Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Paschal kuna Uzi alianzishaga kuhusu JPM kuwa Raisi humo umu. Naamini Raisi huandaliwa mapema mno ni sisi tu hatujui@Paschal Mayala
kuandaliwa kupo kwa aina mbili
_system kukuandaa
-kuandaliwa katika ulimwengu wa roho...
Unaweza kuandaliwa na system lakini connection na rohoni kukakukataa hapo piga ua hautapita
unless otherwise itokee kitu "Fulani"
Membe na Mr lowassa wao walijiandaa ki system but katika ulimwengu wa roho walikataliwa.
 
Wadau tupeane hoja makini hapa.Unadhani Membe angekuwa Rais leo angechukua hatua gani sala la Korosho!? Tungefika hapa tulipo leo!?
Angembeba aliyempelekea hela ya kampeni
 
Hahhaahhaa... Pole Mkuu.

Tafuta sunday class hapo jirani la English Course.
 
Mods naomba msinichanganye Thread yangu na hizo thread ambazo rasmi naona ziko kimkakati zaidi, na kama mtanichanganya basi nitawaona au nitalazimika kuamini kwamba nanyi ni sehemu ya mkakati huo.

Leo na siku chache nyuma kumeanza kuwa na thread nyiingi humu zikimhusisha Bernard membe aliyeukosa urais 2015 akigombea ndani ya watia nia ndani ya CCM.
Wanaoweka thread zao humu ni watu ambao avatar zao zinajirudia rudia. (Jambo linalotia shaka na kutuaminisha kuwa huu ni mkakati.)

Mimi sitaki kurefusha stori bali nauliza yafuatayo .
;kama membe ni mwanadiplomasia mahiri (kulingana na wanamkakati hawa).

Mbona hatusikii akiitwa hata kwenye utatuzi au usuluhishi wa migogoro mbalimbali ya kidiplomasia duniani, mzee mahiga amekuwa muda wote akilipaisha jina la nchi hii kwa kuitwa mara nyingi na kukabidhiwa majukumu makubwa ya kidiplomasia ikiwemo IGAD kabla ya kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya nje aliko sasa hivi.na pia mzee Mkapa na Kikwete pia, ambako mpaka sasa mzee mkapa ni msuluhishi wa mgogoro wa burundi.
Tusisahau pia mama Aisha kigoda yeye alihudumu katika nafasi kubwa kabisa katika UN.
Pia tusisahau mama Getruda mogela na mama Anna tibaijuka waliohudumu sehemu mbalimbali katika UN HABITAT na jumuia ya madola.

Lakini huyu membe pamoja na kuhudumu mambo ya nje kwa muda mrefu, tangu alipotoka katika nafasi hiyo ni kama amesahaulika ndani na nje ya nchi.

Je mnaoibuka kimkakati sasa hivi na mkionekana rasmi kuja na staili ile ile ya kimtandao mnaweza kutuambia ni lini alijisafisha na kashfa ya fedha za Ghaddafi?(ambayo huenda Jumuia za kimataifa zinalitambua na kujiweka kando nae).

Na je kama yeye ni mwanadiplomasia mahiri,zaidi ya kutumia muda mwingi kujiandalia mazingira ya kuusaka urais, ni lipi alilotufanyia nchi hii kama waziri wa mambo ya nje, ambalo inaweza kumpa legacy kwa wananchi wazalendo wa nchi hii?
Na hivyo kutulazimisha kumuamini kwa hilo?

Na mwisho kabisa...ni kwa nini sasa ambapo kuna mgogoro wa bei ya zao la korosho huko mikoa ya kusini.

Angalizo:
Hii inaweza kutufanya wananchi tulazimike kumuamini vizuri musiba na Tamko lake juu ya majina Yale. Namnukuu nusiba.

1.subash Patel.
2.Abdulahman kinrana
2.Nape nnauye.
3.Tundu lissu.
4.Zitto zubery kabwe.
5.mlowola.
6.Yussuph makamba.
7.Aikael mbowe.
8.Massoud kipanya.
9.Said michael(cartoonist)
10:Rostam Aziz.

Na wengine wanne majina nimeyasahau lakini clip ipo YouTube.

CCM INA TARATIBU ZAKE ZA KUWAPATA WAGOMBEA WA CHAGUZI MBALIMBALI. kila muda unapowadia lakini hii ya mitandaoni sasa hivi tena ikichagizwa na Avatar za Chadema tunaowajua humu JF, hakika si bure!

Msituvurugie nchi yetu na kasi yetu mpya ya maendeleo. Mnapaswa kukemewa kama ukoma!
Walaaniwe wale woote waliokaa miaka zaidi ya 18 iliopita na kujiundia kundi la wanamtandao, maana umetuharibia nchi mpaka sasa inatusumbua kuirudisha kwenye mstari.

Kama huyu membe hakufaa kwa wana ccm kumchagua kwa wakati ule, ni sabuni gani kaogea hadi atufae kwa sasa!
Ahsanteni. Naomba kuwakilisha na tujadiliane kwa hoja si matusi.
 
Mpaka siku wapinzani watapopata akili kwamba kila tukio linakuja kwa kusudi maalumu ndio angalau wanaweza kucheza vizuri karata za siasa zao!

Nacheka sana ninapoona watu wamekumbwa na upepo huu wa sasa unaoendelea hapa mtandaoni eti kuna mtu awe rais alafu eti kirahisi tu hivi kama kunywa maji?

Niwaambieni wapinzani nyie hata muwekewe kujifunza kwa picha hamtakaa muelewe.

Ikiisha hii movie ya Membe jiandaeni na nyingine pia.
 
Mtamponza mzee wa watu hizi sredi za.membe imekuwa too much ngojeni muda ufike
 
''Sisi watanzania'' hao kina sisi unamaanisha nani na nani??? Maana unajumuisha watu as if tulikaa watz wote tukaamua huyo ugoro wako ulouleta...siku nyingine andika wewe na mke wako na familia yako sio..''SISI WATANZANIA''
Jitoe wewe na familia yako.sisi wengine tunaunga mkono hoja
 
Wala hawatongozeki kirahisi bali ni ma-low IQ tu, hawajaanza leo walianza kumsifia Kenyata, wakaja kumsifia Kikwete na sasa wamehamia kwa B.Membe, kwa akili yao ndogo hakuna kitu wanasimamia hivyo chochote kikija na Mbowe akiyaambia yanafwata yanafikiri yatamchonganisha na Raisi Magufuli!
 
BAVICHA mnachekesha sana, mmefikiria mtamfitinisha vipi Magufuli ndani ya CCM, mmeamua kuja na single ya Membe!

Makundi yalishasahaulika ndani ya CCM, sababu Rubani yuko imara na kutanguliza maslahi ya umma, kwa hivyo hategeki! Mtu ukiwa mchafu ndiyo utashambuliwa kila kona Kama alivyo Mbowe.

Naona maagizo ya CHADEMA ni kuleta threads nyingi za kuaminisha kuwa kuna mpasuko na Membe ana kundi! Hiyo ni post 2015! Tutaona maajabu mengi, tafuteni watu wenye akili na uzalendo wawatengenezee mikakati, lakini muwe tayari kusurubisha ubinafsi na maslahi binafsi, sijui Kama mtaliweza hili.
 
Back
Top Bottom