Urais wa Maisha: Baraza la Maaskofu na Kadinali Pengo wapo?

Wanabodi hili ni bandiko la 2015

Kwa Kasi hii ya Magufuli, kuna haja Kufanya Uchaguzi wa Rais 2020?
Wanabodi, kwanza angalieni tarehe ya bandiko hili, kisha angalia hoja No. 4, 5, 6, 7 na 8 za bandiko hili, kisha sikiliza kilichozungumzwa jana Bungeni Dodoma kuhusu hoja hii.

No sio urais wa maisha bali ni urais wa kipindi cha kutosha angalau vipindi viwili vya miaka 10.

P
 
Acheni uongo na dharau,usikoment tu ilimradi tu, Tec wana utaratibu wakutoa walaka kipindi cha kwarezima juu ya mambo ya kidin na mwenendo mzima nmna nchi ilivyo.Hiv karibuni kumbuka kuna padre aliambiwa wana shaka uraia wake baada ya kuikosoa serikali.
Bado kuna katibu wa tec pia aliwah kunyanganywa mpak hat kusafiria ati wana shaka na uraia wake baada walaka kuikosoa serikali.
Unayosema viongoz din hasa wakatolik kuwa wamekaa kimia hawasemi na sio kweli, huna kumbukumbu tu.
 
Wacha aongezewe tu,tusonge mbele kimaendeleo kama mwl alikaa miaka 25 na bado tulitamani aendelee leo tuna mtu anafuata nyendo zake japo si kwa ukamilifu,sidhani kama kuna shida,shida ya kubadilisha badilisha uongozi mnaweza jikuta mmepata kiongozi asiyefaa au akaharibu mazuri yaliyokuwa yanaendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani yale waliokuwa wakipigia kelele na nyaraka kila siku kipindi cha JK, kwani ndiyo hayo hayo yanayofanyika sasa na bwana MAGU?
 
Walitaka achaguliwe nani? Au Dovutwa?
 
Hoja ya kuwahusisha viongozi wa dini, na hasa Kanisa Katoliki, ni ya msingi.
Sababu ni kwamba kiongozi mwandamizi wa Kanisa Katoliki wakati huo, Kardinali Pengo, alijitutumua sana kukosoa serikali za marais Mwinyi na Kikwete, lakini akawa bubu kwa serikali za Mkapa na Magufuli. Na kwa serikali ya Magufuli ndio kabisaaa Pengo alifikia hatua ya kujitoa ufahamu kabisa, na kuwasifia hata wapambe wa Magufuli, mtu kama Makonda! Kwa nini wawakosoe marais Waislamu tu? Huo ni Udini!
 
Kwani yale waliokuwa wakipigia kelele na nyaraka kila siku kipindi cha JK, kwani ndiyo hayo hayo yanayofanyika sasa na bwana MAGU?
Kwahiyo katiba haivunjwi?Watu hawauwawi?
Haki haziminywi?Hakuna cha kupigia kelele?
 
Tunasubiri tamko kutoka TEC,huyu mtu anatuhatirishia Umoja na Amani ya Nchi yetu.
 
Twende mbele turudi nyuma pia.. Mbunge Kessy sio mkatoliki ni Muslims mwenzuni .. ndiye aliepiga kelele kama analia vile akisema chonde chonde Magufuli aongezewe mda atake asitake. Kwa mantiki hiyo kanisa katoliki na baraza la maaskofu mnawalaum bure tu .
 
Yaani, tunaenda kuukalia msumali wa moto. matakoni jipu, unyayoni jipu.
 
Wanafiki wamejifungia wanakula sacramenti tu na kushushia na mvinyo hamna kitu watasema hao almradi wanapata ujira wao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…