Uchaguzi 2020 Urais wa CHADEMA moto: Kampeni zaanza kwa kishindo, Msigwa na Lissu hapatoshi !

Sheikh Yahaya kafufuka au utabiri huu kautolea kaburini?
Halafu usipotoshe, Magufuli hajamlipia faini Msigwa. Alijileta kutaka kumlipia lakini wanachadema ndio walio mlipia kupitia vijisenti vyao.

Mkuu, si mambo ya Sheikh!
Mwenendo na matendo tu!
Ina maana mkuu hukuwaona akina Selasini na Komu walivyokuwa wamebadilika?
Zipo ishara tu, zinazoweza kutumika na kuonesha muelekeo wa mtu flani katika siasa wakati flani!
Kuhusu hilo la Magufuli kumlipia, ni kweli cdm walilipa kwa ile michango n.k ndipo ikatoka taarifa kuwa Magufuli kamlipia baada ya familia yake kuwasiliana nae kuomba msaada! Sasa ni nani alikuwa anajua kabla kuwa familia yake na Magufuli walikuwa wakiwasilana kwa ajili ya ule msaada!?
...Yapo mengi nyuma ya pazia mkuu!
Hata akina polepole walipokwenda na yale mashangingi yao amini kuwa kabla kuna mambo yaliyokuwa yameshapangwa!
 
Kulipiwa faini na magufuli ni "classical bribe"

My take:-
Never let a politician grant you a favor because he will control you forever.
 
Kweli Urais wa Tanzania umekua rahisi sana,mpaka Msigwa?
 

Ikitokea ukatokea muujiza wa kipekee kabisa kwamba Mh. Lowassa akaamua tena kwenda kuwapa kampani, akachukua form ya Urais na kuwaambia kuwa amekuja kuwasaidia kuziba pengo lililopo la mgombea Urais.

Na hivyo amekuja kuwasaidia agombee halafu baada ya uchaguzi atarudi tena nyumbani kwake CCM, pamoja na mapungufu yote haya kwenye mchakato wao, CHADEMA wanaweza kupata kura nyingi zaidi kuliko ambazo watapata bila ya kuwa na Mh. Lowassa.
 
Kampeni?
 
Upande wa pili najulishwa kuwa fomu kwa ajili ya mgombea urais itatolewa moja tu.
 
Katika nyakati fulani pale Ufipa Street waliwahi kuibuka Vijana waliojipa jina"KIZAZI CHA KUHOJI"...Hawa pamoja na kujipa Haki ya Ku
hoji wakati huo huo wakikinzana na Utamaduni na haki ya wengine kuhoji swala la Tundu Lissu.

Kizazi ambacho kilikuwa Mstari wa Mbele kutuita "MAKATILI" wale tu tuliojaribu Kuhoji uhalisia wa Tukio la Lissu la tarehe 07 September 2017, tukio la Risasi 54 za SMG pamoja na Shuhuda Mkuu Dereva wetu Rambo from Wodi ya Saikolojia Brussels!.

Hebu tumsikie Msigwa kidogo akihojiwa Redioni! (Nanukuu).

"Sio kwamba simuungi mkono Tundulisu hapana,ila mara kadhaa amekuwa mtu mwenye tamaa ya kutaka yeye ndio aonekane wa maana wengine tuonekane takataka, nakumbuka mara baada ya tukio la risasi pale Dodoma,alipofika Nairobi akaniambia Peter this is my ticket and I'm going to win,sasa kutumia tukio kama lile la kupigwa risasi kwa ajili ya kutaka sympathy ya kura au nafasi ya kugombea urais si sahihi, nimezungumza na mwenyekiti wetu Mbowe, amenijulisha kuwa nafasi zitatoka kwa yeyote atakayehitaji mwenye vigezo na amesisitiza chadema ni chama cha demokrasia hivyo hata wanaompiga vita Nyalandu wanakosea sana" - Peter Msigwa (ILASI FM 2020).

#Note : Msigwa anatafuta nini kuanza kugusia Tukio hili?..Time Factors
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…