Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Uchaguzi 2020 Urais 2020, CCM twende na Benard Membe. Mwanadiplomasia nguli wa kuivusha Tanzania

Habari wakuu

Kutokana na hali inavyoenda ya uendeshaji wa nchi ni wazi rais anatakiwa abadilishwe kupitia sanduku la kura mwaka 2020

Hivyo sisi watanzania tunapenda na tunatamani kusikia sauti ya kiongozi wetu mpendwa mwenye nia ya kulivusha taifa kwa hapa lilipokwamia, ndugu, mheshimiwa na mwanadiplomasia Benard Membe

Jitokeze wazi tusikie kauli yako watanzania tufarijike kwani mwaka 2020 ni jirani sana

Nawasilisha
Nimetimiza miaka 10 ya ulevi, leo 9 octoba ni maadhimisho - JamiiForums

Umeona jinsi ulevi unavyokusumbua lakini
 
Naona kama mnajifurahisha, yaani naona kama Maigizo, watu na akili zenu mnakaa mnadanganyana Membe anaenda kuchukua nchi 2020.

Mimi na akili zangu za kuvukia barabara nauliza ATAPITIA NJIA GANI?

Ndani ya CCM , Mwenyekiti ndiye mgombea urais na ndiye mwenye sauti ya mwisho ,

Kupitia Upinzani ,ndio kabisa hawezi kushinda , Tuliona kwa LOWASSA,.
Labda kama ana hela za kuchezea,

Kupitia Uhaini, hapa atadakwa mapema sana..

NAWAULIZA NYIE MLIOKULA HELA ZAKE NA KUTUMWA MITANDAONI , MNAJUA ATAKUWA RAIS KWA NJIA GANI?

Mtuambie, sio mnasumbua mitandaoni lakini hamtuambii atapitia njia gani , ya golgotha au kaanani,

JIWE ameshajizatiti ana JESHI, TISS, UHAMIHAJI, POLIS , TUME YA UCHAGUZI,N.K

MEMBE ana nini? Au anataka kuliwa hela zake kama Lowassa?
Huku upinzani kwa sasa vimebaki vitoto vilivyotoka chuo visivyojua kutafuta pesa kwa nguvu zao zaidi.ya ajira serikalini na kudanga vina muda mwingi wa kushinda kwenye mitandao na kutukana havina hoja zaidi ya viroja.
Wenye akili na upeo mkubwa karibu wote wanaondoka.

Ukiangalia kelele za "Membe" kwa mwenye akili anaona tu kuwa kuna vichekesho mahali fulani, wana njia mbili au tatu..

1: waasi ili itokee CCM B kisha atangazwe kuwa mgombea ambaye ataungwa mkono na baadhi ya wanaccm wenye maslahi binafsi.
Hii inawezekana kama afanyavyo Cilos Chilima wa Malawi..kwa sasa..

2. Aondoke kisha ajiunge na upinzani uliopo sasa awe badala ya lowasa..

3. Apitishwe na kamati na vikao vya CCM kwa sabbu yoyote ile.

4. Afanye mapinduzi ya kumtoa rais madarakani kwa njia isiyo ya kidemokrasia.!

Kati ya hizo hapo juu huenda akawa rais.

Mwisho kama wengine walivyosema kuna watu wanajaribu kutengeneza picha kuwa wapinzani wanatekwa na kupotezwa.!
Wanaweza kutumia mtego huu ili kutengeneza aina fulani ya taharuki kwenye jamii. Kisha wakajaribu kutimiza lengo lao.

Sio wa kupuuzwa kwa namna yoyote.
 
Tunahitaji Raisi kwaajili ya Tanzania na watanzania, Hatuhitaji Rais kwaajili ya mataifa ya nje. Magufuli anatosha. Huyo Maembe abaki tu kuwa Rais wa mioyo yenu km Lowasa.
 
Membe hana tofauti na Jiwe....Muwekeni Warioba hapo Mwansheria Mkuu Tundu lisu waiweke sawa nchi miaka kama 5 hivi wapike vijana wa ukweli Apart from That tukubali tu kuwa hii nchi mpaka mwisho wa dahari Itakuwa hivi hivi au hali itakuwa Mbaya zaidi
 
Membe ukimsikiliza anaongea kwa umakini mkubwa wala haongei kwa kufokafoka kila saa kama vile anafokea watoto wadogo, Membe analugha ya kidiplomasia maana yeye ni mwanadiplomasia mashuhuri. Hata penati aliyokosa samatta juzi juzi angekua Membe angeipata tu maana angatumia diplomasia kufunga Goli.
 
Ingawa magu anaelekea kushindwa mimi siwezi kumuunga mkono membe bali ntamuunga mkono magu amalize tu muda wake
 
JPM ndo Rais bora mpaka sasa...apunguze tu umwinywaji wa demokrasia..Awe fair kwa kila mtu..Membe ataturudisha kwa JK..JK alivuruga sana uchumi.
 
Ni bora hao wanaodokoa kidogo kuliko wanaokomba kabisa ,na kutishia wanaohoji juu ya ulafi wao kama kakikundi


Lowassa na Membe wamekomba kidogo? Nani kakudanganya…...wale hawafai ni zaidi ya mafisadi wale wazungu wa migodi.
 
Nimecheka Sana hii combination ya Chadema na ccm haijawahi tokea kweli Membe for presidence

Nini kimetokea kwa elimu yangu hapa nimetoka kapa kabisa labda ikifika kesho Jtatu nitajua maana Leo Jpili

Kweli siasa ya science Huu upendo na kupendana kwa ccm na Chadema nini kimetokea?
Probably fighting common enemy
 
Tuache uongo sio kweli kabisa kuwa eti lowassa ndiye aliyemuweka jk mafarakani,huu ni uongo na ujuha wa mwaka
 
bora aje yeyote atakaye jali maisha ya watu kuliko huyu anayejali vitu kuliko watu. et wasaliti hawastahili kuishi kisa tuu wanapinga mfumo wake wa uongozi.

yaan wanatekwa wanapotezwa wanapigwa risasi mchana kweupe bila hata haya harafu nikushangilie nitakua mwehu.

kwangu mm uzima ni bora kuliko maendeleo japo nayo hayapo. kunamaendeleo ya matangazo tu ila maendeleo halisi hakuna.

membe simkubalu kabisa maana naye anaonekana ni wa visasi. aliwahi kusema akishika urais watu 11 wajiandae kukimbia nchi. so naye ni wale wale. so mm nitachochea. huu moto ili uko mbele nitafute pa kupenyea na kushika madaraka.
 
Back
Top Bottom