Urais wa Tanzania hautafutwi kwa nguvu ya pesa wala upendeleo

Urais wa Tanzania hautafutwi kwa nguvu ya pesa wala upendeleo

Sio kila anaetoa hela anahtaji return wewe. Nimekuambia kuna watu by nature wanapenda mawazo mapya so anaweza kukusaidia tu bila kutaka chochote kwako. Nina ndugu alisomeshwa bure na mmama mjane tena masikin wa huko Italy kwasababu tu alikuja kikanisa kujitolea akamsikiliza akamsaidia kufikia ndoto zake. Hiz akili za kimasikin hiz kwamba kila anaekusaidia anahtaji chochote mnazo waswahili na ni kwasababu hatuna exposure hatujui dunia ya nje inajiendeshaje.na ndio maana nikakuuliza ninani aliyeenda ikulu bila kuiba au ndugu zake kuiba. Ni upuuzi tu
Usijitoe ufahamu,

Kuchangiwa Nyerere nauli kwenda kudai Uhuru Si kuutafuta Urais Kwa pesa.

Kuusaka Urais Kwa pesa ni kutumia pesa kutengeneza vikundi Nchi nzima Ili kupata uungwaji mkono kuukwaa Urais.
 
Ndo ujue pia Urais hautafutwi Kwa pesa Wala upendeleo!!
Kikwete aliingia ukumbini akijua ni Lowasa kumbe wenzake wamebadili na kuwa Magufuli.
Mrema alimshinda Mkapa ambaye wakati huo alikuwa hajui siasa, mwalimu akaamuru Mkapa apewe nchi.
 
Alimsaliti 100%.Akataka Membe shemejie sijui nduguye awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzia 2015 hadi 2025.
Tukisema kuwa KIKWETE alimsaliti Membe Kwa kushindwa kuhakikisha anakuwa Rais Kwa rungu la uenyekiti, ni Kweli au Si Kweli?
 
Usijitoe ufahamu,

Kuchangiwa Nyerere nauli kwenda kudai Uhuru Si kuutafuta Urais Kwa pesa.

Kuusaka Urais Kwa pesa ni kutumia pesa kutengeneza vikundi Nchi nzima Ili kupata uungwaji mkono kuukwaa Urais.
Ukiwa na pesa Nyingi unakuwa na mawazo makubwa ikiwemo kuweka Viongozi madarakani na kama Taifa limejaa Mapimbi unakaa Mwenyewe madarakani

Ndio unawaona Trump, Putin, Kiduku, Ruto, Ramaphosa, Tshekedi nk....nk hao wote wananukia Fedha

Bongo mnaweka maskini halafu wakikwapua mnaanza kulialia

Ikulu siyo Kanisani au Msikitini 🐼
 
Nyerere alitumia vikundi nchi nzima sema we hujui. na waliokuwa wanamuwezesha ni akina rupia mbowe na wazee hawa wa kkoo. Kama hujui kaa kimya chief. Kila alikoenda watu walijitolea chochote wakiamin mawazo yake. Sema kwasababu kile walichokuwa wanatoa by then kwasasa we unaiona ni kidogo. Watu walijitolea nyumba zao kuweka vikao vya mikakati na kuchangishana hela za kampein. We unafikiri Nyerere na hela zake za ualimu angeweza kufanya kampein nchi nzima acha uzuzu wewe.
 
Ukiwa na pesa Nyingi unakuwa na mawazo makubwa ikiwemo kuweka Viongozi madarakani na kama Taifa limejaa Mapimbi unakaa Mwenyewe madarakani

Ndio unawaona Trump, Putin, Kiduku, Ruto, Ramaphosa, Tshekedi nk....nk hao wote wananukia Fedha

Bongo mnaweka maskini halafu wakikwapua mnaanza kulialia

Ikulu siyo Kanisani au Msikitini 🐼
IKULU ni Mahali Patakatifu.

Trump, Tshekedi, Ruto Si Watanzania wale. Jikite kwenye mada, historia inasemaje kuhusu wasaka Urais Kwa pesa.
 
Huyo Mzee binafsi ktk hili la Lowassa anasingiziwa.

Urais Huwa una TABIA ya kuvaa utelezi na kuwatoroka wote wautafutao Kwa bidii.

Pale IKULU hakuna biashara yoyote Hadi watu wapigane vikumbo kuusaka Urais!!

Ujumbe huu uwafikie wote wanaoumezea mate Urais wa Tanzania!!
Lakini Kikwete Urais aliotafuta kwa namna yoyote mpaka akaupata.
 
Lakini Kikwete Urais aliotafuta kwa namna yoyote mpaka akaupata.
Si Kweli,

Urais ulimtafuta kabla.

Lowwassa alikuwa na pesa za kutosha, na watu husema pesa ndo Kila kitu,

Iweje Lowassa asalimu Kwa KIKWETE asiye na pesa?

IPO mifumo isiyoonekana ikikukataa imekukataa!!
 
Tukisema kuwa KIKWETE alimsaliti Membe Kwa kushindwa kuhakikisha anakuwa Rais Kwa rungu la uenyekiti, ni Kweli au Si Kweli?
Kikwete alitaka Membe awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ila alidhibitiwa vikali na Mzee Mwinyi pamoja na Mzee Mkapa na ndipo alipoteuliwa Magufuri bila ridhaa ya Kikwete.Yale yale yaliyotokea 1995 wakati Mwinyi alipotaka kati ya Salmin,Lowasa na Kikwete mmoja awe Rais wa Jamhuri ya Muungano lakini Nyerere akakataa na kumleta Mkapa kutoka sehemu isiyojulikana.
 
Si Kweli,

Urais ulimtafuta kabla.

Lowwassa alikuwa na pesa za kutosha, na watu husema pesa ndo Kila kitu,

Iweje Lowassa asalimu Kwa KIKWETE asiye na pesa?

IPO mifumo isiyoonekana ikikukataa imekukataa!!
Mkuu wewe ni CCM damu damu kwa utetezi huo.Kauli ya Nyerere kusema,"Ikulu ni mahali patakatifu" ni kwa sababu ya Kikwete.Kikwete kama 2005 angekuwapo Nyerere asingepata Urais nakwambia.Kikwete ndiyo mcheza rafu namba moja Tanzania,anakumaliza huku akikuchekea.
 
Kikwete alitaka Membe awe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ila alidhibitiwa vikali na Mzee Mwinyi pamoja na Mzee Mkapa na ndipo alipoteuliwa Magufuri bila ridhaa ya Kikwete.Yale yale yaliyotokea 1995 wakati Mwinyi alipotaka kati ya Salmin,Lowasa na Kikwete mmoja awe Rais wa Jamhuri ya Muungano lakini Nyerere akakataa na kumleta Mkapa kutoka sehemu isiyojulikana.
Kwahiyo unakubali kuwa Rais anayemaliza muda wake pamoja na Rungu la uenyekiti Bado Hana maamuzi ya mwisho juu ya nani awe Rais,

Ndomana umetamka " Alidhibitiwa".

Sasa Usaliti wa JK unatoka wapi?

Tusimuonee JK katika hili.

UKWELI ni vizuri usemwe.
 
Usaliti wa Kikwete ni kuengue majina yote mazuri ya wagombea na kumwacha Membe na wanawake wawili ili Membe apite kirahisi kwa mujibu wa mila za Watanzania.
 
Back
Top Bottom