Urusi inaweza kuivamia Ukraine muda wowote, Marekani yatoa angalizo, yataka raia wake waondoke Ukraine

Kama unataka vamia nchi ni Sasa Biden is Altzeimer patient
 
Wamarekani wa kwamtogole.
 
hawa wamarekani walishindwa huko afghanistan mwaka jana tu
RUSSIA kachanga karata zake vyema sana yaani nyie hangaikeni tu
 
Unamaanisha nini kusema Raisi ni kibaraka wa nchi za Magharibi? So Putin anataka kutoa kibaraka wa nchi za Magharibi afu aweke kibaraka wa Urusi ? Ukraine ni nchi huru na ina haki ya kujiamulia mambo yake. Kwenye dunia hii ukiwa mdogo (less strong) utaonewa sana. Ukraine ingeshakuwa ana nukes kwa sasa, Urusi angekuwa na adabu.
 
 
Nadhani Putin ana point kwa mustakabali wa Russia ni kama sisi tulivyoiweka Zanzibar, nakubali kuwa kwanini Ukraine ila kumbuka nchi zinginine zote hizo wenye mpaka na Russia na hasa hapa tuitaje Poland kwa kiasi kikubwa Belarus ni kama eneo la Russia sio tishio kwao tatizo na Ukraine kuna ardhi walikuwa wanagombania na ni nchi kubwa sana yenye mpaka na Russia mpaka mkubwa sana NATO kwenda pale ni kama uchokozi na Ukraine wameanza hizi chokochoko za kujiunga na Nato kwa maana wakijiunga wanakuwa wanalindana na hapo wanaweza kudai sehemu ya Russia. Nadhani hata sisi Burundi au Rwanda wanaweza kuwa sio tishio sana kwetu kama Kenya. Russia ukiwasikiliza kwenye hili wana haki na wao wanatizama future huko mbeleni. Nato waache hizi inatosha wanayoshikilia sio tena kugonga mlango wa Russia kwa kupitia Ukraine. Ukraine ni nchi kubwa sana na inaweza kuja kuwa tishio huko mbeleni kwa Russia, watu wanaona mbali..
 
Wakubaliane wafanye mkataba na Ukraine chini ya mwamvuli wa Umoja wa Mataifa na uridhiwe na pande zote mbili na kila upande ukubali kuheshimu yaliyomo kwenye huo mkataba. That's all.
 
Mkuu, nakupa homework ufanye utafiti Zelensnky ni nani.

Ukipata mawili matatu kuna moja utalikosa ambalo ni ujasusi wake.

Kisha ntakueleza yeye kijasusi ni nani.

Ila nakupa dondoo kwamba kijasusi Zelensky ni apprentice kwa Putin ambae ni master.

Hivyo hii kwa kuanzia ni Master Vs Apprentice.
 
Putin na Russia hawapendi kuona Ukraine yatumika kuwa kichaka cha NATO.

Si wafahamu sehemu zenye vichaka huficha nini?
 
Unahitaji elimu kubwa sana ndugu,juu siasa za Urusi dhidi ya nchi Magharibi
 
hawa wamarekani walishindwa huko afghanistan mwaka jana tu
RUSSIA kachanga karata zake vyema sana yaani nyie hangaikeni tu
Dunia nzima inajua kuwa,NATO kujaribu kutaka kuishurutisha kijeshi Urusi ni sawa na kuonja sumu kwa kuinywa,au kuvaa mabomu ili kuangamiza halaiki ya watu,maana yake watu watakufa na wewe utakufa.
Kwa nje watu wanaona na kusikia toka propaganda za west kuwa Urusi ni wavamizi au wanataka kuionea Ukraine.
Lakini watu hawaoni kama Urusi inalinda mipaka yake ,usalama wake,uhuru wake.
Kwa sababu Yankee anajitahidi sana kulazimisha Nchi nyingi jirani na Urusi zijiunge na NATO ili Yankee apate Barabara ya Moja kwa Moja Hadi Moscow,namaanisha ili iwe rahisi kwake kuichunguza,kuipeleleza,na hata iwe rahisi kuivamia kijeshi Urusi.
Sasa Urusi akili zake zinachaji sana.
Hivyo Wakileta ujinga Putin anaingia Kiev kibabe,na NATO wakitaka vita na Urusi,urusi wako tayari.
kwa sababu kuruhusu Ukraine iingie NATO ni pigo kubwa sana kijeshi ambalo Urusi atakua amepigwa.
Kwa hiyo kwenye kulinda mipaka yake Urusi hataani.
Na kesha sema amechora mstari Mwekundu wakivuka TU,anavamia kweli.
Kijeshi hiyo ni kauli ya mwisho kabisa.
 
Ndugu yangu huyo utamwelewesha Hadi mwezi uishe haelewi.
Hawa Jana movie za akina van Damme,Anold Schwarzenegger na Rambo zimewapoteza kabisa.
Wanaonaga kwamba Marekani haiwezekani na ndio Kila kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…