Urais wa Tanzania hautafutwi kwa nguvu ya pesa wala upendeleo

Ndo ujue Urais hautafutwi Kwa pesa au upendeleo,

Urais ukikutaka, utakutafuta uliko,

Ufalme ulipomtaka Daudi, ulimfuata porini ukamkuta anachunga Kondoo na mbuzi😀😀

Wanasiasa wa Nchi hii wajifunze somo hili Toka Kwa Rabbon
Uko sahihi,kuna watu wanafanya kila kitu kwa usahihi na juhudi lakini hawafanikiwi, lakini kuna watu wala hawako serious lakini mafanikio yanawafuata
 
Kwa upumbavu huu wa middle class wa kitanzania, ndio maana nchi bado sana,eti Urais umewafuata hao uliowataja wakati ukweli yaani naked truth,mtu mmoja alikua na uwezo wa kutafuta Rais wa nchi, soma hii eti Mauritius ndio nchi inayowekeza kwa wingi hapa nchini, nini kilimfanya Nyerere ambaye Alisha ng'atuka kwenye siasa kurudi na kutuletea rais aliyejiita ni Mr.clean wakati ni mmoja wa mafisadi wakubwa?
Unashida kwenye dishing,sio bure wewe.
 
Uko sahihi,kuna watu wanafanya kila kitu kwa usahihi na juhudi lakini hawafanikiwi, lakini kuna watu wala hawako serious lakini mafanikio yanawafuata
Ni Kweli kabisa,

Si wote wenye mbio washindao katika michezo ya riadha,

Wakati na Bahati huwapata wote,

Na Kila jambo Lina wakati wake.

(Mhubiri 9:11, mhubiri 12:1...)

Urais ni KITI anachokalia Mungu tangu asili, mwanadamu hukaa Kwa niaba ya Mungu, Si vyema mtu kukitafuta Kwa nguvu,pesa na bidii.

Tufanye KAZI Kwa bidii, Ili Mungu amridhie mmoja wa Mtanzania mwenzetu kukikalia sawasawa na SHERIA tulizojiwekea.
 
Salaam, Shalom!!

Tangu uhuru, wote walioutamani Urais, Urais uliwakimbia. Kwa kadri unavyozidi kuutamani Urais wa Nchi hii ambayo Nyerere alikuwa mwasisi wa mifumo ya uongozi na utawala, Kwa spidi hiyo hiyo ya kuutafuta, utateleza mikononi mwako usiamini kilichotokea.

1. Rais Mwinyi, hakuwahi kuutafuta Urais, Urais ulimtafuta.

2. Rais Mkapa hakujulikana, Wala hakuwahi kuutafuta Urais, Urais Ulimtafuta.

3. Rais KIKWETE hakutumia pesa kuusaka Urais, Urais ulimtafuta.

4. Kadhalika, Rais Magufuli pia hakuwahi kuota ndoto za Urais na kuzianika hadharani, Urais ulimtafuta Hadi Chato.

Hizi kelele za kuwa Marehemu Lowassa alisalitiwa na Rais KIKWETE ni unafiki tu, Urais hautafutwi Kwa pesa, na Urais haugaiwi kiurafiki Wala kindugu kwamba ukimaliza kula niachie nami zamu yangu!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA [emoji1241].

Amen
Hata Mama Samia, urais ulimtafuta akiwa zake huko Tanga kwenye majukumu yake ya kawaida! Kweli naamini sasa Urais wa Tanzania una siri kubwa ndani yake!!
 
Ni Kweli kabisa.

Pia Urais hauwekewi uzio usikutoroke utakapoamua kukuacha.
 
Salaam, Shalom!!

Tangu uhuru, wote walioutamani Urais, Urais uliwakimbia. Kwa kadri unavyozidi kuutamani Urais wa Nchi hii ambayo Nyerere alikuwa mwasisi wa mifumo ya uongozi na utawala, Kwa spidi hiyo hiyo ya kuutafuta, utateleza mikononi mwako usiamini kilichotokea.

1. Rais Mwinyi, hakuwahi kuutafuta Urais, Urais ulimtafuta.

2. Rais Mkapa hakujulikana, Wala hakuwahi kuutafuta Urais, Urais Ulimtafuta.

3. Rais KIKWETE hakutumia pesa kuusaka Urais, Urais ulimtafuta.

4. Kadhalika, Rais Magufuli pia hakuwahi kuota ndoto za Urais na kuzianika hadharani, Urais ulimtafuta Hadi Chato.

Hizi kelele za kuwa Marehemu Lowassa alisalitiwa na Rais KIKWETE ni unafiki tu, Urais hautafutwi Kwa pesa, na Urais haugaiwi kiurafiki Wala kindugu kwamba ukimaliza kula niachie nami zamu yangu!!

Wasaka Urais Kwa pesa, endeleeni kuutafuta Urais kama mtaupata!!

Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA [emoji1241].

Amen
Uko sawa
 
Hayo makelele yote yanayohusu kutengwa kwa Jk ,ndiyo majibu yenyewe
Huyo Mzee binafsi ktk hili la Lowassa anasingiziwa.

Urais Huwa una TABIA ya kuvaa utelezi na kuwatoroka wote wautafutao Kwa bidii.

Pale IKULU hakuna biashara yoyote Hadi watu wapigane vikumbo kuusaka Urais!!

Ujumbe huu uwafikie wote wanaoumezea mate Urais wa Tanzania!!
 
Mkuu Rabbon unamtetea huyo mzee.
 
Mkuu Rabbon unamtetea huyo mzee.
No,

Nasimamatu ktk mstari wa HAKI.

Mzee alitukosesha fursa muhimu kupata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi katika Awamu yake.

Anyway, hatutachoka Wala kusinzia hata jambo Hilo litimie juu ya nchi yetu nzuri niipendayo TANZANIA 🇹🇿
 
Ulipo tupo, wazee wa safari ya matumaini wakapiga hela halafu wanategemea mbeleko ya JK.

Yaani wamekula hela ya Mzee wakampa matumaini halafu wakamtegemea JK.
 
KAZI aliyoifanya Magu Nchi hii Kwa muda mfupi inatosha kuthibitisha kuwa kamati ilituletea mtu sahihi.
 
Back
Top Bottom