Urais wa Maisha: Baraza la Maaskofu na Kadinali Pengo wapo?

Urais wa Maisha: Baraza la Maaskofu na Kadinali Pengo wapo?

Swala la ukimya viongozi wa dini kwa maneno yaliyosemwa Bungeni na Andunje Ndugai na vikaragosi vyake halitakiwi kuhusishwa na dini bali sote tulillaani kwa nguvu zote. Raisi awe Mkristo au Mwisilamu hatakiwi hata kidogo kuichezea katiba kuhusu kipengere cha muda wa kukaa madarakani. Siku hizi andunje anajikomba sana kwa bwana mkubwa ili amnusuru cheo cha Uspika kwenye Bunge lijalo.
Wao Rais akiwa muislam mbona hawakai kimyaa?
 
Magufuli hana ubavu wa kujiongezea muda akitaka kuona nguvu ya jeshi(JWTZ) na mataifa kama Marekani aje ajaribu atabinywa kende mwaka mmoja tu anakimbia Ikulu au anapinduliwa.
Hilo jeshi lako alishaliweka mfukoni siku nyingi sana.
Wala usitegemee litamgeuka
 
SUBUTU, Marekani mwenyewe anagwaya maana hatuombi msaada kwake! na hilo la Jeshi sahau kabisa, majaribio yote yaliyofanywa wakati wa Nyerere yaliishia wapi? Unafikiri JPM ni mjinga kushindwa kulidhibiti jeshi mapema?
Ulivyo mjinga pengine hujui hata jaribio la kumpindua Nyerere lilikuja kuzimwa na askari kutoka kwa mabeberu(Uingereza) baada ya Nyerere kuwaomba msaada na pia tuliomba msaada kwa Nigeria na Ethiopia na wakaleta wanajeshi wao hapa nchini kuweka mambo sawa.

Waambieni huko mataga wawe wanawapa historia ya ukweli.
 
Inaonekana nchi hii Rais akiwa muislam.
Basi kutwa tunapatiwa waraka wa Uongozi Bora unaoheshimu katiba kutoka
Kwa Viongozi WA kanisa katoliki
Na Baraza la maaskofu.

Wenye kumbukumbu wote mnakumbuka jinsi hata tetesi zikitokea wakati wa Kikwete ..haraka Sana taasisi hizo zinatoa matamshi makali kukemea na hata kutishia hali ya amani kutoweka huko mbele iwapo
Katiba haitaheshimiwa.

Sasa leo Spika wa Bunge kazungumza bungeni kabisa kuwa mpango wa kubadili katiba tuwe na Rais wa maisha unakuja..

Hapa najiuliza na hili wenzetu mtalikalia kimyaa? Na hili Baraza la Maaskofu na kanisa katoliki ni sahihi kwenu?
Hivi ikitokea katiba ikabadilishwa na mtu.

Wenu Mungu akamchukua na akarithiwa na muislam ... mtaendelea kukaa kimyaa na urais wa maisha? Au nyinyi nyote mtaaamka na kuanza kudai haki za kiraia na demokrasia pana na kila aina ya haki mtazikumbuka?

Msisahau nyinyi mna mipango yenu na Mungu ana mipango yake..msije..geuka huko mbele
Hakuna MUISLAM anawèza kubali UPUMBAVU huo.

Nchi hii si ya WAKRISTO peke yao.
 
Screenshot 2020-06-10 at 16.59.00.png

Heri walao hii mashine imesema chochote
 
Unafiki ni mwingi sana utakuta wakati JK yupo wengi humu walikuwa wanafurahia na sasa upepo umegeuka hao hao wanawaponda maaskofu
Tuache unafiki na ifike mahali dini zisiingizwe kwenye siasa ila mpiganie maslahi ya Taifa kwa ujumla bila kujali wewe ni dini gani
 
Kusema kweli TEC ya sasa inastaajabisha Sana. Madhulumu kibao yanafanyika, hawakemei. Wamebaki wanasubiri vitu vichache ambavyo jiwe anafanya vizuri ili wasifu. Wamesahau wajibu wao ni pamoja na kuhubiri Imani inayotenda haki Kama anavyofundisha mama Kanisa. Nakumbuka enzi za jk, Wakati huo baba yangu akiwa M/kiti wa parokia, namna nyaraka na semina maalum za kuwahamasisha watu wasimchague JK zilivyokuwa zinafanyika kwa ustadi Mkubwa. Kumbe ilikuwa gelesha tuu. Watakatifu waliokufa wakitetea uhai Kama Fr. Romeo na Ignatius wa Loyola watakuwa wanaumia wakiliona Kanisa la Tanzania.
Mungu atunusuru.
 
Shida iko pande zote.

Rais Magufuli anayepigiwa Chapuo ili atawale milele anapaswa kutambua kuwa wanaopiga hizi kelele wanapiga ili kulinda maslahi yao na wala siyo kwa mapenzi ya dhati kwake..
 
Back
Top Bottom