Urais wa Maisha: Baraza la Maaskofu na Kadinali Pengo wapo?

Wao Rais akiwa muislam mbona hawakai kimyaa?
 
Magufuli hana ubavu wa kujiongezea muda akitaka kuona nguvu ya jeshi(JWTZ) na mataifa kama Marekani aje ajaribu atabinywa kende mwaka mmoja tu anakimbia Ikulu au anapinduliwa.
Hilo jeshi lako alishaliweka mfukoni siku nyingi sana.
Wala usitegemee litamgeuka
 
SUBUTU, Marekani mwenyewe anagwaya maana hatuombi msaada kwake! na hilo la Jeshi sahau kabisa, majaribio yote yaliyofanywa wakati wa Nyerere yaliishia wapi? Unafikiri JPM ni mjinga kushindwa kulidhibiti jeshi mapema?
Ulivyo mjinga pengine hujui hata jaribio la kumpindua Nyerere lilikuja kuzimwa na askari kutoka kwa mabeberu(Uingereza) baada ya Nyerere kuwaomba msaada na pia tuliomba msaada kwa Nigeria na Ethiopia na wakaleta wanajeshi wao hapa nchini kuweka mambo sawa.

Waambieni huko mataga wawe wanawapa historia ya ukweli.
 
Hakuna MUISLAM anawèza kubali UPUMBAVU huo.

Nchi hii si ya WAKRISTO peke yao.
 

Heri walao hii mashine imesema chochote
 
Unafiki ni mwingi sana utakuta wakati JK yupo wengi humu walikuwa wanafurahia na sasa upepo umegeuka hao hao wanawaponda maaskofu
Tuache unafiki na ifike mahali dini zisiingizwe kwenye siasa ila mpiganie maslahi ya Taifa kwa ujumla bila kujali wewe ni dini gani
 
Kusema kweli TEC ya sasa inastaajabisha Sana. Madhulumu kibao yanafanyika, hawakemei. Wamebaki wanasubiri vitu vichache ambavyo jiwe anafanya vizuri ili wasifu. Wamesahau wajibu wao ni pamoja na kuhubiri Imani inayotenda haki Kama anavyofundisha mama Kanisa. Nakumbuka enzi za jk, Wakati huo baba yangu akiwa M/kiti wa parokia, namna nyaraka na semina maalum za kuwahamasisha watu wasimchague JK zilivyokuwa zinafanyika kwa ustadi Mkubwa. Kumbe ilikuwa gelesha tuu. Watakatifu waliokufa wakitetea uhai Kama Fr. Romeo na Ignatius wa Loyola watakuwa wanaumia wakiliona Kanisa la Tanzania.
Mungu atunusuru.
 
Shida iko pande zote.


Rais Magufuli anayepigiwa Chapuo ili atawale milele anapaswa kutambua kuwa wanaopiga hizi kelele wanapiga ili kulinda maslahi yao na wala siyo kwa mapenzi ya dhati kwake..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…