Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Raisi wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev amesema Urusi inaweza kumaliza vita vinavyoendelea ikipenda kwa kutumia silaha za nyuklia kama ilivyofanya Marekani mwaka 1945. Namna nyengine ya kumaliza vita hivyo alisema ni kwa Ukraine kusita kupokea silaha kutoka mataifa ya nje.
Hayo aliyasema alipokuwa akijibu tuhuma za nchi za NATO kwamba nchi hiyo inatumia silaha zilizopitwa na wakati na mbinu za karne iliyopita.Akasema hilo sio kweli jeshi la Urusi ni la kisasa na linatumia mbinu tofauti za kivita.
Akaongeza kwamba katika vita vyovyote vile hata viwe vita vya dunia vita hivyo humalizwa kwa njia ama ya kukaa mezani na kutiliana saini au kutumia mbinu kama zile ilizotumia Marekani katika vita vya pili vya dunia.