Urusi imehusisha asilimia 75% ya jeshi lake lote kwenye huu ugomvi, na bado shughuli ipo

inaonekana NATO haipo sayari hii kwamba huo mzigo wao mpaka leo haujafika tuu RUSSIA kaishajiandaa na yote hayo
unahisi kwamba RUSSIA hakujua kwamba NATO watamsaidia MBWA wao namna ya KUBWEKA?
NATO anajua kabisa kuwa Russia bado hajafungulia turbo hapo!

Hao ni wanajeshi wa internship ndio wanatembeza kichapo na mavifaa ya kizamani! Hajafungua ile mizigo new model😅😆😁 ila akiifungua hamna kenge atabakia.
 
Jamaaa hatani aisee na hii ya kusema kapeleka asilimia 75 ni mitego Kwa Nato ili wajifanye hamnazo awabutue nao. Bunge la ujeruman Leo hii wanalaumiana na wanaogopa kumvaa mrusi kichwa kichwa unahis wajerumani hawajui mtiti wa Urusi
Mjerumani alichapika vilivyo hajasahau kile kipigo cha kihistoria 😅 kilichozalisha topic za form 2 kwenye vitabu mbali mbali nchini!
 
Anaesema kaacha wachache ni ww
 
Don't trust western media
 
Acha kupotosha wewe,aliyekumbia jeshi zima la urusi lina wanajeshi 120,000 kakudanganya,google kisha urudi hapa kubisha tena.Jeshi la urusi lina wanajeshi zaidi ya milioni 1 waliopo kazini na zaidi ya milioni 2 wa akiba.Na pia hiyo idadi ya waliongia ukraine umeitoa wapi?
 
Ndoto za alinacha. Huo ugomvi hauishi leo wala mwezi huu
 
Sio kweli. Kimkakati (strategic) na kijeshi (military) huwezi kutumia hata nusu ya nyenzo, u aweza pigwa kama kenge mwizi siku za usoni.
 
bila swaka upo karibu na bwana Putini
 

Unajiaibisha!! Tatizo huijui lugha ya malkia!! Wanaposema Urusi imeingiza asilimia 75 ya jeshi lake (120,000) Ukraine wanamaanisha ni wale wanajeshi waliokuwa mpakani na Ukraine, walioandaliwa kwa kazi hiyo ya dharula. Idadi ya wanajeshi hao inakadiriwa kuwa ni 150,000. Sasa mwenzangu na mimi anadhani ni asilimia 75 ya jeshi lote la Urusi!!! Pole!! Jeshi lote la Urusi si askari 150,000!!! Pole tena!!! Uliza upewe data!!
 
Upo sahihi na nikwambie kitu Mkuu. Akili ya mrusi alifikiri Ni Kama kumchukua mtoto na kumchapa fimbo bila yeye kurudishia. Yanayoendelea akuyategemea na mtazamo wa kiburi Cha Putin ni siraha za nyukilia tu.
 
Hii vita ikiendelea kwa mda wa mwezi mmoja plus urusi atakuwa kwenye mgogoro mkubwa wa kiuchumi anacho jaribu kufanya ni kufanya uaribifu wa miondo mbinu, majengo na makazi ya watu kwa kutumia nguvu kubwa na silaha ambazo sio sehemu husika ili vita isichukue mda mrefu. Hii ni mbinu ya kuwavunja raia morali kisaikolojia ili waogope lakini hali ikiendelea hivi hivi lazima watakaa mezani kufikia muafaka jambo ambalo ni gumu kupigana vita sio lelemama haijalishi how strong you are
 
Unaijua nguvu kubwa ya Russia? Russia ikitumia nguvu kubwa yawezekana asilimia 90-95 ya watu duniani wakapoteza maisha kwa sababu atatumia chemical, biological na nuclear weapons. Mpaka sasa Ukraine hata chemical weapons
Hayo ni maneno yenu ya kila siku ya kwenye karatasi tofauti na tunavyoona uhalisia grounds. By the way hizo nuclear,biological na chemicals weapons anazo Mrusi peke yake? Mrusi ni Chui wa Karatasi.
 
Western media propaganda
 
Tutaona wataalamu wengi wa kivita wanaotoka katika vijiwe vya kahawa
 

Kuwekeza wanajeshi 120,000 kwenye vita ni jambo la gharama sana, akiendelea kuburuza itamgharimu sana kiuchumi, muda sio mrefu hao wanajeshi wataanza kuiba bata na kuku kutoka kwa wanavijiji.
Naona jamaa anapata hasira sana kadiri anavyozidi kucheleweshwa, na hatari nyingine ni pale wananchi wataanza kuzoea na kuhimili mabomu yake, kawaida siku za mwanzo mwanzo husababisha uwoga, lakini mkizoea milipuko, mnakua sugu nyote na kuendelea kwenye mapambano.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…