Urusi inaweza kuivamia Ukraine muda wowote, Marekani yatoa angalizo, yataka raia wake waondoke Ukraine

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Marekani imeonya kuwa Urusi inaweza kuivamia kijeshi Ukraine muda wowote. Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani, Jake Sullivan amesema uvamizi huo unaweza ukaanza kwa makombora na mashambulizi ya anga.

Tangazo la Marekani linatokana na taarifa mpya za kijasusi kuhusu kuongezeka kwa wanajeshi wa Urusi kwenye mipaka ya Ukraine katika wiki moja iliyopita.

Akizumgumza na waandishi habari katika Ikulu ya Marekani, Sullivan amesema huo ni ujumbe wa dharura kwa sababu wako katika hali ya dharura.

Amesema Urusi ina majeshi yote inayohitaji kufanya mashambulizi makubwa ya kijeshi na nchi hiyo inaweza kuchagua ndani ya kipindi kifupi kuanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukraine.

Amesema uvamizi kama huo unaweza ukaanzia kwa kuushambulia Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Huku wasiwasi ukiongezeka, Rais wa Marekani, Joe Biden, leo Jumamosi anatarajiwa kuzungumza kwa njia ya simu na Rais wa Urusi, Vladmir Putin kuhusu kuongezeka kwa mzozo huo. Mazungumzo kati ya Putin na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron pia yanatarajiwa kufanyika.

Hata hivyo, Urusi imerudia kukanusha mipango yoyote ya kuivamia Ukraine. Licha ya kukanusha huko, nchi kadhaa ikiwemo Marekani, Uingereza, Australia, Canada, Norway, Denmark, New Zealand, Japan na nchi nyingine za Ulaya zimewataka raia wake kuondoka Ukraine mara moja.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jen Psaki amewaambia waandishi habari kwamba wanatambua Rais Putin anafanya uamuzi wa kuivamia Ukraine, hivyo kutakuwa na mazingira magumu kwa raia wa Marekani walioko Ukraine.

''Tunataka kuweka wazi hatari iliyopo kwa raia wetu, kwa raia yeyote ambaye atabakia ndani ya Ukraine,” alifafanua Psaki.

Marekani yaihakikishia Ukraine kuhusu uhuru wake
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema vikosi vya Urusi vinaweza kuivamia Ukraine muda wowote.

Akizungumza kwa njia ya simu na waziri mwenzake wa Ukraine, Dmytro Kuleba, Blinken amemuhakikishia kwamba Marekani itaendelea kuiunga mkono uhuru na uadilifu wa Ukraine.

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz amezungumza kwa njia ya simu na Blinken, Macron pamoja na Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, huku viongozi hao wakithibitisha umuhimu wa kuweka vikwazo vikali na vya haraka iwapo Urusi itaivamia Ukraine.

Serikali ya Ujerumani imesema juhudi zote za kidiplomasia ni kuishawishi Urusi kupunguza mvutano, huku lengo kuu likiwa kuzuia vita barani Ulaya. Scholz anatarajia kuelekea Ukraine siku ya Jumatatu kujadiliana hatua za pamoja na madhubuti kukabiliana na vitisho.

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg amesema muungano huo umejiandaa kwa hali yoyote ile.

Ijumaa, wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema Rais Biden ameamuru kupelekwa wanajeshi zaidi 3,000 nchini Poland mbali na 1,700 ambao tayari wako nchini humo, ili kuimarisha vikosi vya NATO vilivyoko huko.

Wanajeshi walioko Ujerumani pia kuhamishwa
Jeshi la Marekani pia linawahamisha wanajeshi 1,000 kutoka Ujerumani kwenda Romania, ambayo kama ilivyo Poland inapakana na Ukraine.

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Mark Milley Ijumaa alizungumza kwa simu na mwenzake wa Urusi, Jenerali Valery Gerasimov. Ofisi ya Milley haikutoa maelezo zaidi kusuhu kilichozungumzwa zaidi ya kusema makamanda hao wawili walijadiliana masuala kadhaa yanayohusiana na usalama.

Source: Reuters

60700758_303.jpg
 
Hapo kwenye simu atakayeongea ni putin tu baiden atakuwa anasikiliza
 
Urusi imeshachoka, ilipaswa wawawai kabla.
 
Hivi Russia kwa akili zao wanafikiri kwamba leo hii kuna nchi wanaweza wakaifanya kuwa koloni lao, kama wanafikiri hivyo watakuwa wanajidanganya sana.

Hawa warusi mwaka 1979 waliivamia Afghanistan na kuikalia hiyo nchi kwa takriban miaka kumi ambapo walilazimika kuondoka baada ya kuzidiwa nguvu na vikosi vya Taliban na Northern Alliance.

Sasa leo tena wanataka waivamie Ukraine kwa kisingizio cha kuogopa Nato kujitanua wakati hao Nato tayari wapo kwenye mataifa mengine jirani nao kama Poland, Jamhuri ya Slovakia, Hungary na Romania, sasa walikuwa wapi wakati hayo mataifa yanajiunga na Nato?

Hatua hiyo ya Russia kuivamia Ukraine itakuwa na madhara makubwa kwao na kama wanafikiria kutumia gesi wanayouza Ulaya magharibi kama 'Tool for Leverage' basi watakuwa wanajidanganya sana kwani nchi za magharibi tayari wameshajipanga na njia mbadala.
 
Marekani imeonya kuwa Urusi inaweza kuivamia kijeshi Ukraine muda wowote. Mshauri wa masuala ya usalama wa Marekani, Jake Sullivan amesema uvamizi huo unaweza ukaanza kwa makombora na mashambulizi ya anga.

Tangazo la Marekani linatokana na taarifa mpya za kijasusi kuhusu kuongezeka kwa wanajeshi wa Urusi kwenye mipaka ya Ukraine katika wiki moja iliyopita.

Akizumgumza na waandishi habari katika Ikulu ya Marekani, Sullivan amesema huo ni ujumbe wa dharura kwa sababu wako katika hali ya dharura.

Amesema Urusi ina majeshi yote inayohitaji kufanya mashambulizi makubwa ya kijeshi na nchi hiyo inaweza kuchagua ndani ya kipindi kifupi kuanzisha mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Ukraine.

Amesema uvamizi kama huo unaweza ukaanzia kwa kuushambulia Mji Mkuu wa Ukraine, Kyiv.

Huku wasiwasi ukiongezeka, Rais wa Marekani, Joe Biden, leo Jumamosi anatarajiwa kuzungumza kwa njia ya simu na Rais wa Urusi, Vladmir Putin kuhusu kuongezeka kwa mzozo huo. Mazungumzo kati ya Putin na Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron pia yanatarajiwa kufanyika.

Hata hivyo, Urusi imerudia kukanusha mipango yoyote ya kuivamia Ukraine. Licha ya kukanusha huko, nchi kadhaa ikiwemo Marekani, Uingereza, Australia, Canada, Norway, Denmark, New Zealand, Japan na nchi nyingine za Ulaya zimewataka raia wake kuondoka Ukraine mara moja.

Msemaji wa Ikulu ya Marekani, Jen Psaki amewaambia waandishi habari kwamba wanatambua Rais Putin anafanya uamuzi wa kuivamia Ukraine, hivyo kutakuwa na mazingira magumu kwa raia wa Marekani walioko Ukraine.

''Tunataka kuweka wazi hatari iliyopo kwa raia wetu, kwa raia yeyote ambaye atabakia ndani ya Ukraine,” alifafanua Psaki.

Marekani yaihakikishia Ukraine kuhusu uhuru wake
Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Antony Blinken amesema vikosi vya Urusi vinaweza kuivamia Ukraine muda wowote.

Akizungumza kwa njia ya simu na waziri mwenzake wa Ukraine, Dmytro Kuleba, Blinken amemuhakikishia kwamba Marekani itaendelea kuiunga mkono uhuru na uadilifu wa Ukraine.

Kansela wa Ujerumani, Olaf Scholz amezungumza kwa njia ya simu na Blinken, Macron pamoja na Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau, huku viongozi hao wakithibitisha umuhimu wa kuweka vikwazo vikali na vya haraka iwapo Urusi itaivamia Ukraine.

Serikali ya Ujerumani imesema juhudi zote za kidiplomasia ni kuishawishi Urusi kupunguza mvutano, huku lengo kuu likiwa kuzuia vita barani Ulaya. Scholz anatarajia kuelekea Ukraine siku ya Jumatatu kujadiliana hatua za pamoja na madhubuti kukabiliana na vitisho.

Katibu Mkuu wa Jumuia ya Kujihami ya NATO, Jens Stoltenberg amesema muungano huo umejiandaa kwa hali yoyote ile.

Ijumaa, wizara ya ulinzi ya Marekani ilisema Rais Biden ameamuru kupelekwa wanajeshi zaidi 3,000 nchini Poland mbali na 1,700 ambao tayari wako nchini humo, ili kuimarisha vikosi vya NATO vilivyoko huko.

Wanajeshi walioko Ujerumani pia kuhamishwa
Jeshi la Marekani pia linawahamisha wanajeshi 1,000 kutoka Ujerumani kwenda Romania, ambayo kama ilivyo Poland inapakana na Ukraine.

Mkuu wa Majeshi, Jenerali Mark Milley Ijumaa alizungumza kwa simu na mwenzake wa Urusi, Jenerali Valery Gerasimov. Ofisi ya Milley haikutoa maelezo zaidi kusuhu kilichozungumzwa zaidi ya kusema makamanda hao wawili walijadiliana masuala kadhaa yanayohusiana na usalama.

Source: Reuters

View attachment 2117221
Russia tayari iliweka majeshi yake zaidi ya 130,000 hadi kufikia mkesha wa christimas, huku nchi zingine za NATO zikiwa zinasherehekea siku hiyo ya kuzaliwa Yesu Kristo.

Ukraine imezungukuwa kila kona na wakati wowote Putin akiamua kunyanyua simu Ukraine itakuwa mikononi mwa Russia.

Leo mchana raisi Putin na Biden wamezungumza kwa simu kwa saa moja unusu bila kufikia mwafaka khasa baada ya Russia kuigundua manowari ya kivita ya Marekani ikiwa ndani yamaji yake katika bahari ya Okhotisk ndani ya maji ya Russia.

Russia ikaiamuru manowari hiyo iondoke mara moja na wanamaji hao wa Marekani wakatii amri hiyo.

Lengo la Moscow na Putin ni kuiondoa serikali ya vibaraka inoongozwa na Volodymiyr Zelensnky ambayo iliingia madarakani kwa kusaidiwa na majasusi wa CIA, NATO na nchi za magharibi mwaka 2019.

Lengo la serikali hii ya vibaraka ni kutumika kuizunguka Russia kiusalama na kuikomboa Crimea jambo ambalo Putin kama jasusi hatari la zamani la KGB aliligundua na sasa analichukulia hatua.

Jambo lililo wazi kwa sasa ni kwamba Russia ikiamua wakti wowote ule kuivamia Ukraine, yaweza kufanya hivyo na NATO, Marekani na nchi zingine za magharibi zitaangalia tu bila kufanya lolote kama ilivyokuwa kwa jimbo la Crimea.

Russia haitaki kuona Ukraine ina kuwa mwanachama wa NATO jambo linoweza kusababisha Russia kutishiwa usalama wake kwa Ukraine kutumika kama daraja la uvamizi.

Hivyo sisi wengine na dunia nzima tujiandae tu kuona mwamba huyu wa Russia akifanya mambo yake ambayo huyatenda kwa nadra lakini yenye ufanisi mkubwa.
 
Russia tayari iliweka majeshi yake zaidi ya 130,000 hadi kufikia mkesha wa christimas, huku nchi zingine za NATO zikiwa zinasherehekea siku hiyo ya kuzaliwa Yesu Kristo.

Ukraine imezungukuwa kila kona na wakati wowote Putin akiamua kunyanyua simu Ukraine itakuwa mikononi mwa Russia.

Leo mchana raisi Putin na Biden wamezungumza kwa simu kwa saa moja unusu bila kufikia mwafaka khasa baada ya Russia kuigundua manowari ya kivita ya Marekani ikiwa ndani yamaji yake katika bahari ya Okhotisk ndani ya maji ya Russia.

Russia ikaiamuru manowari hiyo iondoke mara moja na wanamaji hao wa Marekani wakatii amri hiyo.

Lengo la Moscow na Putin ni kuiondoa serikali ya vibaraka inoongozwa na Volodymiyr Zelensnky ambayo iliingia madarakani kwa kusaidiwa na majasusi wa CIA, NATO na nchi za magharibi mwaka 2014.

Wacha wee! Kama vile upo ndani ya kituo cha KCTV mjini Pyongyang, North Korea ukitangaza taarifa ya habari!
 
Imeeleweka. Unaweza shangaza wengi urusi akafanya kitendo kigumu cha kuvamia ukraine. Mwanzo nilijua chanzo cha ugomvi huu ni lile jimbo la crimea.

Vipi ukraine akijiondoa kwenye mpango wa Nato inaweza leta nafuu?

Nilimuona pia rais wa france vipi mazungumzo hayakuleta muafaka?
 
Russia haitaki kuona Ukraine inaingizwa kwenye NATO ambayo ina mpango wa kujipanua upande wa mashariki ambako ni karibu na Crimea.

Putin akiwa jasusi mahiri na watu wake wamegundua hiyo plan ya NATO (kumpandikiza Zelensky) ili afanikishe Ukraine kuingizwa NATO.

Zelensky ambae kwa asili ni myahudi amesita hatua hiyo na anataka kufanyike kura ya maoni jambo ambalo likatoa mwanya kwa Putin kukusanya jeshi lake kulinda mipaka yote.

Hivyo unavosema Ukraine ikiachana na mpango wa kujiunga NATO kwamba kutaleta unafuu, hilo ndilo moja ya masharti makuu ya Putin hataki nchi ilokuwa sehemu ya USSR iwe pango la NATO, kiusalama si sawa.

Macron nae ana hasira na Putin baada ya Russia kupeleka majeshi yake Bukhina Faso walipoombwa na serikali ya kijeshi ya nchi hiyo, hivyo ana mawili kwa Putin, ila anaungana nae kwa upande wa kwamba Russia lazima asikilizwe madai yake.

Hivyo leo jioni hii Macron, kansela ya Ujerumani, Biden na Zelensky watazungumza tena kutafuta muafaka kwani Russia amemua aingie mazima khasa baada ya kelele na mikwara ya Uingereza ambao hawajafanikiwa kumshawishi Putin.

Halafu, ukumbuke Russia ana lile bomba la mafuta kwenda Ulaya ambapo kuna nchi kama Hungary ambayo imeingia mkataba na Gazprom kupokea mafuta kutoka Russia hadi 2039!

Ndo maana nchi zingine za NATO na Ulaya zinasita kusaidia jitihada za NATO kuisumbua Russia.

Ila safari hii kuna moto mkali sana utoleta matatizo makubwa kwa Ukraine ingawa mwisho wa siku utasikia Ukraine iko mikononi mwa Russia.
 
Russia ataivamia Ukraine, lini hatujui.
Ikishaivamia ndani ya masaa 48 atasimika serikali ya kibaraka wake.Ukraine itanyukwa vibaya sana lakini inatetea uhuru wake.
Nato na jumuiya ya Ulaya nao wamepanga kumuekea Bilionea Raisi Putin vikwazo binafsi.
Pia kutoka 2014 watu zaidi ya 14,000 wameishakufa,toka chochoko za Russia kumdhaifisha Ukraine,baadhi ya majimbo yalio mpakani na Russia kutegemea upande wa kishoka.
 
Putin hataki kuona Ukraine inakuwa kichaka cha NATO na washirika wake.

Kumbuka Russia ni moja ya nchi zijulikanazo kama "world Super Powers" na ana kiti maalum UN na anacho kitufe cha bomu la nyuklia.
 
Hata Ukraine ilikuwa sehemu ya kuzalisha mabomu ya nuclear. Lakini iliyasalimisha kwa Russia baada ya anguko la Soviet.
Russia akate umasikini kwanza kwa wananchi wake badala ya kutumia mapesa mengi kutaka kuwatawala majirani kwa nguvu.Ajifunze kwa China.China ina uchumi mkubwa mno kuliko Russia, na kijeshi inajipambanua pia.
 
Back
Top Bottom