Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 11,550
- 40,697
Mimi binafsi sipendi vita, na katika vita vya Ukraine sitaki kushabikia upande wowote kuhusu mauaji, japokuwa siungi mkono kabisa uvamizi wa kijeshi wa Russia katika nchi ya Ukraine kwa kuwa ilitosha mgogoro huu kumalizwa kidiplomasia.
Nilihisi na hata kutamani kuona Urusi ikimaliza tukio la kuivamia Ukraine ndani ya siku tatu tu ili kuepusha mauaji endelevu ambayo yangetokana na muendelezo wa kupigana vita kwa muda mrefu. Lakini hali imekuwa tofauti sana, mpaka leo hii, takribani mwezi mmoja tangu kuanza vita vya Ukraine hali bado tete huku Russia ikishindwa kumaliza shughuli za uvamizi kwa wakati.
Ukiachilia mashambulizi kutoka angani ambayo kutwa na usiku yamekuwa yakifanywa na Russia, tena yakilenga makazi ya watu, shule, hospitali, taasisi za uzalishaji nishati na maeneo mengine ya umma, hakuna kipya, kikubwa na cha zaidi ambacho Russia inaelekea kukifanya kupitia ardhini. Nguvu ya kupigana vita vya ardhini ni kama ndogo au inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine. Sehemu ya askari wa Russia waliofanikiwa kuingia na kukaa katika miji ya Ukraine ni kama wametelekezwa na Russia kiasi cha kukosa chakula au kuzingirwa upya na kisha kuangamizwa na askari wa Ukraine
Nawaza tu, mara ghafla anga la Ukraine na mataifa jirani yanayozunguka Ukraine likifungwa na kuzuiwa kwa Russia kukaribia ili kuishambulia Ukraine, nini kitafuata?