Urusi huenda imebakia na nguvu ya mashambulizi kutoka angani tu, ardhini pumzi imekata?

Urusi huenda imebakia na nguvu ya mashambulizi kutoka angani tu, ardhini pumzi imekata?

Mimi binafsi sipendi vita, na katika vita vya Ukraine sitaki kushabikia upande wowote kuhusu mauaji, japokuwa siungi mkono kabisa uvamizi wa kijeshi wa Russia katika nchi ya Ukraine kwa kuwa ilitosha mgogoro huu kumalizwa kidiplomasia.

Nilihisi na hata kutamani kuona Urusi ikimaliza tukio la kuivamia Ukraine ndani ya siku tatu tu ili kuepusha mauaji endelevu ambayo yangetokana na muendelezo wa kupigana vita kwa muda mrefu. Lakini hali imekuwa tofauti sana, mpaka leo hii, takribani mwezi mmoja tangu kuanza vita vya Ukraine hali bado tete huku Russia ikishindwa kumaliza shughuli za uvamizi kwa wakati.

Ukiachilia mashambulizi kutoka angani ambayo kutwa na usiku yamekuwa yakifanywa na Russia, tena yakilenga makazi ya watu, shule, hospitali, taasisi za uzalishaji nishati na maeneo mengine ya umma, hakuna kipya, kikubwa na cha zaidi ambacho Russia inaelekea kukifanya kupitia ardhini. Nguvu ya kupigana vita vya ardhini ni kama ndogo au inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine. Sehemu ya askari wa Russia waliofanikiwa kuingia na kukaa katika miji ya Ukraine ni kama wametelekezwa na Russia kiasi cha kukosa chakula au kuzingirwa upya na kisha kuangamizwa na askari wa Ukraine

Nawaza tu, mara ghafla anga la Ukraine na mataifa jirani yanayozunguka Ukraine likifungwa na kuzuiwa kwa Russia kukaribia ili kuishambulia Ukraine, nini kitafuata?
urusi imesema sio vita ni operation ya kijeshi
 
Utaambiwa ana mabomu ya nyuklia ameyaficha 😊😊😄😄, sjui wengine wana mabomu ya maji..teh teh teh ...
 
Asubuh ya leo watu wamesarenda ukraine inatumia raia kama ngao ndo maana raio wanalazimishwa wasikimbia. Urusi sio marekani marekani huwa inapiga bila kujari raia ama laa
img_9_1648321899688.jpg
img_2_1648321824202.jpg
img_7_1648321884740.jpg
img_1_1648442056867.jpg
unafikir wanajeshi wa urusi wamezikamataje hizo ant tank sema hii vita ina progagnda nyingi.
 
Ardhini wameuwawa wengi mno; mpaka sasa hivi wanafikia Takribn 15,000 ambao ni karibu divison mbili ukijumuisha na majenerali saba pamoja na makanari wapato 20; jeshi gani hilo. Jamaa hawajui vita ya ardhini kabisa, walikuwa wanaendesha vifaru barabarani kama wako mitaanbii vikawa vinabondwa kama vibuyu.

Hata angani pia hawapeleki ndege na helicopter kwani nazo zimeangushwa kama kasuku. Wanachotumia sasa hivi ni makombora ya mbali tu, wanayarusha kutokea kwenye manowari huko Black Sea.
Warus wanachukuliaga vita poah sana yan walivyokua wanaingia kwa msururu ,Ukraine utafikir msafara wa harus ,hawana protection wanajiendea kama mazombi,kuna mji huko karibu na kyv waliuteka ,wasinyo na akili wamejikusanya sehemu kama wanachek mpira ,aisee wamefanyiwa counter attack moja wamejeuka majivu,walionusurika nadhan hawatarud urusi
 
Siyo kweli, warusi wanajua kurusha makombora na kubomoa majumba tu, siyo kupigana vita. Wanavyofanya sasa hivi Ukraine ndivyo walivyofanya Aleppo Syria na pia walifanya hivyo Grozny Chechnya. Siku chache zijazo Ukraine itapata Patriot Air Defense System uone kama Urusi itaweza vita tena.
Msituchagulie pakuwapapasa hao UKRAINE
VIVA PUT IN
 
Urusi wapo vizuri tuu, shida ni Ukraini wanajeshi kujichanganya na Raia, inaleta shida kwa Urusi kufanya upembuzi yakinifu kwa vita ya aridhini. Ndio maana Urusi ameona isiwe tabu ngoja atokee angani sasa.
Sasa uko angani wanawezaje kufanya upembuzi wa raia?Kati ya angani na aridhini n wapi ilikuwa rahisi kufanya huo upembuzi,uongo mwingine muwe mnajipanga kwanza.
 
Hivi unaujua ukubwa wa eneo la Ukraine mpaka ufikiri operesheni ingeisha ndani ya siku tatu?
Pia ujue kuwa hii siyo vita halisi kama USA na Iraq, hii ni operations maalumu ambayo ililenga kuondoa nguvu za kijeshi za Ukraine ambazo marekeni walikuwa wamewajengea kwa lengo la kuweka makombora ya kuilenga Urusi. Wakati Russia wanailalamikia Marekani na kutaka security assurance lengo hasa lilikuwa kutaka marekani aondoe maabara za biological weapons na aache kusuply makombora kwa Ukraine. Karibu 80% ya nguvu za kijeshi ya Ukraine imeteketezwa!
Uteketeze 80% ya nguvu za kijeshi halafu ushindwe kumiliki hata kijiji? Hizi propaganda za kijamaa ni kiboko.
 
Kwanini operesheni imechukua muda.?
Ninavyokwambia ndo kwanza jamaa wanajipanga kwenda huko.
Hii wiki yapili sasa washafika.
Midege yoote mikubwa ya Mrusi ni kubeba mizigo.
Supersonic unazosema hizo kabisaa zinaangushwa mapema tu.
Haziruhusiwi kuruka hata mail moja.
Kaa utulie hapo.
Mrusi kamaliza ila hawa ndio wanaanza.
Ndivyo urusi wamekuambia wamemaliza? Mbona kichekesho hiki
 
Mimi binafsi sipendi vita, na katika vita vya Ukraine sitaki kushabikia upande wowote kuhusu mauaji, japokuwa siungi mkono kabisa uvamizi wa kijeshi wa Russia katika nchi ya Ukraine kwa kuwa ilitosha mgogoro huu kumalizwa kidiplomasia.

Nilihisi na hata kutamani kuona Urusi ikimaliza tukio la kuivamia Ukraine ndani ya siku tatu tu ili kuepusha mauaji endelevu ambayo yangetokana na muendelezo wa kupigana vita kwa muda mrefu. Lakini hali imekuwa tofauti sana, mpaka leo hii, takribani mwezi mmoja tangu kuanza vita vya Ukraine hali bado tete huku Russia ikishindwa kumaliza shughuli za uvamizi kwa wakati.

Ukiachilia mashambulizi kutoka angani ambayo kutwa na usiku yamekuwa yakifanywa na Russia, tena yakilenga makazi ya watu, shule, hospitali, taasisi za uzalishaji nishati na maeneo mengine ya umma, hakuna kipya, kikubwa na cha zaidi ambacho Russia inaelekea kukifanya kupitia ardhini. Nguvu ya kupigana vita vya ardhini ni kama ndogo au inakumbana na upinzani mkali kutoka kwa wanajeshi wa Ukraine. Sehemu ya askari wa Russia waliofanikiwa kuingia na kukaa katika miji ya Ukraine ni kama wametelekezwa na Russia kiasi cha kukosa chakula au kuzingirwa upya na kisha kuangamizwa na askari wa Ukraine

Nawaza tu, mara ghafla anga la Ukraine na mataifa jirani yanayozunguka Ukraine likifungwa na kuzuiwa kwa Russia kukaribia ili kuishambulia Ukraine, nini kitafuata?
Biden ameongea kauli moja iliyotafsiriwa kama ni kuruhusu Putin ashughulikiwe. Ni mjeuri huyu mrusi anayependa kuona Soviet Union ya wakati ule ikiwa inarudi miaka ya sasa lakini Wamarekani wameshaitawala sana dunia kwa sasa.

Ukishanunua simu ya kisasa umekubali kutawaliwa na mmarekani, huo ni ushawishi ambao Russia hana kwa sasa. Wanamzunguka Putin na asipokuwa mwangalifu watamfanya kitu mbaya.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji23]
 
Hivi unaujua ukubwa wa eneo la Ukraine mpaka ufikiri operesheni ingeisha ndani ya siku tatu?
Pia ujue kuwa hii siyo vita halisi kama USA na Iraq, hii ni operations maalumu ambayo ililenga kuondoa nguvu za kijeshi za Ukraine ambazo marekeni walikuwa wamewajengea kwa lengo la kuweka makombora ya kuilenga Urusi. Wakati Russia wanailalamikia Marekani na kutaka security assurance lengo hasa lilikuwa kutaka marekani aondoe maabara za biological weapons na aache kusuply makombora kwa Ukraine. Karibu 80% ya nguvu za kijeshi ya Ukraine imeteketezwa!
Unajiongopea mkuu... Russia anachezea kichapo Kila kukicha... Russia amebakiza kurusha makombora Tena ambayo hayana dira Wala muelekeo..
 
Watwange Ukraine siku kadhaa kwani mnaongea kwa kutumia akili zipi [emoji848]

Inamaana nguvu za kijeshi za Ukraine na hata kilometers za miraba kwa eneo ni sawa na Iraq [emoji848]

Na hiyo misaada ya silaha za kivita na wanajeshi toka Canada [emoji848]

Kufanya kwenu kazi NGOs kusiwaondolee akili za kudadavua ukweli halisi kwa mahaba yenu juu ya USA na EU [emoji4]
Mkuu umepiga kwenye mshono hapo kwenye mstari wa mwisho
 
Anga linafungwa na nini? Kufuli za Solex ama?

Kuna nchi za kufungia anga kama Libya ila sio Russia.

Unaifahamu Tu-160? Ka google usome, hio ni bomber ambayo supersonic inapiga mach 2.05 at altitude.

Inabeba ton 20 ya free falling body ikiwemo silaha za nuclear cause ni nuclear capable bomber.

Ndio ndege yenye kasi zaidi, kubwa zaidi ya kijeshi na nzito zaidi kuwahi kuruka ambayo ina sweep wing.

Nimesema hio ndege ni supersonic kwenye speed kali licha ya ukubwa wake, mbawa zake huwa zinarudi nyuma inakua kama Mig.
Ikiwa slow inapanua mbawa zake kama Boeing 787 au ndege ya abiria ya kawaida.

Hio ndege ina uwezo wa kuipiga Kiev kukabaki shimo baadae kizazi kijacho wakaja kudhani kuna kimondo kilitua kama kule Arizona. Tena inapiga nje kabisa ya anga umbali wa km 5500.

Kumbuka hizo wanazo zaidi ya 60.

Kuna kitu kinaitwa s500 kuna mdau mmoja amesema humu ina uwezo wa kuzuia hata punje ya mchele[emoji23][emoji23][emoji23], mi namuunga mkono, kwa maana s500 inashusha satellite.

Kama radar inaona tone la mvua basi hata punje ya mchele ukiirusha tokea Kiev itaonekana tu ikiingia Russia.

Nato haina uwezo wa kuifungia Russia anga.

Ndio maana nikasema labda wafunge na kufuli.

Unaposikia Russia wanasema wanafanya operation ujue wanafanya operation.

Putin hataki kuichukua Ukraine iliyo vipande vipande anaitaka nzima nzima, na Ukraine.

Kwa hio mkuu Russia si nchi ya mchezo mchezo kwenye vita.

Halafu huwezi kumpangia mtu kushambulia vipi.
Mbwembwe tu hizo Russia ameshazea za chembe Ukraine....mlisema siku 2 Ukraine itakuwa imetekwa leo unaenda mwezi mambo magumu...
 
Warusi wataomba poo mda si mrefu.
Mahesabu ilikua watwange Ukraine siku kadhaa tu waiweke chini yao.
Imeshindikana,kuna vikosi vipo pale ndani sio NATO wala EU combat force wanapigana kwa kwenda mbele,hakuna utambulisho ila wapo.
Kuna mabus yanaondoka na nguo zana na wanajeshi every week.
Wanaenda huko.
Ukraine kama yeye mpaka leo angeshasurrender.
Pale ni battle field tu.
Mrusi anapigana na Mmarekani na watu wake.
Kinachoogopwa Putin anaweza kuanzisha libeneke nchi zote za Scandinavia anawamudu.
Yuko jirani tu nao.
Hapo ndo utaskia WW3.
HAWAwataungana na ndio exit ya Putin.
Kwa ubishi atajiua tu km Hitler.
Hawezi kuanzisha vita na NATO Ukraine tu inamtoa jasho kama sio haja kubwa
 
Hapo kichwan hamna kitu

Ingekua 80% ya nguvu ya jeshi ya Ukraine imeteketezwa s Ukraine yote ingekua chini ya Urus? Yani 20% ya nguvu inaizuia urusi ishindwe chukua hata mji mmoja ??

Nyie ndio mnasababisha CCM inaendelea kudunda.. ujinga mtupu
Saivi wanapigana kama wakora hamna jeshi
 
Wamarekani wa kwa mtogole muwe na akili hata kwa 25% kuwa bila ya misaada ya silaha za kivita na wanajeshi toka EU kama Canada, hao Ukraine wangekuwa katika hali gani hivi sasa [emoji848]

Russia hajaomba msaada kwa Taifa lolote zaidi ya kupambana kiume na USA na EU hadi sasa, na mzidishe maombi China, North Korea, Iraq na Iran wasitie maguu kumsapoti RUSSIA kama USA anavyosapotiwa na EU katika hii vita, la sivyo WWIII ina-download wakati wowote itaitika ndipo tutapozidi kuendelea kukaza mafuvu kujua uwezo wa RUSSIA kiuchumi, kiujasusi, kivita, kiteknolojia, kibiashara na hata kirasilimali duniani [emoji847]
Nguvu za mtu ni pamoja na support aliyonayo. Huwezi ukabagua eti hizi ni nguvu za fulani ana zile ni za mtu mwingine.

Ukraine ana marafiki wa kweli. Urusi ana marafiki wanafiki
 
Waache wauane tu mi nasubiri vita iishe maana watu watakuwa hakuna wataanza kuita watu kutoka nchi zingine ili wakuze uchumi wao hapo sasa ndio kuokota dodo kwenye mpera chap naibuka zangu yukreini kuwa raia nishachoka na mfumuko wa bei bongo,
 
Warus wanachukuliaga vita poah sana yan walivyokua wanaingia kwa msururu ,Ukraine utafikir msafara wa harus ,hawana protection wanajiendea kama mazombi,kuna mji huko karibu na kyv waliuteka ,wasinyo na akili wamejikusanya sehemu kama wanachek mpira ,aisee wamefanyiwa counter attack moja wamejeuka majivu,walionusurika nadhan hawatarud urusi
[emoji16][emoji16][emoji16] Western propaganda Ni shiida.
Screenshot_20220326-013126.jpg
 
Back
Top Bottom