Urusi imeingia kwenye 18 ya Marekani, dunia ijiandae kuona majimbo mapya ya Marekani katika ardhi ya Urusi

Marekani kukanyaga ardhi ya Russia ni kitu hatari anachoogopa kufanya hata kwa bahati mbaya.
Ni sawasawa na tembo kukanyaga ufalme wa simba.
Endelea kutega sikio mkuu, kitachotokea huko mbele kitakushangaza sana.
 
Tembo huwa anajipitia popote tu ilimradi iwe njia yao. Hata makazi ya binadamu.
Ya kweli mkuu, tembo hupita popote iwe majini au ardhini na hakuna mnyama anaeweza kuwa na mawazo ya kipumbavu eti kujaribu kumvamia.
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ni kweli anapita popote, Je nini kinamtokea akipita kwenye ufalme wa simba?
Mara nyingi hakuna kinachotokea. Simba huwa anakwepa na kuwaacha wapite sababu licha ya kwamba wao sio washindani wa chakula pia Tembo hutembea katika makundi. Ni nadra sana simba kuwavamia tembo. Inatokea ila ni nadra na ni kazi ngumu sana kumwangusha tembo. Ni rahisi zaidi Simba kuuwawa ikiwa hatakuwa makini.
 
Za asubuhi ndugu zangu, kwema?

Kwa wale wanajamii forums wenzangu wafuatiliaji wa siasa za kibabe na za kimikakati za nchi za magharibi hasa Marekani. Bila shaka mtakubaliana na mimi kwamba sasa Russia (itake isitake) inakwenda kugawana baadhi ya majimbo yake ya mpakani na Marekani kupitia mgongo wa vita yake (Russia) na Ukraine.

Ni nani asiejua kwamba toka miaka mingi iliyopita, lengo kuu la Marekani na washirika wake lilikuwa ni kuigawanya Urusi vipande vipande ili iwe na eneo dogo, jeshi dogo na uchumi wa kawaida kwa ajili ya masilahi mapana ya kijeshi, kiuchumi na kiubabe kwa Marekani na washirika wake!

Hata kugawanyika kwa umoja wa nchi za Soviet pia kulikuwa na mkono wa Marekani na washirika wake, ambao wanataka kuiona Russia inakua nchi yenye kaeneo ka kawaida, jeshi la kawaida na uchumi wa kawaida kama ilivyo Iran, North Korea, Venezuela nk.

Sasa basi, kwa vile mkakati wa kuigawanya Urusi kwa njia ya kawaida ulishindikana, ndo ukatengenezwa mkakati wa kuanzisha zengwe katika mipaka ya Russia kwa kuitumia nchi ya Ukraine huku Marekani akiamini kwamba zengwe hilo lingeweza kuzaa matunda kwa kuishawishi Russia (bila kujua) iingie katika vita na Ukraine, na hatimae baadae Urusi itapoanza kuwa weak (kuelemewa) kutokana na vita hivyo.

Marekani na washirika wake waitumie nafasi hiyo kuitwanga Russia (kupitia jeshi la Ukraine) na hatimae kuingia mpaka Russia kama vile Russia ilivyoingia Ukraine. Ukraine itapoingia Russia, Marekani ataendelea kutuma silaha nzito nzito mno za kijeshi ili kuwapa nguvu zaidi wanajeshi wa Ukraine kuteka baadhi ya majimbo ya Russia yaliopo katika mpaka na Ukraine.

Ikumbukwe kwamba Marekani na washirika wake hawajaingia kwenye hii vita kijeshi, lkn wamekuwa wakituma silaha mbali mbali kwa jeshi la Ukraine ili kutimiza mipango yao, na kwa kiasi kikubwa zimeleta mafanikio makubwa kwa jeshi la Ukraine.

Mmarekani chini ya CIA yake sio mjinga wa kutuma tu mamilioni ya dola na silaha nzito nzito kwa Ukraine bila kujua hizo hela atazirudisha vipi. Bila shaka anajua anachokifanya, na huu ni mkakati wa muda mrefu ambao Putin bila kujua ameingia kichwa kichwa vitani asijue madhara yake ya baadae.

Vita hii ni kama mpira wa miguu ambapo timu iliyoanza kushambulia, sasa inashambuliwa huku wachezaji wake hadi wa akiba wakiwa hoi bint tabaani wasijue nini kifanyike ili kuzuia kufungwa.

Vita ilianza kwa Russia kuishambulia Ukraine na kuleta furaha kubwa huko Moscow hali iliyokuwa inapelekea Putin kuongea kibabe na kwa kejeli kubwa dhidi ya Ukraine na washirika wake (Marekani, UK)

Lakini sasa vita imegeuka, Russia sasa ndio inashambuliwa, furaha ya Moscow imegeuka majonzi, mpaka wanajeshi wa akiba wamepelekwa Ukraine, lkn kichapo ni kilekile.

Putin anataman ipatikane suluhu hata kesho ili Marekani asipate nafasi ya kukamilisha mission zake, ila ni kama vile amechelewa,,, na yeye kutafuta suluhu kupitia yeye mwenyewe hawezi, maana itaonekana ameshindwa vita alivyoanzisha, hivyo itakuwa aibu kwake, kwa jeshi lake na nchi yake.

Marekani anapokuwa na lengo la kuvamia nchi fulan kwa ajili ya masilahi yake fulan, basi huwa na njia nyingi tofauti tofauti za kukamilisha lengo hilo bila kujali itamchukua muda gani, na atapata kwanza hasara kiasi gani.

Tuliona alivyotumia mgongo wa Osama kuivamia Afghanistan, tuliona alivyotumia mgongo wa silaha sijui za sumu kuivamia Iraq chini ya Sadam Hussein, tuliona alivyotumia mgongo wa waandamanaji kuivamia Libya, na sasa anatumia mgongo wa jeshi la Ukraine kuivamia Russia.

Japo si kwa nchi yote, lkn kuna baadhi ya maeneo tutakuja kusikia yalivamiwa, kutekwa na kushikiliwa na jeshi la Ukraine (kumbe nyuma ya pazia) maeneo hayo yatakayotekwa yatakuwa chini ya usimamizi wa Marekani.

Hivi sasa Ukraine ishaanza kurudisha maeneo yao yaliotekwa, na kuyarudisha nyuma tena kwa kasi majeshi ya Russia. Ni swala la muda tu mtakuja kuona haya niliyoandika hapa yanatokea, na Putin hatothubutu kurusha bom la nyuklia hata 1, maana kwa vile Mmarekani atakuwa katika baadhi ya maeneo ya ardhi yake, basi akijaribu kurusha atajikuta anajiangamiza yeye mwenyew na watu wake.

Miezi kadha iliyopita China ilitaka kufanya kosa lile lile alilofanya Mrusi, eti alitaka kuivamia Taiwan aifunze adabu. Mimi kwa kutambua hatari iliyopo mbele ya China endapo angeivamia Taiwan, nilikuja fasta fasta kutoa ushauri wangu kwa ndugu zetu wa China ili kuiepusha na mtego uliokuwa umetegwa na wakubwa pale China angethubutu tu kuivamia Taiwan.

Sina haja ya kuweka link ili kuwachosha wasomaji, kwahiyo naweka tu kipande cha picha ya onyo langu hapo chini. Ila atakaetaka kuusoma uzi wenyewe niliowaandikia wa China atautafuta mwenyew ausome kwa kutulia.

Karibuni kwa uchangiaji zaidi, hasa kwa wale wenye uelewa mpana kuhusu malengo na mikakati ya vita hii.

Moderators najua kuna jukwaa la international, lkn nimeuleta uzi huu uku kwa sababu zangu [emoji120]

Nawatakieni siku njema.
Tuliza mshono ww na Ki history chako cha O level na high level
Putin na Russia yake ni namba nyingine, USA na Russia wanajuana hao
 
Ni kweli anapita popote, Je nini kinamtokea akipita kwenye ufalme wa simba?
Mkuu tembo hajawahi kudhuriwa na mnyama wa aina yoyote hapa duniani, iwe majini au ardhini.
Ukiona tembo kavamiwa na simba, mamba au mnyama yoyote basi jua huyo ni mtoto tena aliepotezana na mama yake. Fuatilia maisha ya tembo porini ndo utakubali. Jamaa anajamini kupita kiasi, anaweza kusimama barabarani hata dakika 30 bila gari yoyote kupita mpaka pale atakapoamua yeye mwenyew kuipisha ipite. So huo mfano wako kwa tembo umekosea sana unless kama utakua haumjui tembo vizuri.
 
Kuna wakati najiskia kucheka, wizara ya ulinzi Russia inasema tumeondoka maeneo Yale na Yale kwa sababu Ukraine katumia silaha za West...
Kwa nin Russians wasijibu kwa silaha za kirusi?
🤣🤣🤣 Genge la Putin halitokuelewa humu mitandaoni.
 
Mara nyingi hakuna kinachotokea. Simba huwa anakwepa na kuwaacha wapite sababu licha ya kwamba wao sio washindani wa chakula pia Tembo hutembea katika makundi. Ni nadra sana simba kuwavamia tembo. Inatokea ila ni nadra na ni kazi ngumu sana kumwangusha tembo. Ni rahisi zaidi Simba kuuwawa ikiwa hatakuwa makini.

Mkuu tembo hajawahi kudhuriwa na mnyama wa aina yoyote hapa duniani, iwe majini au ardhini.
Ukiona tembo kavamiwa na simba, mamba au mnyama yoyote basi jua huyo ni mtoto tena aliepotezana na mama yake. Fuatilia maisha ya tembo porini ndo utakubali. Jamaa anajamini kupita kiasi, anaweza kusimama barabarani hata dakika 30 bila gari yoyote kupita mpaka pale atakapoamua yeye mwenyew kuipisha ipite. So huo mfano wako kwa tembo umekosea sana unless kama utakua haumjui tembo vizuri.
Mmeshindwa kuelewa metaphor.
Tembo ana mwili mkubwa na mwenye nguvu lakini siku zote wanajaribu kukaa mbali na simba sababu ya tabia zao.
Simba ukimbana na akachoka atafanya chochote kile ili akumalize na haijalishi kama atakufa.
 
Za asubuhi ndugu zangu, kwema?

Kwa wale wanajamii forums wenzangu wafuatiliaji wa siasa za kibabe na za kimikakati za nchi za magharibi hasa Marekani. Bila shaka mtakubaliana na mimi kwamba sasa Russia (itake isitake) inakwenda kugawana baadhi ya majimbo yake ya mpakani na Marekani kupitia mgongo wa vita yake (Russia) na Ukraine.

Ni nani asiejua kwamba toka miaka mingi iliyopita, lengo kuu la Marekani na washirika wake lilikuwa ni kuigawanya Urusi vipande vipande ili iwe na eneo dogo, jeshi dogo na uchumi wa kawaida kwa ajili ya masilahi mapana ya kijeshi, kiuchumi na kiubabe kwa Marekani na washirika wake!

Hata kugawanyika kwa umoja wa nchi za Soviet pia kulikuwa na mkono wa Marekani na washirika wake, ambao wanataka kuiona Russia inakua nchi yenye kaeneo ka kawaida, jeshi la kawaida na uchumi wa kawaida kama ilivyo Iran, North Korea, Venezuela nk.

Sasa basi, kwa vile mkakati wa kuigawanya Urusi kwa njia ya kawaida ulishindikana, ndo ukatengenezwa mkakati wa kuanzisha zengwe katika mipaka ya Russia kwa kuitumia nchi ya Ukraine huku Marekani akiamini kwamba zengwe hilo lingeweza kuzaa matunda kwa kuishawishi Russia (bila kujua) iingie katika vita na Ukraine, na hatimae baadae Urusi itapoanza kuwa weak (kuelemewa) kutokana na vita hivyo.

Marekani na washirika wake waitumie nafasi hiyo kuitwanga Russia (kupitia jeshi la Ukraine) na hatimae kuingia mpaka Russia kama vile Russia ilivyoingia Ukraine. Ukraine itapoingia Russia, Marekani ataendelea kutuma silaha nzito nzito mno za kijeshi ili kuwapa nguvu zaidi wanajeshi wa Ukraine kuteka baadhi ya majimbo ya Russia yaliopo katika mpaka na Ukraine.

Ikumbukwe kwamba Marekani na washirika wake hawajaingia kwenye hii vita kijeshi, lkn wamekuwa wakituma silaha mbali mbali kwa jeshi la Ukraine ili kutimiza mipango yao, na kwa kiasi kikubwa zimeleta mafanikio makubwa kwa jeshi la Ukraine.

Mmarekani chini ya CIA yake sio mjinga wa kutuma tu mamilioni ya dola na silaha nzito nzito kwa Ukraine bila kujua hizo hela atazirudisha vipi. Bila shaka anajua anachokifanya, na huu ni mkakati wa muda mrefu ambao Putin bila kujua ameingia kichwa kichwa vitani asijue madhara yake ya baadae.

Vita hii ni kama mpira wa miguu ambapo timu iliyoanza kushambulia, sasa inashambuliwa huku wachezaji wake hadi wa akiba wakiwa hoi bint tabaani wasijue nini kifanyike ili kuzuia kufungwa.

Vita ilianza kwa Russia kuishambulia Ukraine na kuleta furaha kubwa huko Moscow hali iliyokuwa inapelekea Putin kuongea kibabe na kwa kejeli kubwa dhidi ya Ukraine na washirika wake (Marekani, UK)

Lakini sasa vita imegeuka, Russia sasa ndio inashambuliwa, furaha ya Moscow imegeuka majonzi, mpaka wanajeshi wa akiba wamepelekwa Ukraine, lkn kichapo ni kilekile.

Putin anataman ipatikane suluhu hata kesho ili Marekani asipate nafasi ya kukamilisha mission zake, ila ni kama vile amechelewa,,, na yeye kutafuta suluhu kupitia yeye mwenyewe hawezi, maana itaonekana ameshindwa vita alivyoanzisha, hivyo itakuwa aibu kwake, kwa jeshi lake na nchi yake.

Marekani anapokuwa na lengo la kuvamia nchi fulan kwa ajili ya masilahi yake fulan, basi huwa na njia nyingi tofauti tofauti za kukamilisha lengo hilo bila kujali itamchukua muda gani, na atapata kwanza hasara kiasi gani.

Tuliona alivyotumia mgongo wa Osama kuivamia Afghanistan, tuliona alivyotumia mgongo wa silaha sijui za sumu kuivamia Iraq chini ya Sadam Hussein, tuliona alivyotumia mgongo wa waandamanaji kuivamia Libya, na sasa anatumia mgongo wa jeshi la Ukraine kuivamia Russia.

Japo si kwa nchi yote, lkn kuna baadhi ya maeneo tutakuja kusikia yalivamiwa, kutekwa na kushikiliwa na jeshi la Ukraine (kumbe nyuma ya pazia) maeneo hayo yatakayotekwa yatakuwa chini ya usimamizi wa Marekani.

Hivi sasa Ukraine ishaanza kurudisha maeneo yao yaliotekwa, na kuyarudisha nyuma tena kwa kasi majeshi ya Russia. Ni swala la muda tu mtakuja kuona haya niliyoandika hapa yanatokea, na Putin hatothubutu kurusha bom la nyuklia hata 1, maana kwa vile Mmarekani atakuwa katika baadhi ya maeneo ya ardhi yake, basi akijaribu kurusha atajikuta anajiangamiza yeye mwenyew na watu wake.

Miezi kadha iliyopita China ilitaka kufanya kosa lile lile alilofanya Mrusi, eti alitaka kuivamia Taiwan aifunze adabu. Mimi kwa kutambua hatari iliyopo mbele ya China endapo angeivamia Taiwan, nilikuja fasta fasta kutoa ushauri wangu kwa ndugu zetu wa China ili kuiepusha na mtego uliokuwa umetegwa na wakubwa pale China angethubutu tu kuivamia Taiwan.

Sina haja ya kuweka link ili kuwachosha wasomaji, kwahiyo naweka tu kipande cha picha ya onyo langu hapo chini. Ila atakaetaka kuusoma uzi wenyewe niliowaandikia wa China atautafuta mwenyew ausome kwa kutulia.

Karibuni kwa uchangiaji zaidi, hasa kwa wale wenye uelewa mpana kuhusu malengo na mikakati ya vita hii.

Moderators najua kuna jukwaa la international, lkn nimeuleta uzi huu uku kwa sababu zangu 🙏

Nawatakieni siku njema.
Umeongea ukweli mtupu mkuu. Japo humu walio wengi ni warusi wa namtumbo. Watakuja hapa mbio kukanusha bila umeelewa wowote
 
Putin alipiga mkwara kwamba kama wanajeshi wa Ukraine hawatojisalimisha wao na silaha zao au kumpindua raisi wao. Basi wajue kwamba siku 5 zilizopo mbele yao ndio utakuwa mwisho wao.

Sasa jeshi halikujisalimisha na badala yake linatoa kichapo kitakatifu kwa genge la Putin mpaka mwenyew anahisi kuchanganyikiwa.
Yaan Putin na mkubali kwa mawazo yake yakupinga ushoga.
Ila kwa Vita amekalushwa.Huku mtaani tunasema Putin kawa Mchumba kwa Ukrain
 
Inawezekana huu uvamizi wa Putin ukaanzisha uasi wa kimajimbo ndani ya Russia. Ni suala la muda.
Ukizingatia kwa sasa putin ana upinzani mkubwa hata wa ndani ya nchi yake. Hata hii vita wananchi wengi,hata wanajeshi walikuwa hawaitaki. Ni vile tu putin anaiongoza urusi kwa mkono wa chuma. Hataki mtu ndani yake awe against na yeye. Hata waandishi wa habari huwezi kusikia anaandika against na anachokitaka putin
 
Kuna propaganda nyingi sana kwenye vita hii hasa kutoka vyombo vya habari vya magharibi. Mafanikio ya Ukraine kwenye uwanja wa mapambano yanatiwa chumvi ili ionekane Urusi si chochote. Kwenye vita suala la kuteka eneo au askari, kuua au kuuliwa ni jambo la kawaida. Warusi ni binadamu kwahiyo wakiwa vitani watakufa au kutekwa. Kwahiyo, tusubiri final outcome of the war kwa sasa Marekani na vibaraka wake wako bize na propaganda.
Bora umesema ukweli Toka nione video za warusi wakijenga shule na hospital ndani ya ardhi ya Ukraine kana kwamba hakuna kinachoendelea nimewavua vyeo wote hawa chawa wa NATO na jamaa zao wamewekeza sana kweny midomo na vyombo vya habari na ukitazma Ile speech ya Putin wakati wakuidhinisha Ile mikoa minne ya Ukraine kuwa ni sehemu ya Russia utagundua Kuwa awa jamaa wa NATO wanamidomo sana

Sent from my Infinix PR652B using JamiiForums mobile app
 
Mmeshindwa kuelewa metaphor.
Tembo ana mwili mkubwa na mwenye nguvu lakini siku zote wanajaribu kukaa mbali na simba sababu ya tabia zao.
Simba ukimbana na akachoka atafanya chochote kile ili akumalize na haijalishi kama atakufa.
Narudia tena.. tembo hajawahi na hatowahi kumu avoid simba au mnyama wa aina yoyote hapa duniani.
Simba hana ujanja wala nguvu ya kumdhibiti hata kifaru, itakuwa tembo? Bila shaka wewe unaongea kishabiki lkn sio ki uhalisia.
 
UMESHINDWA KUELEWA METAPHOR.
Au unadhani nimekurupuka kuchukua mfano wa tembo na simba. Siongelei wanyama hapa bali ni METAPHOR.
Kwa akili yako ya kawaida kabisa unadhani Marekani anaweza kukanyaga Russia nchi ambayo anaiogopa tangu enzi za cold war?
 
Za asubuhi ndugu zangu, kwema?

Kwa wale wanajamii forums wenzangu wafuatiliaji wa siasa za kibabe na za kimikakati za nchi za magharibi hasa Marekani. Bila shaka mtakubaliana na mimi kwamba sasa Russia (itake isitake) inakwenda kugawana baadhi ya majimbo yake ya mpakani na Marekani kupitia mgongo wa vita yake (Russia) na Ukraine.

Ni nani asiejua kwamba toka miaka mingi iliyopita, lengo kuu la Marekani na washirika wake lilikuwa ni kuigawanya Urusi vipande vipande ili iwe na eneo dogo, jeshi dogo na uchumi wa kawaida kwa ajili ya masilahi mapana ya kijeshi, kiuchumi na kiubabe kwa Marekani na washirika wake!

Hata kugawanyika kwa umoja wa nchi za Soviet pia kulikuwa na mkono wa Marekani na washirika wake, ambao wanataka kuiona Russia inakua nchi yenye kaeneo ka kawaida, jeshi la kawaida na uchumi wa kawaida kama ilivyo Iran, North Korea, Venezuela nk.

Sasa basi, kwa vile mkakati wa kuigawanya Urusi kwa njia ya kawaida ulishindikana, ndo ukatengenezwa mkakati wa kuanzisha zengwe katika mipaka ya Russia kwa kuitumia nchi ya Ukraine huku Marekani akiamini kwamba zengwe hilo lingeweza kuzaa matunda kwa kuishawishi Russia (bila kujua) iingie katika vita na Ukraine, na hatimae baadae Urusi itapoanza kuwa weak (kuelemewa) kutokana na vita hivyo.

Marekani na washirika wake waitumie nafasi hiyo kuitwanga Russia (kupitia jeshi la Ukraine) na hatimae kuingia mpaka Russia kama vile Russia ilivyoingia Ukraine. Ukraine itapoingia Russia, Marekani ataendelea kutuma silaha nzito nzito mno za kijeshi ili kuwapa nguvu zaidi wanajeshi wa Ukraine kuteka baadhi ya majimbo ya Russia yaliopo katika mpaka na Ukraine.

Ikumbukwe kwamba Marekani na washirika wake hawajaingia kwenye hii vita kijeshi, lkn wamekuwa wakituma silaha mbali mbali kwa jeshi la Ukraine ili kutimiza mipango yao, na kwa kiasi kikubwa zimeleta mafanikio makubwa kwa jeshi la Ukraine.

Mmarekani chini ya CIA yake sio mjinga wa kutuma tu mamilioni ya dola na silaha nzito nzito kwa Ukraine bila kujua hizo hela atazirudisha vipi. Bila shaka anajua anachokifanya, na huu ni mkakati wa muda mrefu ambao Putin bila kujua ameingia kichwa kichwa vitani asijue madhara yake ya baadae.

Vita hii ni kama mpira wa miguu ambapo timu iliyoanza kushambulia, sasa inashambuliwa huku wachezaji wake hadi wa akiba wakiwa hoi bint tabaani wasijue nini kifanyike ili kuzuia kufungwa.

Vita ilianza kwa Russia kuishambulia Ukraine na kuleta furaha kubwa huko Moscow hali iliyokuwa inapelekea Putin kuongea kibabe na kwa kejeli kubwa dhidi ya Ukraine na washirika wake (Marekani, UK)

Lakini sasa vita imegeuka, Russia sasa ndio inashambuliwa, furaha ya Moscow imegeuka majonzi, mpaka wanajeshi wa akiba wamepelekwa Ukraine, lkn kichapo ni kilekile.

Putin anataman ipatikane suluhu hata kesho ili Marekani asipate nafasi ya kukamilisha mission zake, ila ni kama vile amechelewa,,, na yeye kutafuta suluhu kupitia yeye mwenyewe hawezi, maana itaonekana ameshindwa vita alivyoanzisha, hivyo itakuwa aibu kwake, kwa jeshi lake na nchi yake.

Marekani anapokuwa na lengo la kuvamia nchi fulan kwa ajili ya masilahi yake fulan, basi huwa na njia nyingi tofauti tofauti za kukamilisha lengo hilo bila kujali itamchukua muda gani, na atapata kwanza hasara kiasi gani.

Tuliona alivyotumia mgongo wa Osama kuivamia Afghanistan, tuliona alivyotumia mgongo wa silaha sijui za sumu kuivamia Iraq chini ya Sadam Hussein, tuliona alivyotumia mgongo wa waandamanaji kuivamia Libya, na sasa anatumia mgongo wa jeshi la Ukraine kuivamia Russia.

Japo si kwa nchi yote, lkn kuna baadhi ya maeneo tutakuja kusikia yalivamiwa, kutekwa na kushikiliwa na jeshi la Ukraine (kumbe nyuma ya pazia) maeneo hayo yatakayotekwa yatakuwa chini ya usimamizi wa Marekani.

Hivi sasa Ukraine ishaanza kurudisha maeneo yao yaliotekwa, na kuyarudisha nyuma tena kwa kasi majeshi ya Russia. Ni swala la muda tu mtakuja kuona haya niliyoandika hapa yanatokea, na Putin hatothubutu kurusha bom la nyuklia hata 1, maana kwa vile Mmarekani atakuwa katika baadhi ya maeneo ya ardhi yake, basi akijaribu kurusha atajikuta anajiangamiza yeye mwenyew na watu wake.

Miezi kadha iliyopita China ilitaka kufanya kosa lile lile alilofanya Mrusi, eti alitaka kuivamia Taiwan aifunze adabu. Mimi kwa kutambua hatari iliyopo mbele ya China endapo angeivamia Taiwan, nilikuja fasta fasta kutoa ushauri wangu kwa ndugu zetu wa China ili kuiepusha na mtego uliokuwa umetegwa na wakubwa pale China angethubutu tu kuivamia Taiwan.

Sina haja ya kuweka link ili kuwachosha wasomaji, kwahiyo naweka tu kipande cha picha ya onyo langu hapo chini. Ila atakaetaka kuusoma uzi wenyewe niliowaandikia wa China atautafuta mwenyew ausome kwa kutulia.

Karibuni kwa uchangiaji zaidi, hasa kwa wale wenye uelewa mpana kuhusu malengo na mikakati ya vita hii.

Moderators najua kuna jukwaa la international, lkn nimeuleta uzi huu uku kwa sababu zangu [emoji120]

Nawatakieni siku njema.
Nonsense
 
Ya kweli mkuu, tembo hupita popote iwe majini au ardhini na hakuna mnyama anaeweza kuwa na mawazo ya kipumbavu eti kujaribu kumvamia.
Kabisa boss. Hata Mamba na ubabe wao majini hutulia Tembo wapite wakijifanya kama vile wana upendo na furaha sana kupata hiyo nafasi ya Tembo kupita kwenye makazi yao.
images - 2022-10-06T102319.345.jpeg

images - 2022-10-06T105203.587.jpeg
 
Umeongea ukweli mtupu mkuu. Japo humu walio wengi ni warusi wa namtumbo. Watakuja hapa mbio kukanusha bila umeelewa wowote
Asante mkuu kwa kulitambua hilo. Najua wapo warusi wa namtumbo wanaojaribu kukanusha, lkn mda si mrefu watajionea wao wenyew kwa macho yao.
 
Ukizingatia kwa sasa putin ana upinzani mkubwa hata wa ndani ya nchi yake. Hata hii vita wananchi wengi,hata wanajeshi walikuwa hawaitaki. Ni vile tu putin anaiongoza urusi kwa mkono wa chuma. Hataki mtu ndani yake awe against na yeye. Hata waandishi wa habari huwezi kusikia anaandika against na anachokitaka putin
Kweli mkuu, nashukur kwa tasmini nzuri na inayoeleweka.
 
Back
Top Bottom