Urais wa Maisha: Baraza la Maaskofu na Kadinali Pengo wapo?

Urais wa Maisha: Baraza la Maaskofu na Kadinali Pengo wapo?

Kwani ni rais wa wacatholic hoja zingine dhaifu kweli.. Mbona Masheikh wako kimya?
Ndo nashangaa kwanini waislamu wako kimya kama hawakubaliani na uongozi uliopo , huyu aliyeleta hoja ya dini analeta siasa za kuwatenganisha watu
 
Si jukumu lao pekee na kumbuka si uwalalamikie kuwa hawasemi hata wewe sema ili nao wawe influanced na wewe wakemee pia

Pia ni ngumu kama taasisi kuzungumzia allegations badala ya hoja shikizi
 
Kichwa chake kinatafunika na fikra za Nyerere.

Hakuna namna ya kutenganisha dini kutoka kwenye siasa.
Kwa uislamu ni siasa na siasa iko ndani ya uislamu.

Kwa nyakati hizi hiyo habari unaiona kama utani, ngoja hayo mawazo yachukue utendaji ndo utaelewa kama siasa na dini ni baba mmoja mama mmoja.
 
Pengo sio mtz wala kiongozi wa dini yule ndio maana hata Papa kamuondoa baada ya kupata taarifa kua maaskofu wote waliandika waraka lkn yeye peke yake kwa ulevi wake wa rushwa akawa upande wa watesi wetu awamu ya tano......

HUYU NDIO ASKOFU WA KWELI👇👇👇👇

ONYO KWA WABUNGE, SPIKA, NA RAIS MAGUFULI
Nimemsikia Mbunge mmoja akiongea Bungeni akitaka Bunge libadilishe Katiba ya Nchi ili kumfanya Rais Magufuli aendelee kutawala hata baada ya kumaliza kipindi chake cha kikatiba cha miaka 10. Kama hilo halitoshi, Spika Ndugai amesikika akimhakikishia Mbunge husika kuwa kazi hiyo ya kubadilisha kipengere cha Katiba kinachoweka ukomo wa Rais kuwa miaka 10 itafanywa na wao wote [Wabunge] katika Bunge lijalo. [Spika anaonekana kuwa na uhakika kuwa Rais Magufuli na wao wenyewe watachaguliwa tena katika Uchaguzi wa Mwaka huu].
Ninapenda niwalejeze Spika Ndugai, Wabunge, na Watanzania wote kwa ujumla kuhusu habari ya Mfalme Darius na Bunge lake katika Dola ya Uajemi (Persia) na Umedi (Mede) yapata miaka 2500 iliyopita.
Mfalme Darius aliunda Baraza (Bunge) lake lenye Wajumbe 120 aliowateua yeye wenyewe. Katika hali ya kutaka kumkomoa Danieli ambaye alionekana kuwa na uwezo mkubwa wa kiuongozi kuwazidi wao, Wabunge wenye nia ovu walianzisha mikakati ya siri ya kutaka kumnyamazisha Danieli. Mikakati yote iliposhindwa, waliamua kutunga sheria ambayo walijua kuwa itamfurahisha Mfalme Darius lakini huku ikiwa na lengo lililojificha la kumnyamazisha kabisa Danieli kwani walijua kuwa hatima ya sheria ile ilikuwa ni kifo cha Danieli. Walitunga sheria ya kutukuza mawazo ya Mfalme kwa kusifu na kuabudu mradi au sanamu aliyoitengeneza Mfalme. Walimshawishi Mfalme aitie muhuri au aisaini sheria ile. Wakapitisha Azimio la Ki-Bunge la kuzuia mtu ye yote au mamlaka ye yote kutangua sheria ile. Hata hivyo, Mungu hakuruhusu uovu ule na akaingilia kati. Wabunge wote waliopitisha Azimio lile waliuawa pamoja na wake zao na watoto wao lakini Danieli alipona na aliendelea kustawi zaidi. Kwa uelewa zaidi kuhusu habari hii someni Biblia Takatifu katika Kitabu cha Danieli 6:1-28.
Tunapenda kuwaonya na kuwatahadharisha Wabunge na watu wote wanaofanya mikakati ya kutaka kutunga Sheria mbalimbali zenye hila mtambuka ikiwemo kutaka kumfurahisha Rais aliyeko madarakani lakini lengo kuu lililojificha likiwa ni kulinda matakwa yao binafsi kwa njia ya kuwazuia au kuwanyamazisha watu wengine wanaoonekana kuwa ni tishio kwa nafasi zao na matakwa yao! Mungu anatoa onyo kali kwa watu na viongozi wa namna hiyo (Isaya 10:1-4).
Ushauri wangu kwa Rais Magufuli ni kuwa awe makini sana na watu ambao kila kukicha wanapenda kumsifia tu pasipo hata kumtahadharisha. Akiwafuata watu wa namna hiyo, basi ajue kuwa anaikaribisha hasira ya Mungu kwake mwenyewe na kizazi chake!
Ninamshukuru Mungu mwenye rehema nyingi kwa kunipa ujasiri wa kuyaandika haya (Ezekieli 33:1-20).
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani
 
Attachments

  • ASKOFU MWAMAKULA.jpg
    ASKOFU MWAMAKULA.jpg
    12.3 KB · Views: 13
Inaonekana nchi hii Rais akiwa muislam.
Basi kutwa tunapatiwa waraka wa Uongozi Bora unaoheshimu katiba kutoka
Kwa Viongozi WA kanisa katoliki
Na Baraza la maaskofu.

Wenye kumbukumbu wote mnakumbuka jinsi hata tetesi zikitokea wakati wa Kikwete ..haraka Sana taasisi hizo zinatoa matamshi makali kukemea na hata kutishia hali ya amani kutoweka huko mbele iwapo
Katiba haitaheshimiwa.

Sasa leo Spika wa Bunge kazungumza bungeni kabisa kuwa mpango wa kubadili katiba tuwe na Rais wa maisha unakuja..

Hapa najiuliza na hili wenzetu mtalikalia kimyaa? Na hili Baraza la Maaskofu na kanisa katoliki ni sahihi kwenu?
Hivi ikitokea katiba ikabadilishwa na mtu.

Wenu Mungu akamchukua na akarithiwa na muislam ... mtaendelea kukaa kimyaa na urais wa maisha? Au nyinyi nyote mtaaamka na kuanza kudai haki za kiraia na demokrasia pana na kila aina ya haki mtazikumbuka?

Msisahau nyinyi mna mipango yenu na Mungu ana mipango yake..msije..geuka huko mbele
Tupo pamoja nimeona upuuuuzi mkubwa wa spika karibu ningepasua laptop yangu leo. Mkristo mie na nasema hata kupewa awamu ya pili ni kwasababu tu ya ujinga wa watz wengi ila rais aliyepo hafai kabisa kuendelea. Ni masikitiko!
 
Mkuu
Kwa k
Inaonekana nchi hii Rais akiwa muislam.
Basi kutwa tunapatiwa waraka wa Uongozi Bora unaoheshimu katiba kutoka
Kwa Viongozi WA kanisa katoliki
Na Baraza la maaskofu.

Wenye kumbukumbu wote mnakumbuka jinsi hata tetesi zikitokea wakati wa Kikwete ..haraka Sana taasisi hizo zinatoa matamshi makali kukemea na hata kutishia hali ya amani kutoweka huko mbele iwapo
Katiba haitaheshimiwa.

Sasa leo Spika wa Bunge kazungumza bungeni kabisa kuwa mpango wa kubadili katiba tuwe na Rais wa maisha unakuja..

Hapa najiuliza na hili wenzetu mtalikalia kimyaa? Na hili Baraza la Maaskofu na kanisa katoliki ni sahihi kwenu?
Hivi ikitokea katiba ikabadilishwa na mtu.

Wenu Mungu akamchukua na akarithiwa na muislam ... mtaendelea kukaa kimyaa na urais wa maisha? Au nyinyi nyote mtaaamka na kuanza kudai haki za kiraia na demokrasia pana na kila aina ya haki mtazikumbuka?

Msisahau nyinyi mna mipango yenu na Mungu ana mipango yake..msije..geuka huko mbele
Mkuu,
Kwa kweli najaribu kutafakuri Nini hatima ya Jambo hili katka nchi ambayo hatukutarajia watu Kama maaskofu na mashekhe kukaa kimya au wanamuogopa mfalme ?
 
Inaonekana nchi hii Rais akiwa muislam.
Basi kutwa tunapatiwa waraka wa Uongozi Bora unaoheshimu katiba kutoka
Kwa Viongozi WA kanisa katoliki
Na Baraza la maaskofu.

Wenye kumbukumbu wote mnakumbuka jinsi hata tetesi zikitokea wakati wa Kikwete ..haraka Sana taasisi hizo zinatoa matamshi makali kukemea na hata kutishia hali ya amani kutoweka huko mbele iwapo
Katiba haitaheshimiwa.

Sasa leo Spika wa Bunge kazungumza bungeni kabisa kuwa mpango wa kubadili katiba tuwe na Rais wa maisha unakuja..

Hapa najiuliza na hili wenzetu mtalikalia kimyaa? Na hili Baraza la Maaskofu na kanisa katoliki ni sahihi kwenu?
Hivi ikitokea katiba ikabadilishwa na mtu.

Wenu Mungu akamchukua na akarithiwa na muislam ... mtaendelea kukaa kimyaa na urais wa maisha? Au nyinyi nyote mtaaamka na kuanza kudai haki za kiraia na demokrasia pana na kila aina ya haki mtazikumbuka?

Msisahau nyinyi mna mipango yenu na Mungu ana mipango yake..msije..geuka huko mbele
Nadhani hapa ni hoja ya maendeleo na Wala sio udini.hili hata likiwekwa kwenye katiba lazima liendane na moyo wa mhusika kuiletea nchi hii maendeleo.bila kujali dini yake
Nchi hii ktk historia mpaka Sasa imeongozwa na waislam pamoja na wakristo.Haijawahi kuibuka hoja ya urais wa maisha,kwa hiyo hapa issue sio ukristo au uislam.mimi binafsi Magu kwa maendeleo anayoyafanya hapa nchini hata angekuwa Hana dini ningeungana na wanaosema aendelee,sababu Ni moja tu,hao wenye dini zao mbona hawakufanikiwa kuonyesha ulimwengu kwamba Tanzania unaweza kusimama kwa miguu yake?tumepewa mpaka msaada wa net za mbu,huku Kodi zetu zikitumika kulipa mishahara hewa n.k
 
Hawapingi maendeleo wanapinga udikteta, dikteta Hana rafiki kesho zamu yako
 
Acheni uongo na dharau,usikoment tu ilimradi tu, Tec wana utaratibu wakutoa walaka kipindi cha kwarezima juu ya mambo ya kidin na mwenendo mzima nmna nchi ilivyo.Hiv karibuni kumbuka kuna padre aliambiwa wana shaka uraia wake baada ya kuikosoa serikali.
Bado kuna katibu wa tec pia aliwah kunyanganywa mpak hat kusafiria ati wana shaka na uraia wake baada walaka kuikosoa serikali.
Unayosema viongoz din hasa wakatolik kuwa wamekaa kimia hawasemi na sio kweli, huna kumbukumbu tu.
Usifanye watu maboya..

Kipindi cha JK maaskofu walikuwa wanasimamia kucha kabisa.
 
Hawapingi maendeleo wanapinga udikteta, dikteta Hana rafiki kesho zamu yako
Nadhani tungepiga kura ili tuone huo udikteta ni mkubwa kiasi gani.mwizi akipinga ujenzi wa kituo cha polisi kwenye mtaa wako,na wewe ukamuunga mkono mkafanikiwa kuzuia,Giza likiingia ukaibiwa utakuwa umechelewa Sana kujua lengo lake.
Watanzania tumeumizwa Sana na wapiga dili,na Sasa tumepata mtetezi tunajitokeza adharani kumuunga mkono.bila woga
 
Back
Top Bottom