Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

Urembo wa vikuku, vishaufu na cheni (shanga) kiunoni kwa wadada

kuva vikukuu inatafsiri tofauti kwa jamii na tamaduni tofauti,zote njema na mbaya ila kama mtu unataka kwenda na wakati vaa lakin kumbuka yanaweza kukuta kama hawa wadada maana watu wanauelewa tofauti fanya uchunguzi wa kina ujue chimbuko la huo urembo.mimi najua moja juu ya pete, kwa watu wa ulaya mashariki mwanamke akivaa pete kwenye kidole gumba maana yake ni msagaji(lesbian),lakin kwa watu wengine inaweza isiwe hivyo.

Tuwe makini na mapambo tunayovaa.
 
Leo nimekutana na jambo ambalo sikulitegea kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu, Central sekondari kukatikiwa na shanga lundo kubwa akiwa kwenye daladala akienda shule asubuhi!

Hii ilitokea baada ya gari kujaa kupita kiasi na huyo mtoto alisimama katika harakati za kupishana ili wengiine washuke na kupanda, watu wakaona shanga zinamwagika kutoka kiunoni mwa huyo mtoto, japo yeye hakuonyesha kushituka sana!

Sasa wanajamii tunaelekea wapi? Form three kwenda na mashanga shuleni, huyu mtoto anatafuta nini lakini? Akina mama tujenge tabia ya kuongea na watoto wetu!
 
Wengine ni utamaduni wa kwao anakuwa nazo hizo shanga so no big deal , au sababu za urembo kujifurahisha binafsi
 
Kuna tatizo? Mbona ni mapambo ya kawaida ya mtoto wa kike?

Ungekutana na dume lenye shanga kunako kiuno ndo ingekuwa jambo la kushangaza kwa baadhi ya makabila.
 
Acha ujima ndugu...shanga pia kama vitu vinginevyo labda ni pambo kwa baadhi ya watu kama zilivyo hereni na pete....This is a NON ISSUE!
 
Leo nimekutana na jambo ambalo sikulitegea kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu, Central sekondari kukatikiwa na shanga lundo kubwa akiwa kwenye daladala akienda shule asubuhi! Hii ilitokea baada ya gari kujaa kupita kiasi na huyo mtoto alisimama katika harakati za kupishana ili wengingine washuke na kupanda, watu wakaona shanga zinamwagika kutoka kiunoni mwa huyo mtoto, japo yeye hakuonyesha kushituka sana! Sasa wanajamii tunaelekea wapi? Form three kwenda na mashanga shuleni, huyu mtoto anatafuta nini lakini? Akina mama tujenge tabia ya kuongea na watoto wetu!!!!!!!!!!!!!!!!
Hivi angedondosha kondomu si ungejiua weye...?? SHanga si kitu cha kushangaza katika jamii ya kitanzania.
 
Bahati mbaya tu...huyo wa form three mbona mkubwa kabisa si atakuwa amashabalehe na pengine kashafundwa so hakuna tatizo hapo.
 
Mimi mlinzi wangu Mmasai mwanaume ana vikuku double mguuni.......no big deal ni mila tu wala haihusiani na ngono

6434593741_40222f65bc_z.jpg
 
ni watu wachache sana wanaoishi mjini wanaofata mila hvy yawezekana alivaa kimila au alivaa kama kiburudisho.
 
Leo nimekutana na jambo ambalo sikulitegea kwa mwanafunzi wa kidato cha tatu, Central sekondari kukatikiwa na shanga lundo kubwa akiwa kwenye daladala akienda shule asubuhi! Hii ilitokea baada ya gari kujaa kupita kiasi na huyo mtoto alisimama katika harakati za kupishana ili wengingine washuke na kupanda, watu wakaona shanga zinamwagika kutoka kiunoni mwa huyo mtoto, japo yeye hakuonyesha kushituka sana! Sasa wanajamii tunaelekea wapi? Form three kwenda na mashanga shuleni, huyu mtoto anatafuta nini lakini? Akina mama tujenge tabia ya kuongea na watoto wetu!!!!!!!!!!!!!!!!

hii habari nawasiwasi nayo ni yakutungwa tuu, kama sio kufikirika na tena nawasiwasi imejaa uongo kidogo ndani yake,,,ANYWAI UMEJUAJE KAMA NI MWANAFUNZI WA FORM THREE?? MLIMUHOJI ALIWAAMBIA FORM THREE au umekadiria.
 
Shanga angevaa tu nyumbani kama ambavyo hawaruhusiwi kujipamba sana wakienda shuleni, ishu sio kuvaa shanga,ishu ni kwenda nazo shuleni....
 
shanga angevaa tu nyumbani
kama ambavyo hawaruhusiwi kujipamba sana wakienda shuleni...
ishu sio kuvaa shanga,ishu ni kwenda nazo shuleni....

Boss kwani asipojifunua nani atajua kama kavaa au la?

Mimi sioni tatizo kama hazionekani kwa nje, ila kama mtu ananing'iniza kila mtu aone hapo sio sawa.
 
Kuna jirani yangu amemvisha shanga mwanae ana umri kama wa miaka miwili na nusu leo nitaenda kumwambia asimzoeshe mwae shanga nilikuwa sijui kama shanga zina madhara!
 
Back
Top Bottom