kama umetumia dawa kama unavyosema bila mafanikio kaombe ufanyiwe urine culture ni test inayofanywa ili kubaini bacteria wanao sababisha UTI, hapo wanachukua mkojo wanauweka kwenye mazingira yanayoruhusu wadudu kukua, kama wadudu wakionekana/kukua kidogo basi hapo ni negative yaana hakuna infection, kama wadudu wakikua/kuonekana wengi ni positive manake kuna infection,ndipo wanaangalia ni aina gani ya wadudu walioonekana/kukua kwa darubini au vipimo vingine wakishajua hao wadudu ni aina gani tayari ni rahisi kujua dawa inayotibu/kuua wadudu hao,ukitumia dawa hiyo basi utapona kabisa na ugonjwa utatoweka kama walivyotoweka nzige vinginevyo upate maambukizo mapya.