Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

Urusi kaonesha mfano mbaya, Venezuela naye anafuata: Dunia inaanza kuharibika

No.
Kuheshimu mipaka ni jambo la muhimu sana kwa karne hii na zama hizi za sasa. Aidha, Sheria za kimataifa kuhusu mipaka ya kimataifa inafaa sana kuheshimiwa ili kulinda amani na pia kulinda usalama na maisha ya watu. Ubabe wa kuvamia nchi za watu wengine au kujimegea ardhi kwa nguvu kutoka kwa mataifa ya jirani siyo kitu kizuri hata kidogo kwa dunia ya sasa iliyostaarabika.
Sahihi kabisa
 
Kitu cha kwanza ambacho US ilikifanya baada ya kufanikiwa kuteka baghdad na kuangusha utawala wa sadam ililuwa kushusha bendera ya Iraq na kupandisha bendera ya US huku wakiangusha sanam la Sadam.
Umajua kushusha bendera ya nchi na kupandisha ya nchi nyingine ina maana gani?
Tukio lilikiwa live na walipojishtukia wakakata matangazo.
Pumba tupu wewe; leta ushahidi kama kuna ardhi ya Iraq ilichukuliwa na Marekani., Mambo ya wakati wa vita ni tofauti kabisa na matokeo ya vita hiyo linapokuja swala la mipaka ya nchi. Putin keshajitangazia kubadilisha mipaka hata kabla vita haijaisha.,
 
Safi sana Venezuela [emoji1263] kama muna haja yakufanya hivyo nauwezo munao nikiwa kama mpenda amani nawaunga mkono
Nanyie kama mnaweza vamieni tu baadae msije mkaanza kulialia maisha yamekua magumu
Una viashiria fulani vya extremism, hii ni hatari kwa sababu unaweza kurubuniwa au kurubuni watu kuwa mhanga kwa ahadi ya mabikira 72. Pata usaidizi kutoka kwa FaizaFoxy
 
Pumba tupu wewe; leta ushahidi kama kuna ardhi ya Iraq ilichukuliwa na Marekani., Mambo ya wakati wa vita ni tofauti kabisa na matokeo ya vita hiyo linapokuja swala la mipaka ya nchi. Putin keshajitangazia kubadilisha mipaka hata kabla vita haijaisha.,
Iraq si ilikaliwa kimabavu na majeshi ya marekani mpaka leo yapo. Kampuni za kimarekani zikapewa tenda za kuvuna mafuta. Same to afghanistan.
Sasa kuna tofauti gani na anachofanya mrusi. Marekani aliondoa serikali zilizpkuwepo akaweka zake na majeshi yake.
You only see what you want to see. Fungua macho uone.
 
Acha propaganda wewe kama hujui kuwa Obama alitrudisha majeshi yote ya Marekani mwaka 2011. Unaikumbuka picha hii iliyosambazwa duniani kote siku hiyo?

1702700047703.jpeg
 
Rwanda na Burundi zilikuwa sehemu ya Tanzania mwaka gani ?

Maana Tanzania haija wahi kuwa Koloni,bali muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Jua kusama vizuri, post hiyo ilisema "Tanzania ya leo" ikiwa na maana ya kuwa kabla ya "Tanzania ye leo" kuwapo. Elimu ni kitu cha muhimu sana.
 
Acha propaganda wewe kama hujui kuwa Obama alitrudisha majeshi yote ya Marekani mwaka 2011. Unaikumbuka picha hii iliyosambazwa duniani kote siku hiyo?

View attachment 2843754
Lakini baada ya kuikalia kwa muda gani?
Majeshi yote? Mwaka jana Marekani kambi yake ya jeshi imeshambuliwa na drone za Iran pale Iraq. Hiyo habari imo humu.
Juzi tu tena imeshambuliwa. Sasa ni majeshi yite gani hayo?
Haya twende taratibu...
Haya yote chanzo chake ni US.
Wakati akimtuhumu sadam kuwa anaunda silaha za nuclear, UN ilipeleka wakaguzi na sadam alikubali wakague. Hakukuwa na hizo silaha.
Bado Marekani akakomaa. Wakati akipeleka majeshi, baraza la umoja wa mataifa lilizuia kuivamia Iraq, lakini Marekani akiwa wa kwanza ndiye aliyetangulia kupuuzia UN na yeye na UK na Ufaransa wakaivamia Iraq.
Hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yake si Marekani bwana na akawafungulia njia wengine kuwa kumbe UN imaweza puuzwa.
Hizo silaha wala hawakuzikuta Iraq, na bunge la UK mara kadhaa limelaumu serikali ya aliyekuwa waziri zama hizo Bwana Tony Blair kwa kuunga mkono uongo huo na kuivamia nchi ya Iraq ambapo hata hizo silaha hazikuwepo.
Na marekani amekaa pale na makampuni yake wakivuna mema ya nchi hiyo kwa mgongo qa serikali aliyoiweka mwenyewe.
Same thing kafanya Afghanistan.
Same thing kafanya nchi za south America kwa kupindua serikali halali na kusimika serikali za kidikteta.
And the good thing about serikali za America yeye mwenyewe CIA documents kazirelease unaweza kusoma mwenyewe jinsi alivyoshiriki kupindua serikali nyingi za South America na kuweka serikali ambazo alitaka yeye.
Yeye ndiye mwongoza njia ya haya yote. UN imefeli vibaya na yeye ndiye chanzo cha kuifanya ionekane haina maana wala meno ya kufamya chochote.
Haya yanayotokea sasa, ni matokeo ya kile alichokuwa anakifanya kwa miaka mingi sasa na wengine wameiga.
 
Rwanda Ina nini Cha kulingana na tz? Propaganda zao waishie kuwasumbua Burundi tu na congo,hapa kwa tz watayatimba.
Tusiidharau Rwanda eti kwa sababu ni "kanchi kadogo," tunajidanganya. Vita vya siku hizi ushindi wake unategemea sana Ubora/ Viwango vya Sayansi na Teknilojia na ubora wa akili wa akili walizonazo wapiganaji lakini siyo ukubwa wa nchi au wingi tu wa wapiganaji. Mfano mzuri ulio hai ktk hili ni nchi ndogo ya Israeli ambayo inasumbua mataifa mengi majirani zake.
 
Una viashiria fulani vya extremism, hii ni hatari kwa sababu unaweza kurubuniwa au kurubuni watu kuwa mhanga kwa ahadi ya mabikira 72. Pata usaidizi kutoka kwa FaizaFoxy
Ushaanza ku panic wewe kafiri.

Ukweli ni kwamba kama mabwana zenu katika ukafiri wanavunja sheria walizojiwekea wenyewe au wanatetea kuvunjwa kwa sheria walizojiwekea wenyewe huku wakijifanya ni watengenezaji na wabora, kwanini nyinyi mnapiga kelele wengine wanapozivunja kwa namna yao wao?

Au ubabe una watu wake maalum?
 
Tangu UN ianze, Marekani haijawahi kukamata ardhi ya nchi ambayo mipaka yake inatambuliwa na UN ikaibadilisha kwa nguvu ili ardhi ile iwe mali ya US. Uanzishwaji wa UN ilikuwa ni kufanya dunia iwe sehemu ya haki na kuachana na mfumo wa ukoloni wa Berlin Conference
Kwa nini Marekani aliivamia Iraq ?
 
Pumba tupu wewe; leta ushahidi kama kuna ardhi ya Iraq ilichukuliwa na Marekani., Mambo ya wakati wa vita ni tofauti kabisa na matokeo ya vita hiyo linapokuja swala la mipaka ya nchi. Putin keshajitangazia kubadilisha mipaka hata kabla vita haijaisha.,
Kwa nini Marekani aliivamia Iraq ?
 
Hapa kwetu tunauza kwa vipindi vipindi ambavyo haizidi miaka 99. Ikiisha unaruhusiwa kuongeza
 
Urusi imeonyesha mfano kuwa taifa moja linaweza kumega ardhi ya Taifa jingine na kuifanya yake, Venezuela naye sasa anafuata, anataka kumega nusu ya Guiyana ajichukulie. Hii lawlessness itaishia wapi, Je Tanzania nasi tujitwalie Burundi na Rwanda zote kwa vile wakati wa Mjerumani tulikuwa nchi moja?
Mambo ya kuvamiana vamiana na uporaji Urusi ndio kaanzisha ?
 
Back
Top Bottom