Hahahaha Mkuu ukisiliza update za Russia unaweza jua wameshaua wanajeshi wote wa Ukraine,kuna taarifa nyingine niliona wameua wanajeshi 1000 wa Ukraine [emoji23]. Yani tangu waseme wameshaharibu karibu HIMARS karibu zote,na kutungua Bayraktar drone 100 za Ukraine wakati Ukraine alikua nazo 36 tu nikiona taarifa zao nacheka tu halafu nasema hiiiiiii.
Huko kwao wamefungia vyombo vya habari na ukileta taarifa yako kinyume na za mamlaka jiandae kwenda jela unategemea nini zaidi ya kuwalisha watu wao propaganda?!
Walisema wameharibu Airforce yote ya Ukraine cha ajabu mpaka Leo ndege za Ukraine zinaruka na kufanya mashambulizi dhidi ya wanajeshi wa Urusi. Hawajatoa idadi ya wanajeshi wao waliokufa karibu miezi sita sasa mara ya Mwisho walitoa mwezi March. Babu Yao Putin kaona mambo magumu mpaka kakimbilia Tehran kuomba msaada wa drones,embu fikiria Leo hii Russia ni kwenda kuomba msaada Iran kweli,Yani hapo ni sawa na Marekani aende kuomba msaada wa kijeshi Misri!!!!
Na swali la Mwisho la kujiuliza wanasema wameua wanajeshi 500+,je ushahidi uko wapi?! Watume hata kapicha bhas Ka wanajeshi japo 50 waliodedi