Salaam, Shalom!!
Tangu uhuru, wote walioutamani Urais, Urais uliwakimbia. Kwa kadri unavyozidi kuutamani Urais wa Nchi hii ambayo Nyerere alikuwa mwasisi wa mifumo ya uongozi na utawala, Kwa spidi hiyo hiyo ya kuutafuta, utateleza mikononi mwako usiamini kilichotokea.
1. Rais Mwinyi, hakuwahi kuutafuta Urais, Urais ulimtafuta.
2. Rais Mkapa hakujulikana, Wala hakuwahi kuutafuta Urais, Urais Ulimtafuta.
3. Rais KIKWETE hakutumia pesa kuusaka Urais, Urais ulimtafuta.
4. Kadhalika, Rais Magufuli pia hakuwahi kuota ndoto za Urais na kuzianika hadharani, Urais ulimtafuta Hadi Chato.
Hizi kelele za kuwa Marehemu Lowassa alisalitiwa na Rais KIKWETE ni unafiki tu, Urais hautafutwi Kwa pesa, na Urais haugaiwi kiurafiki Wala kindugu kwamba ukimaliza kula niachie nami zamu yangu!!
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA [emoji1241].
Amen