Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 59,804
- 134,593
Wanabodi hili ni bandiko la 2015Inaonekana nchi hii Rais akiwa muislam.
Basi kutwa tunapatiwa waraka wa Uongozi Bora unaoheshimu katiba kutoka
Kwa Viongozi WA kanisa katoliki
Na Baraza la maaskofu.
Wenye kumbukumbu wote mnakumbuka jinsi hata tetesi zikitokea wakati wa Kikwete ..haraka Sana taasisi hizo zinatoa matamshi makali kukemea na hata kutishia hali ya amani kutoweka huko mbele iwapo
Katiba haitaheshimiwa.
Sasa leo Spika wa Bunge kazungumza bungeni kabisa kuwa mpango wa kubadili katiba tuwe na Rais wa maisha unakuja..
Hapa najiuliza na hili wenzetu mtalikalia kimyaa? Na hili Baraza la Maaskofu na kanisa katoliki ni sahihi kwenu?
Hivi ikitokea katiba ikabadilishwa na mtu.
Wenu Mungu akamchukua na akarithiwa na muislam ... mtaendelea kukaa kimyaa na urais wa maisha? Au nyinyi nyote mtaaamka na kuanza kudai haki za kiraia na demokrasia pana na kila aina ya haki mtazikumbuka?
Msisahau nyinyi mna mipango yenu na Mungu ana mipango yake..msije..geuka huko mbele
Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.4. Na hiyo 2025 tukimuona Magufuli bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili hiyo katiba yetu ili tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.
5. Kwani katiba ni nini?, si ni kipande tuu cha karatasi?!, ingekuwa katiba ni muhimu kihivyo kama ambavyo watu wanataka kutuaminisha humu, nini muhimu zaidi kwa taifa letu Tanzania, kati ya katiba ambayo ni kipande tuu cha karatasi na maamuzi ya rais Magufuli ambaye ni rais wa nchi, aliyechaguliwa na watu, katika uchaguzi huru na wa haki?.
6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, hivyo kama sisi Watanzania, katika umoja wetu, tukiamua tunamtaka Magufuli aendelee tuu idefinately, si tunaweza kuiweka tuu pembeni hiyo katiba, na tukaendelea na Magufuli wetu mpaka tutosheke naye?!.
7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana kuliko hata katiba na ndio maana anaweza hata kuikanyaga, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu, na kumwacha aendelee tuu kama Kagame, Museveni na Mugabe?.
8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Kama katiba inakanywa na hakuna kinachofanyika, Jee kuna ubaya kama tutaibadili katiba na Magufuli akapatiwa muda wa kutosha kabisa wa kuinyoosha nchi yetu kama Kagame anainyoosha Rwanda, , Museveni anavyoinyoosha Uganda na Mugabe anavyoinyoosha Zimbabwe?.
Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.
Paskali
No sio urais wa maisha bali ni urais wa kipindi cha kutosha angalau vipindi viwili vya miaka 10.
P