Mi napenda sana anklet chains,kuliko hata chain ya shingoni.Kuna zile za kihindi zinakuwa nene halafu kama zina vikengele vidogo vidogo ukitembea vinalia halafu kikiwa cha silver kinakuwa pure silver, gold pure gold.
Kuhusu eti sijui ukivaa unatuma sijui ujumbe gani ni Uongo na ni maneno mbofumbofu kama alivyoimba marehemu Mr Ebbo.
Hivi hawa waume za watu na wake za watu wanaopishana kutwa kwenye nyumba za kulala wageni wamevaa vikuku?
Hao wanaoingiliana kinyume na maumbile wataacha kwa vile hawana vikuku?
Mimi ninavyojua haya mambo watu huwa wanafanya na huwa hakuna ambaye anataka ajulikane kama anafanya tena wapo mpaka wanandoa ukiwaona huwezi kuwadhania na wala hawajui vikuku ni nini kawaulize washauri wa ndoa makanisani na misikitini usikie.Wengine na kusali wanasali kabisa lakini ndoa imeingia Usodoma.
Kwa hiyo hakuna cha vikuku wala vibata ingekuwa hivyo wanawake wa kimasai sijui wangekuwaje.