Acha propaganda wewe kama hujui kuwa Obama alitrudisha majeshi yote ya Marekani mwaka 2011. Unaikumbuka picha hii iliyosambazwa duniani kote siku hiyo?
View attachment 2843754
Lakini baada ya kuikalia kwa muda gani?
Majeshi yote? Mwaka jana Marekani kambi yake ya jeshi imeshambuliwa na drone za Iran pale Iraq. Hiyo habari imo humu.
Juzi tu tena imeshambuliwa. Sasa ni majeshi yite gani hayo?
Haya twende taratibu...
Haya yote chanzo chake ni US.
Wakati akimtuhumu sadam kuwa anaunda silaha za nuclear, UN ilipeleka wakaguzi na sadam alikubali wakague. Hakukuwa na hizo silaha.
Bado Marekani akakomaa. Wakati akipeleka majeshi, baraza la umoja wa mataifa lilizuia kuivamia Iraq, lakini Marekani akiwa wa kwanza ndiye aliyetangulia kupuuzia UN na yeye na UK na Ufaransa wakaivamia Iraq.
Hakuna hatua zilizochukuliwa dhidi yake si Marekani bwana na akawafungulia njia wengine kuwa kumbe UN imaweza puuzwa.
Hizo silaha wala hawakuzikuta Iraq, na bunge la UK mara kadhaa limelaumu serikali ya aliyekuwa waziri zama hizo Bwana Tony Blair kwa kuunga mkono uongo huo na kuivamia nchi ya Iraq ambapo hata hizo silaha hazikuwepo.
Na marekani amekaa pale na makampuni yake wakivuna mema ya nchi hiyo kwa mgongo qa serikali aliyoiweka mwenyewe.
Same thing kafanya Afghanistan.
Same thing kafanya nchi za south America kwa kupindua serikali halali na kusimika serikali za kidikteta.
And the good thing about serikali za America yeye mwenyewe CIA documents kazirelease unaweza kusoma mwenyewe jinsi alivyoshiriki kupindua serikali nyingi za South America na kuweka serikali ambazo alitaka yeye.
Yeye ndiye mwongoza njia ya haya yote. UN imefeli vibaya na yeye ndiye chanzo cha kuifanya ionekane haina maana wala meno ya kufamya chochote.
Haya yanayotokea sasa, ni matokeo ya kile alichokuwa anakifanya kwa miaka mingi sasa na wengine wameiga.