Soma thread: Live Kutoka Mbinguni- Rabbon.Ulifika lini Mbinguni ukayakuta hayo unayoyasema? Kwanini manabii + mitume wa nyakati hizi wanafanya lobbying kupata waumini?
Watu wako radhi kumwaga damu za wenzao kuupata Urais, wewe unaongea rushwa ya pesa ambacho ni kitu cha kawaida kwenye chaguzi zetu. Lazima wewe utakuwa unaishi Burundi kama unashidwa kuyaona haya. Kikwete pesa ya EPA ilifanya kazi ili aupate Rais.Salaam, Shalom!!
Tangu uhuru, wote walioutamani Urais, Urais uliwakimbia. Kwa kadri unavyozidi kuutamani Urais wa Nchi hii ambayo Nyerere alikuwa mwasisi wa mifumo ya uongozi na utawala, Kwa spidi hiyo hiyo ya kuutafuta, utateleza mikononi mwako usiamini kilichotokea.
1. Rais Mwinyi, hakuwahi kuutafuta Urais, Urais ulimtafuta.
2. Rais Mkapa hakujulikana, Wala hakuwahi kuutafuta Urais, Urais Ulimtafuta.
3. Rais KIKWETE hakutumia pesa kuusaka Urais, Urais ulimtafuta.
4. Kadhalika, Rais Magufuli pia hakuwahi kuota ndoto za Urais na kuzianika hadharani, Urais ulimtafuta Hadi Chato.
Hizi kelele za kuwa Marehemu Lowassa alisalitiwa na Rais KIKWETE ni unafiki tu, Urais hautafutwi Kwa pesa, na Urais haugaiwi kiurafiki Wala kindugu kwamba ukimaliza kula niachie nami zamu yangu!!
Wasaka Urais Kwa pesa, endeleeni kuutafuta Urais kama mtaupata!!
Mungu ibariki Nchi yangu nzuri niipendayo TANZANIA [emoji1241].
Amen
😂😂😂Bado sijatoboa mkuu,najitafuta
Kumbe sasa tuseme,Watu wako radhi kumwaga damu za wenzao kuupata Urais, wewe unaongea rushwa ya pesa ambacho ni kitu cha kawaida kwenye chaguzi zetu. Lazima wewe utakuwa unaishi Burundi kama unashidwa kuyaona haya. Kikwete pesa ya EPA ilifanya kazi ili aupate Rais.
Kwa hiyo shida ilikuwa kumuongelea Lowassa. Ni hivi hiyo nafasi ilikuwa ikikodolewa macho na makundi mengine baada ya kipindi cha pili cha jk, na Edo alikuwa tishio kwa mambo mawili, kukubalika kwake na pili kasi ya utendaji. Wakaanga sumu, wazee wa fitina, walisoma hilo gap ikawalazimu wamfitinishe mapema kwa mzee baba kwamba hasipoangalia jamaa atachukuwa nafsi kabla ya yeye kumaliza muhula wa pili, na mzee mkubwa alishawishika kwa huo ushahuri akaona hisiwe taabu, wakaamua kumtafutia ajali.Kumbe sasa tuseme,
Lowassa hakuwa na Pesa, na ndio sababu za kuukosa Urais!!
Nitakuwa sawa kusema hivyo?
Kwahiyo ni sawa kusema pesa pekee haitoshi kukupa Urais katika Nchi ya Tanzania.Kwa hiyo shida ilikuwa kumuongelea Lowassa. Ni hivi hiyo nafasi ilikuwa ikikodolewa macho na makundi mengine baada ya kipindi cha pili cha jk, na Edo alikuwa tishio kwa mambo mawili, kukubalika kwake na pili kasi ya utendaji. Wakaanga sumu, wazee wa fitina, walisoma hilo gap ikawalazimu wamfitinishe mapema kwa mzee baba kwamba hasipoangalia jamaa atachukuwa nafsi kabla ya yeye kumaliza muhula wa pili, na mzee mkubwa alishawishika kwa huo ushahuri akaona hisiwe taabu, wakaamua kumtafutia ajali.
🤣🤣🤣Acha ukorofi,
Urais haugaiwi kama nyama mnazikula hapo msibani!!
Kwamba, nikatie Ile yenye mafuta iliyonona😀
Na dharau zake Sasa hivi Kawa kipofu.Umenikumbisha maneno ya Dr. Salmin Amour Juma Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mstaafu, wakati akizungumzia Urais wa Zanzibar, alisema Urais si Halua kwamba kila mtu alambe.
Punguza ubishi. Kikwete alimuengua Lowassa kwaajili ya Membe.Ndo nakwambia,
Pesa za Lowassa hazikumpa KIKWETE Urais, ni zaidi ya hapo.
KIKWETE hawezi kulaumiwa kushindwa kumkabidhi KITI Lowassa sababu Yeye hakuwa final say juu ya nani arithi KITI chake.
Acheni hizo basi,
Yaani wewe JokaKuu unaamini Kweli kuwa KIKWETE angeweza kuamua Membe awe Rais, akawa?
Kwanini asimuengue na Magu Ili Membe apite kiulaini?Punguza ubishi. Kikwete alimuengua Lowassa kwaajili ya Membe.
Fact...Tatizo hamna exposure mnafikiri hela ziko hapa tu. Dunia nzima kuna watu wanawasaidia watu kufikia malengo ya ndoto zao. Hata Nyerere kuna vizee viliuza mpaka baiskeli huko uswahilin. Ili ashike madaraka kila mtu ana watu wanamkubali mawazo yake so wanawekeza kwenye ndoto zake. So kwasasa sisi ni mapimbi bado kila alichosema Nyerere tumegeuza ni msahafu. Wakat hata yeye kaingizwa na watu hakuna Rais popote anaweza kuingia ikulu bila watu pale. Biashara iliyopo ni kuweka mawazo mapya juu katika kulisogeza gurudum la maendeleo nothing more. Hatuwez kuish kwa kuogopa hisia za Marehemu na kumruhusu aishi maisha yake tena aje aishi na yetu. Wakat mtu huyo huyo wakat anatoka ikulu alituambia mwenyewe siasa zake zimeshindwa. Amken vinginevyo wagen watakuja kuchukua kila kitu.
Mtoa mada amesahau hili.2005 ilikuwaje?, Wana mtandao walishinda Kwa kishindo
.Vipi JM Junior 2025 huenda akawa wa kwanza kuupata kwa kuwa natamaa tangu 2015 na hatimaye atapewa na BT, maana Godfather wa siasa ndani ya kampuni ni BT kwa sasa.
we nae unatuvuruga sasa!Wewe ni mwanademokrasia,
Usibebwe na hizi dhana za Urais wa kurithishana.
Wananchi ndiyo asili ya uongozi wa juu wa Nchi.
Wapo ambao Huwa wanafanya tafiti Kwa maslah ya nchi.
Ndo hao waliona Magu anafaa kutuvusha.
Hizo zingine ni story tu.
KIKWETE hakumsaliti Lowassa!!
Kweli kabisa, mfano, Malecela aliutanani sana lakini ukamteleza!!Kuna mawaziri wakuu wanne waliutaka sana urais lakini wote waliangukia pua..