kuliko...
 
Mwanzoni walisema awe Rais wa Maisha....

Mkashuka mkasema aongezewe iwe 7 kwa awamu....

Ghafla mnataka mnyima hata awamu ya pili...yani 5 tu imtoshe!!!

Masisiem em tuelezeni kuna nini huko!??
 
Ngoja tuone hii movement..2015 ilikuwa lowasa..hawa huwa wanafurahisha sana harakati zao
 
“Binadamu wote ni ndugu zangu, Afrika ni moja”

Kwako Bernard Kamilius Membe

Nimekusikia muda mrefu toka wa wandani wako kua una mkakati wa kuingia magogoni 2020 iwe ndani ya CCM au nje ya CCM!

Binafsi sishangai wala kukukatisha tamaa kwakua umenuwia kuusaka Urais kwa njia halali kabisa yenye misingi ya kisheria.

Pili natambua umeamua kuwania ili Kumsaidia Rais wa sasa na mwenyekiti wako kwakua amekiri hadharani kuwa hii kazi ni ngumu mno kwake na haiwezi... alifika mbali zaidi kwakusema hii kazi alisukumiziwa tuuu.... aliibipu ikampigia hivyo kuleta picha kwamba aliingia huku hajui anakwenda kufanya nini. Hii imeonekana kwakuwa hadi sasa hana focus wala Vision!

Ushauri wangu: kama unataka urais wa nchi hii lazima ufanye patano la agano na Edward Lowassa!! Bila Lowassa 2015 leo hii Magufuli angekua anavua samaki Kwao Chatto!! Ni Lowassa aliyemfanya JK awe Rais 2005 na ni Lowassa aliyemfanya Magufuli awe rais 2015 na wewe ukakosa!! Sina sababu yakuelezea kilichotokea kwakua unafahamu!!


Mwenzako Mzilankende amejipanga!! Sasa anaileta Team Lowassa miguuni pale!! Akina Sophia Simba soon watawekwa kwenye hatamu na akina Ole Millya! Sasa kama hii team haikuungi mkono sahau kabisa urais iwe 2020 au 2025!! Mlifanya makosa sana kuhitilafiana vinginevyo leo ungekuwa kwenye first class!!

Narudia tena uwe wewe.. January Makamba ama Ridhiwani Kikwete bila kuunganisha nguvu na laigwanani katu hamtatwaa madaraka ya juu ktk nchi hii.


Hivyo fanya harakati muunganishe nguvu!! Huku akiwepo Maalim Seif kule Mbowe huku Lowassa nakuhakikishia hata Magu akimweka mtoto wa kumzaa awe mwenyekiti wa NEC na kujaza ndugu zake hatafua dafu kama alivyoshindwa Yahya Jammeh aliyeweka ndugu wote tume ya uchaguzi na akaangushwa vibaya.

NB: Huu ni ushauri halali hasa kwa kuzingatia kila raia ana haki ya kugombea... kuchagua na kuchaguliwa kuwa kiongozi yeyote kwamujibu wa katiba yetu.



MUNGU IBARIKI AFRIKA!
Me ni CCM nampenda Sana Membe
 
Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020
Anayeongelewa ni yule yule aliyekuwa waziri awamu ya nne au ni mwingine? Tusisahau Mungu bado anaipenda TZ. Alituepusha na Membe 2015 japo alikuwa na sapoti ya vigogo lakini Mungu akasema NO. Ingekuwa Mungu anapokea rushwa ni wazi Membe anaweza kuwa rais wa TZ. Mungu hata siku moja hapokei rushwa na bado anaipenda saaana TZ.
 
Membe hana tofauti na Lowassa kwa wizi/ufisadi…..hafai hata kidogo kuwa rais.
 
Sikuingia JF kwa siku kadhaa lakini leo na jana naona jina la BM linatrend. Kwani amesema au kufanya nini karibuni hapa? Au ndio anaundiwa Zengwe
 
Kwa taarifa yako na hili bandiko lako refu JK alimtaka Membe na kwa sababu ya hiyo nguvu ya Lowassa ndani ya ccm ndio iliyopelekea Magufuli kuitwaa hiyo nafasi. Usitake kumpa JK sifa asiyokuwa nayo. Na huyu Magu na vile hawezi siasa za ushawishi ndio atapigwa chini kirahisi. Huu ndio mwisho wa kikundi cha utekaji na kupiga risasi wengine.
Mkuu kuna mambo ya kuyatafakari kwa kina sana,Magufuli hatakiwi ndani ya chama na nje ya chama.
Ni Rais pekee anayechukiwa na watanzania kuliko marais wote waliopita,na yeye analijua hilo kabisa,sasa hatokubali kukataliwa ndani CCM na nje, atatumia nguvu kubwa kubaki madarakani na hapo mauaji makubwa mno yatatokea.
Magufuli ameshajiandaa kwa yote,na ndo maana akaiba ile 1.5 trillion kwa ajili ya 2020, ndugu huo utakuwa mwaka mbaya zaidi kwa Tanzania, damu itamwagika mno.
 
Baada ya Jana na Leo kufululiza thread za hiki kichwa adimu, aghalabu nyoyo za wadanganyika zimepata faraja, pengine faraja na neema tulizoziishi enzi za baba Ritz zinatarejea.
1. Mmefanana hulka
2. Umakini
3. Upole na kusikiliza maoni ya watu
4. Ubobezi wa kidiplomasia
5. Halafu wote mlianzia mambo ya nje
6. Marafaki wa mataifa
7. Very smart katika maamuzi
Twende na Membe 2020
Membe oyeeeee
 
Back
Top Bottom